Mulugo awataka wanafunzi kutotembelea JF

Mulugo awataka wanafunzi kutotembelea JF

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
13,786
Reaction score
2,095
Akihojiwa mapema leo na wapo FM kasema ataongoza msako wa wanafunzi wanao miliki simu nakuperezi FB na JF kwani hawaruhusiwi kutumia simu.

Serikali imewaagiza wakuu wa shule za sekondari nchini kuchukua hatua kali dhidi ya wanafunzi watakaobainika kumiliki simu za viganjani na kuwanyang'anya na kisha kuziteketeza kwa moto au kuzitupa chooni.

Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo, wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanika katika kijiji cha Totowe wilayani chunya.

Alisema sheria haiwaruhusu wala kuwapa haki wanafunzi kumiliki simu wakiwa shuleni, hivyo mwanafunzi anayekwenda na simu shuleni anakuwa amevunja sheria na taratibu za shule ambazo zinamzuia kumiliki na kutumia masomoni.

"Nawaagiza walimu kuwa ukimwona mwanafunzi ana simu na kuitumia nyakati za masomo, mnyang'anye na kuichoma moto au kuitupa chooni kwa sababu wakati mwingine simu hizo wanakuwa wamenunuliwa na wapenzi wao na hivyo kuwafanya washindwe kusoma vizuri na matokeo yake wanafeli mitihani, sisi Wizara ya Elimu hatujaruhusu na wala hatufanyi hayo mambo," alisema Mulugo.

Alisema akitokea mzazi akalalamika au kumsumbua mwalimu kutokana na kunyan'anya mwanae simu akiwa shuleni, maofisa watendaji wa vijiji na mitaa wamchukulie hatua za kumkamata na kumpeleka Polisi ili afikishwe mahakani.

Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe wilayani Chunya, alisisitiza kuwa wanafunzi wakiachwa bila kudhibitiwa nidhamu zao, ndio cha kushindwa kusoma na kupata matokeo mabovu kwenye mitihani ya kitaifa na baadae kuharibikiwa kimaisha.

Alisema vijana ambao hawadhibitiwi nidhamu wawapo shuleni ndio wanaoshindwa kufanya vema masomo yao na baadaye kuwa mzigo kwa taifa kutokana na kujihusisha na mambo ya hovyo kama vile maandamano yasiyo na tija, utumiaji wa dawa za kulevya na uhalifu mwingine kwenye jamii.

Aidha, Mulugo aliwataka walimu kuanza kutembeza bakora kwa wanafunzi watukutu ili kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi inarejea mashuleni na kuwafanya watoto warejee kwenye masomo badala ya kujihusisha na mambo ya hovyo.



CHANZO: NIPASHE
 
Ahahahaaaaa Tanzania ni muungano wa tanganyika na visiwa vya ZIMBABWE pumbavu kabisa lile limeona JF panamuumbua kilaza mwizi wa vyeti mkubwa.
 
Hahaha kwa hiyo msako utaendeshwa humu ili wanafunzi wasiperuzi huku?
 
Lol....wÁlimu hamna,maabara hamna,mazingira ya kufundishia mabovu,mishahara midogo!!adili kwanza na hivo sio dealing with perceptions!!Na huyu si ndo anatoa propaganda vikobo vmerudishwa kwan vilifutwa lini?Lol..big mburula

LSent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
aiseeeeeeee.......??????????!!!!
 
Singapore mbona wanafunzi wanapewa website wakajisomee- tutafika lini. Waweke vitu muhimu kwenye mitandao. Pili juzi mtoto wa waziri Fulani alizindua mtandao
 
Kwani kulikuwa na mada gani hata ahojiwa na WAPO FM? Kwa maoni yake, mhh...inaweza kuwa hatari, kwani mshambiliaji anakuwa mkabaji. Huyu mtu anatapatapa tu. Tunahitaji mfumo wa Elimu ufanyiwe mabadiliko makubwa. Natarajia tume ya Pinda itasema hivyo.
 
Huyu jamaa ni kilaza sana. Napata. Aliyemteua hayupo makini
 
Kama hayo maneno kayasema Mulogo sishangai. Yanafanana kabisa na yeye.
 
Hamimu nae anakwama kimawazo sasa

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ahahahaaaa kumbe jina lake Amimu?ahahahaaaaa mbwa mkubwa mwizi wa vyeti sijui kaibaje uwaziri?loooo!!

Ahahaha.......now I understand why the guy was appointed and why still he z holding the office.....his Name right?amimu ....
 
Sasa ile web ya Mrs. Nyalandu wataionaje wanafunzi???
 
Huyu ni zaidi ya kilaza.na aende akakae nao makwao.mmmxxxxxxiiiiiiiuuuuuuu
 
Back
Top Bottom