Mume ajiua baada ya mkewe kumnyima pesa ya kunywea pombe

Mume ajiua baada ya mkewe kumnyima pesa ya kunywea pombe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
James Kamau mwenye miaka 39 mkazi wa kijiji cha Mbogo-ini kilichoko katika kata ya Kahumbu kaunti ya Murang'a nchini Kenya, amejiua baada ya kunyimwa pesa ya kwenda kunywa pombe na mke wake .

KUJINYONGA.jpg


Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa Murang’a, Josephat Kinyua amesema kwamba mwanaume huyo baada ya kutoka kwenye shughuli za kila siku alizokuwa akizifanya, alipitia bar na rafiki yake na kuanza kunywa pombe huku yeye akiwa mlipaji, lakini alipomaliza pesa alirudi nyumbani na kutaka mkewe ampatie pesa nyingine.

“Inaarifiwa kuwa Bw. Kamau alirejea nyumbani kwao ambapo watoto wao watatu walikuwa usingizini, alizua fujo akitaka apewe pesa kwa lazima, baada ya mama yake kusikia vurugu hizo, alimchukua mke wa Kamau na kumpa malazi", amesema Kamanda Kinyua

"Kwa hasira, Kamau alisikika akimuonya mama yake kuwa alikuwa na upendeleo kwa mkewe na akaapa kuwaadhibu wote wawili kwa maombolezi kisha akafunga mlango. Asubuhi yake watoto walipoamka, wakamwona baba yao akining’inia kutoka kwa paa la nyumba sebuleni, ameongeza Kamanda.

Taarifa zaidi zinasema kwamba baada ya tukio hilo walitoa taarifa polisi, na kukuta tayari mtu huyo ameshafariki, na kuchukua mwili kwenda kuuhifadhi katika hospitali ya Murang’a.
 
Ndio Akili Za Wakenya?
Mbona Wachagga Na Ujanja Wao Wa Kupenda Pombe, Hawana Hizi? Unajiua Kweli? Kwani Hatujitathmini Tukajua Hata Utamu Wa Ugali Tu, Tufaidi Aisee?
 
Back
Top Bottom