Mume amtafuna mke wake mdomo za sikio

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

NAIROBI,KENYA

MWANAMKE wa miaka 39 mkaazi wa Tanga Kona, Kenya anauguza majeraha baaada ya mume wake kumnyofoa mdomo na sikio kufuatia ugomvi baina yao.

Jackline Kerubo, mama wa watoto sita, alisema alitaka kwenda kuchuma mboga katika shamba la jirani yake lakini mume wake alimkataza.

Kerubo ambaye ni mume wake aliyefunga naye ndoa miaka 21 iliyopita, anasema kwa sasa anahofia maisha yake pamoja na watoto wake.

Alisema jirani yake aliingilia kati baada ya mume wake kuapa kumpa fundisho . Hata hivyo baada ya kipigo hicho Mume wake alitoweka nyumbani.

Akizungumza na waandishi wa habari, alisema mume wake alitenda unyama huo akiwa jikoni kwa kumpiga kichwani na baadae kumtafuna mdomo na sikio.

Mkuu wa Polisi Maryline Oundo aliwaomba wanandoa kutafuta ushauri wanapokuwa na mizozo na kuitaka jamii kutoa taarifa za kesi zinazokiuka haki za binadamu ili kupata msaada sambamba na watuhumiwa kuchukuliwa hatua.

Bi Kerubo kwa sasa anapatiwa hifadhi katika kituo cha polisi Nambale wakati maafisa polisi tayari wameanza kazi ya kumtafuta mtuhumiwa.
 
Kenya, Wanawake si wanapiga wanaume???

Anyways mwanaume ukimchoka usidharau huku unaishi nae nyumba moja,maamuzi yanatokea baaada ya mwanaune kudharauliwa na mkewe uwaga mara nyingi ndo tunaita ukatili wa kijinsia...

Ingawa kuna wanaume vichaa wengi ila wengi wao vichaa vinapanda baada ya utii kupungua na dharau kuongezeka..
 
Huyo mwanaume adhabu yake wakimkamata wasimfunge,wamrudishe kwa mkewe ili aishi naye hivyo hivyo alivyo maana wakimfunga watakuwa wamempa nafuu,akae naye huyo mwanamke bila ya mdomo na sikio bila kumuacha,hiyo ni adhabu tosha kwake,condition ni kuwa asimuache mpaka kifo kiwatenganishe......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…