Uchaguzi 2020 Muleba Kusini inahitaji Mbunge mzalendo siyo kama wakina Dkt. Mode

Uchaguzi 2020 Muleba Kusini inahitaji Mbunge mzalendo siyo kama wakina Dkt. Mode

Mchumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
280
Reaction score
262
Huu wakati ndani ya Chama cha Mapinduzi tunaweza kusema ni muda wa lala salama au muda wa majeruhi na hii inapelekea wananchi wote pamoja na wanaCCM kusubiri ni nani jina lake litarudi na hii macho yote ni kwa majimbo yote Tanzania nzima. Miaka ya nyuma tungekuwa tumeishashangilia ushindi lakini baada ya Amri jeshi mkuu wa nchi Dr Magufuli kuinyoosha nchi pamoja na kuondoa makandokando tuliyazoea kuyaona. Sasahivi chama kimeongeza nidhamu ya hali ya juu kiasi kwamba kupelekea watu wote kukipenda chama.

Leo hii Muleba ni baadhi ya wilaya ambazo zinaongoza kwa umaskini. Hivi tunavyoenda kwenye uchaguzi lazima tujitahidi kuchagua viongozi ambao wana nidhamu ya hali ya juu na wazalendo katika nchi yao. Kwa bahati mbaya naona kuna baadhi ya wagombea wamegombea na ukiangalia tayari historia zao zinawatafuna. Au tufumbe macho tujipe imani kwamba wakiwa viongozi wataenda kuokoka. Je asili yao ya ubadhilifu wa mali za umma itaisha. Nimeshangaa jimbo la Muleba kusini watu wanazungumzia kuwa Dkt. Modestus ambaye ndiye mganga mkuu wa wilaya kuwa huenda akachaguliwa kupeperusha bendera na baadhi ya majina mengine makubwa lakini mimi hapa nitamzungumzia Dr Mode kama kweli viatu vya ubunge vinamtosha?

Dr Mode anadaiwa kupiga hela za bima ya afya (NHIF) zaidi ya milioni 240 za hospitali ya Rubya. Baada ya kupiga hizo hela ilipelekea kusitishwa kwa misaada ya hiyo fund kutoka Netherland baada ya kuona ubadhilifu wa fedha, ikapelekea kutumwa kwa wakaguzi kufuatilia na kuhakiki hizo pesa za miradi. Tunapozungumzia hospitali ya Rubya tunajua umuhimu wake kwa kuwa wilaya nzima hatuna hospitali ya wilaya. Hivyo kitendo cha kuwa na huduma za hafifu nikurudisha nyuma ustawi wa wananchi wa Muleba kwa ujumla. Hii dhambi popote pale alipo inamtafuna.

Dr Mode ni mtu wa visasi je kama akibahatika kuwa mbunge ni kweli ataleta maendeleo au ni kuanza kushughulikia watu walionekana wanampinga. Hii imejidhihirisha baada ya Dr Davy Kansheba ambaye mke wake ni bodi ya wafadhili aliposaidia kugundua wizi huo aliambulia kufukuzwa kama mbwa katika hospitali hiyo. Alipata kibarua kwa sasa anasimamia kituo cha Afya cha Kibanga cha Maisha Mema Foundation. Nafasi ya ubunge ni nyeti inahitaji mtu mwenye mapenzi ya dhati na moyo kwa ajili ya kuisaidia jamii yake siyo kwa ajili ya kujilimbikizia mali mwenyewe.

Kwenye kura za maoni aliambulia kupata kura 179 je hizo kura alizipata vipi? Alitumia nafasi yake ya kuwa Mganga Mkuu wa wilaya(DMO) kuwalazimisha na kuwatishia watendaji wa vituo vya afya kumtafutia kura na kuwachangisha gharama za uchaguzi kwa lazima. Kwenye bodi ya Kaigara health Centre ambao hawakumuunga mkono kwenye uchaguzi waliishia kufukuzwa na hii tumeona kwa Alhaji Hussein. Huu siyo wakati wa kuwa na viongozi wa kariba ya Dr Mode tunapoingia kwenye mchakato wa mabadiliko ya kiuchumi.

Tunaamini watu wa dizaini ya Dr Mode hawafai maana wao baada ya kuleta umoja wao wanaeneza chuki. Tukimpata kiongozi ,makini hata tutakapoenda kwenye uchaguzi wa jumla tutakuwa na nafasi nzuri ya kushinda kwa kuwa hatuna watu wenye mambo ya ovyo ovyo. Tusirudie makosa kama ya zamani ya kuwapa watu nafasi ambao hawakubaliki na kuwapa upinzani fimbo ya kuchapia. Kwenye kampeni tutatumia muda mwingi kumsafisha mtu wa ovyo badala ya kunadi sera zilizopo kwenye ilani yetu. Naitakia kila la heri kamati kuu ya Chama itupatie mtu msafi mwenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko kimaendeleo. Ni heri tukawapata hata watu waliopata kura kama namba za viatu kuliko kubeba watu kutokana na idadi zao kubwa za kura walizozipata kupitia mlango wa nyuma.

Niwatakie uchaguzi mwema.
 
Tunawaombea mtoane macho kabisa kama alivyo sema musiba
 
Nadhani tuwe na machache ya kuongea, Mm najua hizi tuhuma kwa Dr Mode zinalenga kumwangusha kisiasa nimejiuliza mengi juu ya huyu aliyepost, Rubya ni hospitali kubwa je iliwahi kulalamika juu ya Dr Mode kufanya wizi?

Je, mlalamikaji ndo umetokea wapi maana wewe si mtumishi ndani ya hospitali ya Rubya, je ushahidi wa hela za NHIF kuliwa na Dr Mode unao?

Nadhani tusiongee kwa kuwa mdomo ni mali yako, Huwezi kuwa umekula milioni 200 na zaidi alafu taasisi ikakuacha pasipo mkondo wa sheria kuchukua nafasi yake. Hii nchi inao utaratibu wake wa kushughulika na mtu, Dev punguza kutafuta umaarufu wa kuchafua wengine.

Nadhani mtoa hii mada lete na ushahidi wa kile ulichoongea hili nasi tuamini unachokisema. Tofauti na hapo usichafue mtu acha kila mtu apambane kivyake kwenye ulingo wa siasa, mchafue mtu kwa kile alichokitenda, Tunajiuliza Dr Mode kapita Kagondo hospital, Rubya hospital na sasa ni mganga mkuu wilaya hiyo hiyo ya muleba, kama hatujasikia kesi yoyote ndani ya wilaya juu ya huyu mtu zaidi ya kupambana kuboresha vituo vya Afya.

Hayo mengine wana muleba hatuyajui ww unayeyajua nenda mahakamani! Kesi ya msingi ikiwepo ya yy kujibu basi tutaamini unachokisema, alafu si msemajin wa NHIF, kama nayo haijahusika naye basi ujipime ww mtoa hoja juu ya Dr. Mode.

Tengeneza propaganda nyingine hii wanaikubali wajinga tu, mwenye akili anacheka tu na haina maana, wagombea hatuwapimi kwa mashtaka ya hewani kwenye media. Hata kule Dodoma hakuna anayesema Dr Mode hili achaguliwe lazima tujue media imeandika nini ndo tumpitishe.

Wana Muleba tunasubiri CCM Dodoma ipitishe mtu aliyesahihi kwa maendeleo ya muleba! Tusipoteze mtu sahihi kisa propaganda kama hii! Asante
 
Back
Top Bottom