Mulugo: Wizara kuwafanyia wanafunzi asilimia kazaa ya mtihani ili kuongenza ufahulu

bnf

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
218
Reaction score
79
ALAMA ZA UFAULU KIDATO CHA IV TOA MAONI

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatarajia kubadili alama za ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha Nne ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi wanaomaliza kidato hicho kuingia Kidato cha Tano.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanaomaliza kidato cha Nne wanashindwa kuendelea na masomo ya kidato cha Tano licha ya kuwa na uwezo mzuri wa kitaaluma.

Mulugo ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na Star Tv kabla ya kuufunga mkutano wa mwaka wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania, TAMONGSCO, jijini Mbeya.

Baada ya mazungumzo haya, Mulugo, anakwenda kuzungumza na wajumbe wa mkutano huo na kupata fursa ya kubainisha sababu za kuifikia hatua hiyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa TAMONGSCO Taifa, Mahmoud Mringo, baadhi ya maagizo yanayotolewa na Serikali katika uendeshaji wa elimu nchini ni kikwazo cha maendeleo ya sekta hiyo.

Baadhi ya wamiliki wa shule,wanasema umefika wakati kwa Serikali kutoa ruzuku mashuleni.

Mkutano huo wa siku mbili uliowahusisha wamiliki wa shule na vyuo binafsi kutoka mikoa yote nchini umeakisi changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini ili kuboresha sekta hiyo.

Source: Habari Star TV Tanzania
 
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi inatarajia kubadili alama za
ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha
Nne ili kuwawezesha wanafunzi
wengi zaidi wanaomaliza kidato
hicho kuingia Kidato cha Tano.


Hii ni kama kuchapisha pesa nyingi zaidi ili uchumi weyu uongezeke!
 
Nafikiri pia hivi karibuni kila mtu atakayemaliza kidato cha sita atapewa PhD ili kuonekana kuwa tuna wataalamu wengi nchini. Wameshaanza, siku hizi kila mtu ni daktari, wengi wao hawajawahi hata kuandika makala ama kutoa mada kwenye semina (seminar paper/presentation). Anayesema haya ni yule Naibu Waziri asiyejua Tanzania ni muungano wa nchi zipi!
 
kama ni kweli kayasema haya, basi itakua kabla ya kuropoka alivuta majani flani hivi au kuna vitu vyeupe alilamba lamba, sio bure!
 
Bwana Amimu kilaza huyu,kwa hyo kama wana uwezo wa kusonga mbele iweje wafeli mitihani yao?
 
Aisee!Huyu jamaa kama kupata uwaziri ingekuwa kwa njia ya kufanya pepa,lazima angeshika mkia tu,uwezo wake wa kifikra ni kama mtu aliyezaliwa bila kuwa na ubongo kabisa.
 
Hii Wizara sijui ina mkosi gani. Mtu akiamka tu na hangover zake analeta mabadiliko yasiyo na uelekeo. Kuna mtu alikuja akafuta mitihani ya Fm 2 mwingine akairudisha, mwingine akafuta masomo ya michepuo, mwingine akairudisha, mwingine akaunganisha masomo ,mwingine akayatenganisha, mwingine akaondoa viboko, mwingine anataka kuvirudisha. Kuna aliyekuja kuseme wanafunzi wafanye sayansi za kuaririshana 'alternative to practicals' sijui nani atafuta huu ujinga. Leo huyu nae kama atashusha alama za 4m4 division 4 ataifanya Tanzania kuingia kwenye kitabu cha maajabu.
 
Naogopa kuchangia manake ni kama haiingii akilini coz' i know njia ya kuongoza ufaulu sio kupunguza pass mark....
 
Hii itafaa kwani idadi ya wanafunzi wa mwaka huu ni wachache sana ambao watajoin 4M5 so atleast hii itasaidia.
 
kama ni kweli kayasema haya, basi itakua kabla ya kuropoka alivuta majani flani hivi au kuna vitu vyeupe alilamba lamba, sio bure!

Mkuu si vyema kupinga kila kitu acha serkal mda mwingine ifanye kazi yake.
 
kama vipi basi waweke ukipata kuanzia sifuri na kuendelea mwanafunzi awe amefaulu..
 
Naogopa kuchangia manake ni kama haiingii akilini coz' i know njia ya kuongoza ufaulu sio kupunguza pass mark....

dA Inauma sana leo ukikutana na darasa la nne la mkoloni likiwa na knowldge ya master ya leo.
 
Si wadogo zao std 7 walishusha! Wamenogewa
Hivi ukipunguza alama ndio umeongeza ufaulu au mimi sielewi. Hakika si sawa. So na mwaka huu wakifeli watashusha hadi zibaki 0
 
waziri amegushi elimu sasa wanafunz c lazma division 0.
 
tatizo elimu yetu tunajali quantity na sio quality ndio maana tumeongeza shule za kata bila kuwa na walimu au vifaa vya kutosha ni heri tuwe na wanafunzi wachache wenye ubora unaoridhisha kuliko kuwa na wanafunzi wengi lakini kichwani hamna kitu
 
tangu lile povu la tanganyika na zimbabwe ni muda umepita achani aendelee kutoa povu!
 
Tatizo la elimu yetu sio pass mark tu. Ni majumuisho ya mambo mengi kuanzia mitaala, waalimu na mazingira ya shule zenyewe.

Waziri azingatie hayo, sio kukurupuka tu kisiasa.
 
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatarajia kubadili alama za ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha Nne ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi wanaomaliza kidato hicho kuingia Kidato cha Tano. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanaomaliza kidato cha Nne wanashindwa kuendelea na masomo ya kidato cha Tano licha ya kuwa na uwezo mzuri wa kitaaluma.

Mulugo ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na Star Tv kabla ya kuufunga mkutano wa mwaka wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania, TAMONGSCO, jijini Mbeya. Baada ya mazungumzo haya, Mulugo, anakwenda kuzungumza na wajumbe wa mkutano huo na kupata fursa ya kubainisha sababu za kuifikia hatua hiyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa TAMONGSCO Taifa, Mahmoud Mringo, baadhi ya maagizo yanayotolewa na Serikali katika uendeshaji wa elimu nchini ni kikwazo cha maendeleo ya sekta hiyo. Baadhi ya wamiliki wa shule, wanasema umefika wakati kwa Serikali kutoa ruzuku mashuleni.

Mkutano huo wa siku mbili uliowahusisha wamiliki wa shule na vyuo binafsi kutoka mikoa yote nchini umeakisi changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini ili kuboresha sekta hiyo.

Source Star TV

My Out Look

Mulugo Tuache na Elimu yetu, we Malizia Bata Miaka miwili hii uliyobaki Kabla Hujachinjiwa Baharaini Mazima na MakamandaTukikamata Nchi
Mia
 
Jamani......huu ni US&GE sasa,ati....

(Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanaomaliza kidato cha Nne wanashindwa kuendelea na masomo ya kidato cha Tano licha ya kuwa na uwezo mzuri wa kitaaluma.

Mulugo ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na Star Tv kabla ya kuufunga mkutano wa mwaka wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania, TAMONGSCO, jijini Mbeya.

Baada ya mazungumzo haya, Mulugo, anakwenda kuzungumza na wajumbe wa mkutano huo na kupata fursa ya kubainisha sababu za kuifikia hatua hiyo.)

........huu ni US&GE!
 
Mkuu si vyema kupinga kila kitu acha serkal mda mwingine ifanye kazi yake.


Naomba kukuliza, Serikali imefuta mitihani ya Elimu ya Msingi na Kiato cha Pili ili wanafunzi wengi wafike Kidato cha Nne, je unaweza kutuambia mafanio yake?
Tanzania ni kama mwendawazimu, na Wizara ya Elimu ndio kichwa. Kwa kuwa mwendawazimu amekosa ulinzi, kila mtu aliyepata nafasi kidogo ya kumshika kichwa, amenyoa kwa mtindo autakao. Hatiamaye duia inataka kuamini ya kwamba wote ni machizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…