Mume amkata mke wake mikono kwa kutokuzaa watoto

Mume amkata mke wake mikono kwa kutokuzaa watoto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
9ecbf182b1e5f23a79f6b2af53fc00b0

MAMA mmoja chini Kenya amekatwa mikono yote miwili na mumewe kwa kutumia kisu akidai kwamba ameshindwa kumzalia watoto, katika kile kinachosemekana ni tukio baya zaidi la ugomvi wa nyumbani.

Mama huyo ambaye ni Jackline Mwende mkaazi wa kijiji cha Kathama , Kaunti ya Machakos amedumu katika ndoa na mume wake huyo kwa miaka saba.

Mikono yake ilikatwa kutoka katika kifundo cha mkono na mumewe Stephen Ngila Thenge na pia ana majeraha kichwani na shingoni kutokana na shambulio hilo Julai 24 mwaka huu.

Ndugu zake wamesema kuwa wanandoa hao walikuwa na matatizo na kwamba bi Mwende alitaka kumwacha mumewe, lakini akashauriwa kutofanya hivyo na kiongozi mmoja wa dini.

Mwende amesema kabla ya shambulio hilo, walikuwa wakiishi mbalimbali na mumewe kwa takriban miezi mitatu kwa kosa la kutopata watoto.

”Sijui kwa nini aikuwa akinilaumu licha ya sisi sote kwenda hospitalini mwaka uliopita na kwamba daktari alisema kuwa ni yeye aliyekuwa na tatizo la kuzaa ambalo linaweza kurekebishwa”.

Amesema kuwa mumewe ambaye ni mshonaji nguo katika mji wa Masii, alikataa kufuatilia matibabu
 
So sad,wadada zetu mnaokimbilia kuolewa Kenya haya matukio naona sasa yanafikirisha...!
 
Dah! So sad [emoji17]
Sijui wazazi wa mama huyo wamejisikia uchungu wa aina gani.
 
wakenya wana roho mbaya sana kama wa afrika kusini anyway nisijaribu kutoa kibanzi ndani ya jicho la ndugu kumbe mimi nina boriti ila majirani kuweni na soft hearts na romantic kwenye mahusiano
 
Huyo mende anastahili adhabu ya kukatwa mikono,miguu na kende stupid kabisa.
 
Sasa kwani i asiende kuzaa nje au asimuache nadhani kuna tatizo halijagundulika , kwenye mahusiano watu wemhi wameshindwa kuona alama za kuishi na wagonjwa wa akili hili mo moja tu ya matukio mengi yanayowakumba wanawake Africa .....
 
Unaweza ukachagua rafiki au mchumba, lkn si jirani.
 
Ila watu wanasema Tanzania wanaume ni wanyanyasaji, hawajawahi kwenda Kenya. Huku kuna matukio ya unyanyasaji sana kupita maelezo.

Na naaambiwa hakuna wanaume romantic kama wa Tanzania hapa east Africa........ Sema tu hela hatuna.


Ila huyu mbweha aliyemfanyia hivi huyu mama, kubabake nimemtamani kifucker...... Yaani ni wakumtia mbaroni na kumpa kinyuko cha maana.
 
Back
Top Bottom