Mume aua mke baada ya kumfumania

Mume aua mke baada ya kumfumania

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Penzi limegeuka na kuwa shubiri baada ya mwanaume mmoja kumgeukia mkewe na kumuua katika kijiji cha Kaplelach, Kaunti ya Kericho nchini Kenya.

Inaripotiwa kuwa, mwanamme huyo aliyekuwa na ghadhabu alimfumania mkewe akishiriki mapenzi na jamaa mwingine 'Live' chumbani mwao usiku wa kuamkia Aprili 6,2019.

Kulingana na ripoti ya The Standard, Julius Rotich alimshambulia mkewe na kumuua wakati akijaribu kutoroka, alipofumaniwa akihondomola tendo la ndoa na jamaa mwingine.

Muda mfupi baada ya kisa hicho, Rotich alimpigia simu Paul Cheruiyot ambaye ni chifu wa eneo la Soin na kumuarifu kuhusu alichokuwa amekitenda.

"Alinipigia simu na kuniarifu kuwa, alirejea nyumbani kwake usiku wa manane na kumpata mkewe Rachael akiwa na jamaa mwengine.

"Baada ya kuzuka vita vikali, jamaa huyo alitoroka. Alimgeukia mkewe na kumuua kwa kutumia upanga,"Cheruiyot alisema.

Kulingana na chifu huyo, mshukiwa alijisalimisha katika kituo cha polisi, huku upanga uliotumika kwa mauaji hayo ukipatikana katika eneo la tukio.

Aliongeza kuwa wawili hao walikuwa wakizozana mara kwa mara.

"Kumekuwa na mzozano wa mara kwa mara kati ya wawili hawa. Huenda madhara ya ulevi imedhoofisha ndoa yao ndipo kukazuka vita baina yao,"Chifu huyo aliongeza.

Mwili wa marehemu uliokuwa na majeraha mabaya ya panga, ulisafirishwa hadi chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya Kericho.

Chanzo - Tuko
 
Kafanya jambo la msingi sana na iwe fundisho?
Walishindwa hata kwenda gest au basi kichakani?
 
Ni uamuzi sahihi kuua Mzinifu alieoa/ kuolewa

Aliekusaliti Hapo anakuwa Mkeo sio huyo Mwanaume

Wewe una Mkataba wa ndoa Na Mkeo sio Mzinifu wa Mkeo , Yule utamhukumu kwa kuzini Lakin Mkeo ana Makosa ya kuzini Na ku kusaliti,

Kosa la kusaliti Katika level ya Nchi Ni sawa na kosa la uhaini
 
alistahili....ila tutofautishe tendo la ndoa na zinaa (uzinifu) neno tendo la ndoa ni "TAKATIFU" nje ya hapo ni zinaa, uasherati au tendo la ngono....ngonoka....
 
Back
Top Bottom