Mume Wangu Ametishia Kuniua, Sababu, Urafiki na Mzungu na Kutembelea U-turn

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
mimi ni mshabiki wa blogu ya u-turn, ila mume wangu kwa muda wa miezi minne sasa amekuwa na kisirani kweli heti, kisa mimi kuitembelea hiyo tovuti ya uturn. sababu zake ni kwamba nina ujeuri. basi kuna rafiki yangu mmoja ambaye ameolewa na mzungu aliniita nyumbani kwake. shemeji yake ambaye pia ni mzungu alikuwepo hapo. tukapata vinywaji kidogo, na kubadirishana namba za simu na huyu shemeji yake. mara kadhaa tumewasiriana kama marafiki tu, mume wangu akatokea kuona text moja niliyotumiwa na huyu mzungu mabayo ilikuwa tu ni knijulia hali, matokeo yake kaja juu na kunipiga sana. Alinifukuza kwa siku 4, pia ananitishia kuniua iwapo sitasitisha mawasiliano na huyu mzungu pamoja na kuacha mara moja kutembelea blogu ya uturn. Hataki hata urafiki wangu na yeyote ambaye ana uhusiano na huyo dada mwenye blog ya u-turn. Anasema heti nikiendelea kutokumsikiliza ataniua na huyu mzungu, wakati mzungu wa watu hana hatia yoyote? Jmani huu si ni ubaguzi wa rangi? kwa nini anifukuze au kuniua, kisa urafiki na mtu wa rangi tofauti, hii kweli ni haki? mm urafiki na mzungu siachi, na uturn siondoki, huu ni unyanyasaji wa kijinsia
 

Pole sana na changamoto hii,
Naona umeandika kwa jazba sana. Hebu tulia kwanza,
Lakini
1. Mume alishakuonya kutembelea uturn
2. hapo kwenye bold red, Je ni kweli hauna jeuri?

Sitaki kumtetea mumeo, ila mkae chini muongee ni kwanini hataki utembelee U-turn?? Mi nakushauri msikilize mumeo, alikupenda wewe, haya mambo ya uturn yanapita tu, wazungu wanakuja na kuondoka,
kuwa makini na ndoa dada, wengine wanazitafuta usiku na mchana hata za kusingiziwa lakini wapi, japo hata kuminyiwa jicho, wewe unataka kuchezea ndoa yako?? Think twice.

Uliahidi kwenye kiapo cha ndoa kumtii, na hiyo ndio sifa kubwa! kuna kitu gani special uturn hadi ung'ang'anie kiasi hicho??
 
Sasa kwa vile umejiunga na JF, tegemea matatizo zaidi, maana utapata addiction ya kufa mtu!...
Lakini wewe mwenyewe umesema kwamba una jeuri, kwanini umfanyie jeuri mumeo?
Marafiki wasikufanye uharibu ndoa yako!
 
sasa wewe mpaka leo haujielewi kama unataka hazbendi , rafiki mzungu au globu ya U turn?, tunaomba bethi setifiketi yako pliz
 
Pia kumbuka haya maneno yako

watanzania wanaharibiwa na mange kimambi, ku posti picha za wazungu wazee na vitoto vya kike

https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/59049-kuolewa-na-mzungu-tanzania-ni-ticket-ya-u-celebrity-au-njaa-4.html#post1623520

Huyu shemji yako, lazima atakuwa ni mfuasi wa blogu ya U-turn. Kule ndo chuo kikuu cha mababu wazungu cha muzumbe. Kili Janga wa Babu Ralph na Kisa Maliq, naye kamuacha mumewe na mwanaye kusaka mzungu kwa binti mangeleza wa uturn
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/118185-shemeji-yangu-kamkimbia-mumewe-na-mwanaye-kisa-mzungu-na-range-rover.html#post1741100

na hapa


The new generation of Change in TZ. Asante sana uturn

hiyo ni moja wapo ya michango yako..Jiulize nafsi yako kama ni kweli hauna unalotafuta kwa wazungu... judge yourself
 
Mpendwa asante!Hawa ndo wale wanaotunga uongo kutengeneza jina!Yani yeye anaipenda sana mpaka anapigwa na yeye anaiponda kwamba inaharibu?Kama inaharibu anang'ang'ania ya kazi gani kama na yeye bado hajaharibika?Michango yako we mdada inaonyesha kwanini mumeo anakupiga!
 
we ni limbukeni na huna mda mrefu utaachwa na bwana ako
 
Reactions: CPU
Wote wawili mna wivu. Yeye ana wivu wa mapenzi juu yako kama mke wake. Wewe una wivu wa mali, maisha ya starehe, anasa na ubishoo waliyo nayo wanawake wa Wazungu. That said, between the two of you, its the envious, greedy bitch in you thats out of line in this scenario.
 
Reactions: CPU
dah! mkuu una shahada ya intelijensia ya kirusi nini? kumbe huyu mzembe anatupotezea umeme wetu tu?

tatizo mkuu wanasahau kuwa JF ni teknolojia..na pia watu tunafuatilia consistency ya uchangiaji mada...

huyu ana hasira tu. namshauri akae chini ajifikirie..
 
sasa wewe mpaka leo haujielewi kama unataka hazbendi , rafiki mzungu au globu ya U turn?, tunaomba bethi setifiketi yako pliz
umeona kibri yake huyu asiyejua anachotaka.
unakuwa na kibri halafu hujui unachotaka!!!
 
dah! mkuu una shahada ya intelijensia ya kirusi nini? kumbe huyu mzembe anatupotezea umeme wetu tu?

Ohhhh!!! yaani nilikuwa nawaza nimwambie nini...basi naona mpendwa amemaliza!!

Dada... hivi huyo rafiki wa kizungu ni wa maana sana kuliko mume wako au hiy website ya u-turn???!!! Think twice kama kweli unampenda mume wako!
 
Pole sana na changamoto hii, 1. Mume alishakuonya kutembelea uturn
Ungemsikiliza tuu mumeo dada, inawezekana anapitia hiyo blog au anarafiki yake ambaye yamemkuta na kuharibu ndoa yake n.k. Kwahiyo anaweza kuwa na sababu nzuri kabisa ya kukukataza.
2. Sitaki kumtetea mumeo, ila mkae chini muongee ni kwanini hataki utembelee U-turn?? Mi nakushauri msikilize mumeo, alikupenda wewe, haya mambo ya uturn yanapita tu, wazungu wanakuja na kuondoka,
Huu ni ushauri wa busara sana, utafakari. Mamo ya U-turn ni mambo ya nje, nyiyi ni mwili kitu kimmoja kwahiyo sivizuri kumkwaza mumeo.
 
Ohhhh!!! yaani nilikuwa nawaza nimwambie nini...basi naona mpendwa amemaliza!!

Dada... hivi huyo rafiki wa kizungu ni wa maana sana kuliko mume wako au hiy website ya u-turn???!!! Think twice kama kweli unampenda mume wako!
ushehe yahaya wangu unaniambia lazima huyu atakuwa kala mkorogo tu afanane na wazungu. ningekuwa mod ningempiga ban yeye na shangazi yake. nimekasirika kweli, yaani kama hii laptop si ya kuazima ningevunjilia mbali kwa hasira. (naomba unitulize mzuka keren)
 
Mtoa mada inaelekea ulifurahi sana kuona Max na mwanae walivyotukanwa katika ile blog???? acha USENGE hatutaki kuona hbr za hiyo blog wala upuuuzi wowote unaohusu huko, kifupi koma uwe na huruma kuona boss na mwanae walivyodhalilishwa!!!!


Upuuzi wako na mumeo nahiyo blog HAVITUHUSU!!!!
 

Hebu achana naye asiyejua maana ya hazibendi....wengine wanawatafuta yeye analeta mchezo..!!!!, Twende tukaendelee kusheherekea siku yake ya Klorokwin!
 
kama hajaelewa hii post yako lazima atakuwa kafeli darasa la saba huyu. dah! kama hajabadili ID nitamuona jasiri kweli aisee.
 
kama hajaelewa hii post yako lazima atakuwa kafeli darasa la saba huyu. dah! kama hajabadili ID nitamuona jasiri kweli aisee.

Kuna mijitu inakera sana wanaanzisha mada wakijua fika lengo lao, inakera sana :smash::smash::smash::smash:
 

Kwa maneno haya, kama mtoa mdada mshipa wa aibu bado unafanya kazi, akimbie aishie kabisa. Lakini kwa sababu ya ujeuri unaweza ukamkuta bado ana nguvu za kubisha na kuendelea na upumba wake!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…