Anyisile Obheli
JF-Expert Member
- Dec 13, 2009
- 3,400
- 320
ukiwa makini utalinda ndoa ya rafiki yako
ukilegeza kamba utaibomoa ndoa ya rafikiyo,
hata hivyo onesha kwamba hupendi toka moyoni ushenzi wake,
usidanganyike na sifa akupazo, wewe si mzuri kuliko mkewe amini hivyo,
umakini wako utakusaidia sana kama ukiamua kuwa hivyo, kwa nini nimesema hivyo!Asante anyisile, hapo kwenye bold ni kweli kabisa hasa tukizingatia uzuri ni perception. Kama wachangiaji wengine walivyesema, huyu jamaa anaonekana ama mkware mzoefu au ana kipaji cha kutumia maneno - buttering...anaweza kukupa sifa hata usizonazo ili kufikia lengo.
Annina
umakini wako utakusaidia sana kama ukiamua kuwa hivyo, kwa nini nimesema hivyo!
kwa uzoefu wangu na ndoa naamini mtu unapofikia kuoa/kuolewa, it means umejiandaa na kujua hakuna atakayetokea mzuri kuliko mkeo/mmeo, hivyo asikubabaishe na maneno ya kuufurahisha moyo ili uwe mmoja wavunjifu wa ndoa za watu, kwanza vipi asifu maungo yako? huyo ni firauni tu asotosheka
Anyisile, umesema sawa, shukran.
Annina
hahaaa haaa!! hujatulia we IzaIla bulaza ana mistari..
Wapendwa nina rafiki ambae pia ni jirani yangu. Urafiki ulianzia kwa mtoto wao wa miaka 4, tukafahamiana na mama wa mtoto na tukawa marafiki na hatimae nikatambulishwa kwa baba wa mtoto ambae pia ni mume wa huyu rafiki yangu. Tulipoonana mara ya kwanza akadai nafanana sana na dada mmoja na haamini kama hatuna undugu na huyo dada - mke wake hamfahamu huyo mdada ninaefananishwa nae nami simfahamu pia.
Toka siku hiyo kila tunapoonana amekuwa hakosi cha kusema juu yangu, mara nina macho ya uhamasishaji, lips sijui za kufanyaje.... umbo la kampeni... nk nk. Amekuwa akiyasema hayo mbele ya mke wake na rafiki zake. Sijamzoea wala sina utani nae, na nimeweka wazi kwamba sifurahii anachokifanya lakini ni kama hanielewi. Leo asubuhi tumekutana akiwa na mke wake wanaelekea kazini, mke wake akaja kunisalimia na kunihug, mume nae akaja akafanya kama mke wake hii ni mara ya kwanza kwa yeye kunihug, akashtuka kama kapigwa shoti na akasema nina ngozi laini hajapata kuona! Nilijisikia vibaya na niliona mke wake pia amekosa amani. Sijui kilichoendelea baada ya kuachana nao. Nimebaki na maswali mengi na sijui ana maana gani kwa anayoyafanya lakini naona anavuka mipaka. Nilikuwa na imani mke wake atachukua hatua na kumkanya, sijui kama amefanya hivyo.
Wapendwa mnalionaje hili?
Annina
...........mhhhhhhhhhhh!!Njia nzuri hapo ni kuwaepuka wote huyo rafiki yako na mume wake usiwe close nao. Bila hivyo mtakuja kukorofishana na huyo rafiki yako kwa ajili ya mume wake. Ninavyosema hivi mimi mwenyewe yalishanikuta kama hayo, hivyo hivyo mume wa rafiki kutwa kunisifia hadi mkewe ambaye ni rafiki yangu wivu ukamwingia na kuhisi namchukulia mumewe kumbe mumewe alikuwa limbukeni tu.Halafu mbaya zaidi anakusifia vitu ambavyo mkewe hana hapo ndio kasheshe kweli kweli.
nimependa tu pale kuwa uan umbo la kampeni
mimi sijaelewa tatizo bado; kama yote anayokuambia tena hadharani, bila kuuma maneno na mbele ya mke wake akimaanisha kuwa ni kweli kwamba:
a. macho ya uhamasishaji
b. Lips sijui za nini
c. Umbo la kampeni
d. Ngozi laini hajawahi kuona
e. n.k n.k
Kama haya yote ni sifa ulizonazo kweli na hadi sasa hajasema neno la kukutaka au hata kukujaribu kukutafuta nje ya muda wa ziada au kuonesha kuwa anataka kukunong'oneza jambo kwanini unamfikiria anakutaka au ana nia nyingine zaidi ya kukupa sifa hizo? Kwanini usichukulie tu at face value na wewe kama unaona kuna vitu vizuri kwake ukamrudishia sifa.
a. Kaka una miguu ya CCM
b. Macho ya chama
c. Umbo la kibalozi
d. Ngozi laini ya kifisadi fisadi
Mpe hizo sifa mbele ya mke wake halafu tuone mtaishia wapi, inawezekana ndio mtakuwa mnaheshimiana zaidi. DON'T take it too serious...
On the other hand.. itakuwaje kama hizo ni preview ya kukupigia mahesabu?
[/COLOR][/B]
Asante NN kwa ushauri, nimejaribu kumuonyesha na kumwambia spendi anachokifanya, na kama nilivyosema awali sina mazoea nae wala utani ni kama anaang'ang'ania kunizoea. Hapo kwa bold inawezekana wadada tunapenda attention lakini kwangu mimi anachokifanya si attention bali ni udhalilshaji!
Annina
Nadhani unamuendekeza, posibly kwa sababu zako binafsi!
- Wewe ni single, married, divorced, widowed?
- Wewe unapomuona unahisi vipi? I mean kuna hisia yoyote uliyonayo juu yake?
- Umeshaongea na mke wake kuhusu kutopendezwa na tabia ya mumewe?
- Kwani njia yao ya kwenda kazini inapitia barazani kwako?