Mume wangu ananipa Laki 5 k
Kabla ya kuingia kwenye ndoa, kulikuwa na mwanaume niliyekuwa naye—ni mume wa mtu. Yeye ndiye aliyekuwa analipia ada yangu ya chuo, alikuwa ananipa pesa pamoja na kuhudumia wadogo zangu. Yaani, hata ada za wadogo zangu alikuwa akilipa. Nyumbani kila mtu alifahamu kuhusu msaada wake, kasoro Baba.
Kipindi hicho nilikuwa pia na huyu mume wangu, ambaye wakati huo alikuwa mchumba wangu. Alikuwa ananihudumia kwa mambo madogo madogo, lakini sikuwa nikiomba pesa nyingi kutoka kwake kwa sababu nilikuwa na mbaba wangu. Baada ya kumaliza chuo, sikuhangaika kutafuta kazi. Nilijaribu kufungua biashara, lakini haikufanikiwa, hivyo nikaamua kuolewa.
Kila kitu kilikuwa vizuri, lakini kipindi nikiwa kwenye ndoa niliendelea kuwa na yule mbaba wangu. Alikuwa bado ananihudumia. Shida ilianza baada ya mume wangu kuhamishwa kikazi, tuko mkoani sasa, na siwezi kuonana na yule baba kwa sababu pia nina ujauzito.
Changamoto ni kwamba kipato cha mume wangu ni kidogo sana, mshahara wake ni kama milioni 3 hivi. Anaweza kunihudumia, lakini hawezi kuhudumia ndugu zangu. Siwezi kumuomba pesa ya kumhudumia Mama yangu au kulipia ada za wadogo zangu. Kwa mwezi, mume wangu hunipa laki 5 kwa ajili ya matumizi yangu na kusaidia kwetu, lakini haitoshi hata kwa Mama yangu tu.
Niliwazoesha msaada wa pesa kiasi kwamba kila kitu wananiomba mimi. Nikiwaambia kuwa mambo yamebadilika, hasa Mama, hataki kunielewa. Ananiambia kuwa nilikurupuka kuolewa, na kama mume wangu hawezi kusaidia familia yangu basi niachane naye.
Mama yangu alimtafuta yule baba kuongea naye kuhusu kurudiana na mimi. Baba alisema kama bado nampenda, basi nirudi Dar es Salaam, na yeye atalea mimba yangu na kuendelea kunihudumia. Hata hivyo, alisema hawezi kunipa pesa wakati nikiwa mkoani!
Sina shida yoyote kwenye ndoa yangu. Mume wangu ananijali kwa kila kitu. Hivi sasa tunajenga, na sijachangia chochote, lakini kwa wema wake ameandika majina yetu wote wawili kwenye mali hiyo. Chakula na kila kitu kinapatikana, lakini sina amani kabisa.
Mama yangu kama ameninunia—wiki ya pili sasa hapokei simu zangu na anatuma tu meseji akisema, "Umekamua kuwa mbinafsi kujichagua wewe huku ndugu zako wakiteseka. Ikaa huko huko, lakini jua kuwa wewe si mtoto wangu!" Naomba ushauri, Kaka. Nafanyaje? Naona hii ndoa itanishinda, labda nilikimbilia kuolewa!