Mume kutembea na "zana"

Msiba mtamu kwa jirani, utautafutia kanga mpya au kitenge cha bei na salon utakwenda kujipamba ili uhudhurie mazishi.

Kwa kweli maswaala ya ndoa na majaribu yaliyomo yanahitaji ujasiri. Hakuna njia moja ya utatuzi.

Pole wewe dada kwa kuzikuta zana kwa mumeo halafu hujajua zimetumikaje? Ni majaribu makubwa sana.

Ushauri:
Kanunue za kike weka hapo chumbani, mumeo akirudi jipambe, chukua zana kama mbili na umwage unatoka kidogo. Au ashuhudie box limekwisha.

Akikuuliza mwambie umejifunza kutoka kwake ya kwamba anakupenda sana, nawe unampenda kulikoni, hivyo nawe umeamua kumlinda kama ambavyo yeye anavyokulinda. Mpe na kiss la nguvu "MMBWWAAA!!!!"
 

Mbu usitake kunivunja mbavu kwa kunichekesha,sasa hapo anaefanya majaribio nani?ni huyo mume au??jamani......mmmhhh makubwa!? hapo ilitakiwa mke awe mpole mpaka kwenye sita kwa sita,alafu atake mchezo mume akileta kigugumizi ndio angemuuliza kwa upole kama alivyosema Mchola lakini kwa mtindo aliotumia hata mie ningeruka kimanga,ila akae na mume wake amweleze kwa upole majuto atakayopata baadae,sababu iko siku atasahau zana,na pia nenda kaangalie afya yako mama.ila hapo mume anatumia usemi wa KAMA UNAMPENDA UTAMLINDA!!.
 
Pole dada kwa mkasa huo,lakini lamsingi ni kujiuliza nini mmeo anakosa kwako mpaka aache chake cha halali na kuanza rukaruka mitaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…