Mume asie tosheka na shoga asie fadhila.

arabianfalcon

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
2,285
Reaction score
584
Kwenu wana JF,
Kuna jambo limenikita kwenye roho, niko na mdogo wangu ana mumewe wana watoto wa4 lakini mume wake tabia yake sio nzuri,
Mkewe alipo kwenda nyumbani kutembea rafika wa mdogo wangu wa kike alienda nyumbani kwa mdogo wangu kumuomba shemeji
Eti hana sehemu ya kukaa anaomba ampe hifadhi,yule shemeji bila hata kumuliza mkewe kamkaribisha yule dada akawa ndio mpishi
Na sijui kama mengine pia alikua hafanyi,mdogo wangu amekuja kuambiwa na mwanae kama aunty yuko hapa since last month,
Mdogo wangu kumuliza mumewe anasema unajua ww uko mbali je nikiumwa huyu si ndio atanipeleka hospital, ww uko mbali,
Sio kama anaumwa mzima,zaid anasema mke wangu mm sina nia mbaya na ww usisikilize watu huyu akipata kwake ataondoka.
Huyu dada asokua na haya hata hakuona haya sijui lengo lake nini,wana Jf naomba msaada wenu kwenye hili.
 
kweli tamu ya chai sukari!!! Na kila mmoja ana vijiko vyake vya kuweka ndio ikolee
 
Labda hawana mawasiliano mazuri kwenyr ndoa yao!Siwezi kuimagine hata ndugu yangu alete mtu kukaa kwangu wakati sipo bila kunitaarifu...achilia mbali mume ambae anapaswa kuwa ubavu wangu wa pili.Na aliyekaribishwa rafiki yake...nae akashindwa kumuomba rafiki yake anaenda moja kwa moja kwa mume?!

Hata kama hawana mahusino wote hawamheshimu huyo mdogo wako hata chembe!!!
 
Rafiki mnafiki plus mume asiye na heshima wala ustaarabu! Huyo rafiki alishindwa nini kumwambia mdogo wako hadi aende direct kwa mume? Eenhee.....na huyo shemeji yako alishindwa nini kumtaarifu mkewe kama kweli anamheshimu? Huyo mdogo wako akirudi ndo ataujua ukweli mi naona hapo wanampiga danadana tu!
 
Mwanaume huyo katoa sababu za kipuuzi sana...inawezekana wakawa wanafanya mchezo mchafu.
 
Nadhani chezo lote linalochezwa hapo, huyo man analijua vizuri kwani yeye ndiye aliyekubali kumkaribisha huyo mdada.
 
siku hizi kuna kamsemo ya kuwa acha tubanane tu...mambo ni magumu lakini.....there is no free lunch.........................
 
Huyo jamaa anatuaibisha lakin huwezi jua yaweza kuwa pamoja na kuoa ilando tabia yake
 
Shosti nimemueleza hivyo hovyo nika mwambia kama angenifanyia mie ningeshamaliziana nae, shoga yake ndio hata cm kumpigia mwenzie siunajua shoga wengine kaona mwenzie ana pasport ya Obama sasa na yeye anaitaka kwa nguvu.
 
kwa kuwa akili ni nywele na kila mtu ana zake ili kujua ukweli hapo

ni kumtafutia huyo dada,sehemu nyingine ya kukaaa
full stop...
mtaona reaction yao....
 
Mwanaume huyo katoa sababu za kipuuzi sana...inawezekana wakawa wanafanya mchezo mchafu.

Yani kanitoka namuona kichefu chefu,na mke nae namwambia nenda ukayamalize anasema mie siendi mpaka aondoke,nikamwambia yule anauso wa mbuzi anaitwa haondoki yuko analia2 ananikeraaaaaa! natamani nimpige makofi namuona zuzu.
 
khaaa vitu vingine vinatia hasira mpaka basi, embu mwambie aripoti polisi, rafiki gani asokuwa na haya hana nduguze/ keshaliwa tayari pole sana wewe na mdogo wako, na yeye yuko wapi muda wote anaacha family yake?
 
hehehehheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ingekua mimi ndo wife huyo shosti namtimua, kwa nini hakumpigia wife kumwambia hana pa kuishi ili wife aongee na mume waamue? na huyo mwanaume hana adabu, amejaa dharau na hakufunzwa kwao. all in all mpe pole huyo nduguyo hana lake apo ajiandaa kisaikolojia ipo siku atakuta shosti rum anamkanda kanda mumewe
 
Yani kanitoka namuona kichefu chefu,na mke nae namwambia nenda ukayamalize anasema mie siendi mpaka aondoke,nikamwambia yule anauso wa mbuzi anaitwa haondoki yuko analia2 ananikeraaaaaa! natamani nimpige makofi namuona zuzu.
kesharogwa maskini apotelee huko mbali, nasikia kuna style hii
 
khaaa vitu vingine vinatia hasira mpaka basi, embu mwambie aripoti polisi, rafiki gani asokuwa na haya hana nduguze/ keshaliwa tayari pole sana wewe na mdogo wako, na yeye yuko wapi muda wote anaacha family yake?

hilo ndo swali pia
kabla ya kulaumu wezi
je ulifunga mlango????????
 
kwa kuwa akili ni nywele na kila mtu ana zake ili kujua ukweli hapo

ni kumtafutia huyo dada,sehemu nyingine ya kukaaa
full stop...
mtaona reaction yao....

Nimemwambia aende akachukue chake pale Mume hana na wala shoga hana,sikuizi sijui umuamini nani huyo ndio alikau shoga yake since high school, na yule dada angekua mungwana angemwambia shogake lakini alikua na nia mbaya ndio mana mpaka sasa ameka kimnya, mie naona pangekua hapatoshi,bora uibiwe hujui yani ikishafikia kiasi hiki ningenawa mikono.
 
hebu tujiulize hili swali kwa nini dunia nzima..
kesi za wanaume kutembea na ma shosti wa wake/gf zao ni nyingi????????

mimi naweza kusema hivi......
unapokuwa na mke na unampenda na kumtunza vizuri....
mtu wa karibu kuona na kuvutiwa na wewe ni shosti wake....
na kuvutiwa na kumpenda mtu kunakuja tu kwenyewe.......
so anajikuta tu kashampenda mume wa shosti wake bila kujua..

sasa ukikuta kidume kiwembe.....case closed......
 
kesharogwa maskini apotelee huko mbali, nasikia kuna style hii

Shosti hakuna kurogwa wala nini anampenda sana huyo mumewe na anajua ndio mana anamfanyia visa,sijui kwanini anampa time yote au sijui anaogopa kuzimia akifika kumuona shostito wake na mumewe?
 

Nakubaliana na wewe 100% huyu mdogo wangu ni wale type ya kumvua mume viatu akirudi kazini,akupe maji kapiga goti,ukila chakuna yuko hapo kwenye kiti,namwambia huyu bwana haistahili yote hayo huyo keshazowea kula kwenye mapipa,sasa ndio kaniamini ah haya tena ndio avumulie akichoka atamua chakufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…