Mume anapokutenganisha na ndugu…………………………..

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Kuna wanaume ambao hawataki kabisa kuona mke akiwa na uhusiano wa karibu na ndugu zake (mwanamke). Hataki kabisa kuona mkewe akionyesha kuwa na mshikamano mkubwa sana na ndugu zake. Inawezekana mara nyingi ni hofu ya mwanaume huyu kwamba mshikamano huo unaweza kumvurugia uhusiano wake na mkewe. Hakuna sababu inayoweza kuelezwa wazi kwamba ndio matokeo ya jambo hili.

Kutokana na hofu hiyo, mume hutunga sheria na kanuni ngumu akijaribu kuvunja uhusiano huo na ndugu zake. Lakini tabia hi huambatana pia na mume kutotaka mkewe kuwa na marafiki wa kike. Kila wakati atakuwa anawakosoa marafiki hao na mwisho atamkataza mkewe kufuatana nao bila kutoa sababu ya maana kuhusu kuwakataza kwake huko.

Kumbuka katika kupinga kwake uhusiano wa karibu kati ya mkewe na ndugu zake na marafiki atakuwa anajaribu kutumia kauli zisizofaa, na hata nguvu. ‘Ndugu zako wenyewe hawaeleweki, wanaonekana watu wa majungu tu,' atasema, au ' siku nikikuona tena na yule rafiki yako, utanitambua .' Na kweli anapomuona naye humtambua. Ni kweli kuna wanaume ambao hujaribu sana kadiri wanavyoweza kuwadhibiti wake zao.

Hufanya hivyo kwa kujigeuza kuwa mabosi badala ya kuwa waume. Unakuta mwanaume ndiye mwenye kauli ya mwisho kwenye kila jambo bila kuomba ushauri wala kuusikiliza, utakuta kazi yake ni kutoa amri bila kujali upande wa pili, yaani kujali kuhusu hisia za mkewe, atakuwa ndiye mwenye kufanya maamuzi yote yanayohusu familia bila kujali au kusikiliza upande wa pili. Mume wa namna hii huwa hayuko tayari kusikiliza maoni ya mwenzake wala ushauri.
 
kuna wanaume na magugumaji,wa aina hii ni magugumaji! hao ndio ndugu zangu mungu alonipa niwakane !!!
 
ukiona hivyo ujue mke ana tatizo
 
Alafu BPM you are a really Great Thinker. Wanaume wengi wanafanya hayo kutokana na mambo mengi, kwanza ikiwa hana imani na mkewe, au mke wake anatabia zisizoridhisha, au mme alishashuhudia tabia chafu kama uongo au umalaya kwa mke, marafiki wa mke au ndugu zake au kama aligundua kuwa kabla hajamuoa huyu mke ndugu zake walikuwa wanamtafutia wanaume.
 
ukiona hivyo ujue mke ana tatizo
Kwa kuwa ni vyema tukijifunza wote, ingekuwa ni vyema kama ungeainisha hayo matatizo ili wajirekebishe..............
 

Hizi sababu zote ulizozieleza hapa ni za mwanaume ambaye HAJIAMINI kabisaaaa................. yaani huyo ni mgonjwa na anaogopa hata kivuli chake.
 
kutokujiamini kwa mume. Na mke ukimfuatisha aina ya hili janaume itakula kwako
 

hapa kaka ukiona mwanaume ana hofu hz. Hajiamini au mzinzi anahofia kushtukiwa
 
Mtu aweza kuwa ndugu wa mke wako , lakini ni mshenzi kupindukia!
Kwa kawaida msichana baada ya kuolewaa anakuwa na limits za frequncy za kuonana na nduguze, kama at all itahitajika afanye hivyo.
Ndugu wanini kuonana nao kila siku wakati una mji wako, na mambo ya nyumbani kwako hujayamaliza?...
Kwa msichana aliyeolewa, hana sababu critical ya mawasiliano tight na wanafamilia wake, maana kama kuna issue ya attention ni lazima na mume ahusike!
Kwahiyo hata mimi siwezi kuruhusu UPUMBAVU wa mke wangu kuambatana na nduguze kila uchapo, ni lazima atazalisha ya kuzalisha ndani ya magenge hayo!
Ukiolewa kubali kukaa kwa mumeo, na hata Bible inasema kuwa ...Mke atamwacha Baba na Mama yake, ataambatana na mumewe, nao watakuwa mwili mmoja!
 
totally agree with u. sasa je, na mwanaume nae kuambatana na marafiki zake na nduguze ni busara ama? automatikale kama mume anajishughulisha sana na mkewe, muda mwingi mwanamke atakua yuko occupied na mumewe. lakini tukubali ama tukatae, ni vizuri kuhakikisha kuwa wote mume na mke wana-maintai mahusiano na mawasiliano mazuri na ndugu na marafiki wa pande zote.
 
Huyu mwanaume anakuwa ni mbinafsi na ana roho mbaya, kwan yeye ndugu zake hana ukaribu nao,yeye hana marafiki, na siku mume hayupo na mke amepata tatizo aende wapi wakati hana ukaribu hata na majiran wanaume wa hivi ndio wanafundisha wake zao tabia mbaya, kwan mke nae atatafuta namna ya kuwa na ukaribu na wanawake wenzie na ndugu zake pia, mwisho wa siku anaonekana hana heshima kwa mume,kwann mwanume usijiamini yani mpaka mwanamke anajuta kuolewa nawe, acheni hizo bwana.
 
Ni mwanaume atawaacha wazazi wake ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja, kwa hiyo mwanaume sanbabu yuko strong anaweza ishi mbali na wazazi wake ila mwanamke anahitaji ndugu zake karibu, mbona nyie mnakuwa mnaishi kabisa nao hao ndugu sie kutembelewa tu imekuwa issue
 

Ahsante kwa kunisaidia kumjibu huyu jamaa................ swala hapa sio mke ana ukaribu gani na nduguze au marafiki zake, nilichosema ni ile tabia ya mume kumdhibiti mkewe afanye kila kitu kwa matakwa yake yeye mume............. hii haiwezekani............. kama kuna marafiki au ndugu wanampotosha, hilo ni swala la kulijadili nyie wanandoa na kukubaliana namna ya kuwa-handle hao ndugu au marafiki na sio kupiga marufuku.
 
Kua uone mjukuu wangu

Nina familia na mke wangu amezungukwa na ndugu na marafiki wa kila aina, lakini yeye kama binadamu kamili anavyo vipaumbele vyake, na anafahamu mipaka yake........... kama hajitambui kama yeye ni nani ana wajibu kiasi gani katika familia, basi huyo hafai kuwa mke wangu.
Jambo moja ambalo wengi hatulijui ni kutaka kuwadhibiti watu wengine............. kwa nini? kila jambo katika ndoa ni vyema likajadiliwa, mambo ya kuamrishana kama mtu na bosi wake huo ndio unaitwa mfumo dume.
Mke ni binadamu kamili ambaye ana utashi wake na anajua malengo yenu, kinyume na hivyo, basi huyo hafai kuitwa mke............. kwa nini nitaabike kumlinda mtu mzima na akili zake, kwani yeye ni mtoto mdogo?
 

Waelezee Bibie.......................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…