Mume na Mchepuko wamweka Njia Panda...

Mume na Mchepuko wamweka Njia Panda...

Bbade

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Posts
6,725
Reaction score
21,818
Habarini wana jamvi…

Leo ningeomba mawazo yenu kwenye hiki kisa..ni mkasa wa kweli…nitatumia majina yasiyo rasmi.

Aku na Sam ni wapenzi tangu wakiwa shule ya sekondari, walifanikiwa kumaliza shule na kwenda vyuo tofauti kila mtu na fani yake…Aku akasomea Udaktari na Sam akasomea Ufundi.
Miaka ikapita wakamaliza, wakaja kuoana wakaajiriwa.

Kutokana na mikopo ya chuo hawakutaka kunzisha familia mpaka iishe.

Aku akiwa kazini akakutana na daktari mwenzake mzoefu kwenye kazi akawa kama ndio mwalimu wake kwa kipindi kile…bila kujua Aku akajikuta kwenye penzi na huyu daktari….(Joe)

Aku alimpenda Joe sababu alikuwa ana akili za kiutu uzima na mwenye kujua sana mapenzi kulingana na mume wake (Sam).
Bila kusahau kiuchumi Joe alikuwa vizuri.
Siku zikaenda hatimaye Aku akapata mimba.

Alichukua kipimo nyumbani akakitupa kwenye ndoo ya matakataka kikiwa kinasoma kuwa ni mjamzito, bila kujua mumewe alikiona pia.

Kazini Aku aliweza kujifanyia scan ya picha na kujua ukweli kuwa ni mjamzito, bahati mbaya Joe alikuja kujua kwa kuziona zile picha bila Aku kujua.

Aku akawa hajui mimba ya nani?
Mumewe kamuuliza anampango gani nayo? Ukizingatia wao kama wao hawajajiandaa kuwa na familia….

Daktari Joe naye yuko tayari hata kesho kuoana na Aku….

…maji yameshamwagika….
Tunamshauri vipi Aku.
 
Daktari kutojua siku za hatari na salama huo ni upopoma.

Apambane na hali yake
 
Ni uzembe uliopitiliza mwanamke kutojua mimba ni ya nani kati ya wanaume wawili ama alikuwa anakitembeza kuzidi hiyo idadi tena daktari!!! Ningekuwa ndo yeye ningejizaba makofi mawili mazito
Inawezekana asijue, maana akiwa kazini anapata toka kwa Joe, akirudi nyumbani lazima atimize wajibu wake kwa mumewe.
 
Tutajuaje kua Aku hakutaka Sam aone kipimo? Asingekitupa kwenye ndoo ya taka.

Tutajuaje kua Aku atacheat hata baada ya huu msala kupita? Amemsaliti mtu aliyeanza naye tangu chuo huyu loyalty haipo damuni.

Tutajuaje kua Aku ana akili za darasani tu? Eti hajui siku zake.

Tutajuaje kama hii stori ni kweli? Inasound kama uongo and we all know truth is stranger than fiction.
 
Back
Top Bottom