Mume wangu ananipenda?

Ndo madhara ya wanawake kulazimisha ndoa haya
 
Nakubaliana na wewe Mtoto wa town

Mwanzoni mwa ndoa ni ngumu kumjua mwanaume mwenye uwezo wa kuonyesha ma lovedave hata baada ya miaka 8 ya ndoa. Hata the most boring husbands wanajua kusema I love you miaka ya mwanzo mwanzo.

Ila usione kama una mkosi kwani kuna wenye waume ambao hawapitishi siku bila kupiga simu za I love you kwa wake zao na bado wana misururu ya nyumba ndogo. Mara nyingi hao wanaume ambao ni less romantic ni waaminifu. Nina shemeji yangu ni design hiyo ni workaholic lakini hajawahi kupata kashfa ya cheating na sie mashemeji zake tulikuwa masikio juu especially kabla hatujaolewa na hatujawahi sikia kashfa yoyote kuhusu huyu mume wa dada yetu. Hence waweza kuwa umekosa kimoja; mume mwenye ku show feelings openly, lakini una kitu ambacho hujuhi kuwa wengine hawana; faithful husband.

Kama mumeo ni busy type na ndio inamfanya asiwe na muda wa malovedave wewe kuwa busy zaidi yake hapo mta cope. Ukikaa idle unamkaribisha shetani.

 
Dooh, ndoa zingine na sawa na kuishi na adui yako under the same roof, mwenzako anaumwa wewe unashika njia. Dadangu hapo hakuna mapenzi kaeni muyazungumze labda kuna mapungufu upande wako ili muweze kuyatatua lakini hali hii in longrun is not healthy for the family.

Mkiwa mnaishi hivi si bora kukosa kabisa ukajua uko single mother, kuliko unamwezio lakini he doesn't move a single muscle!
 
Dada yangu hapo ni hivi,
For a man to be that cold, kuna upande wa pili wa hii story tunaumiss hapa.
Inategemea jinsi mlivyokubaliana kuiendesha ndoa yenu,
a) Kwanza ni kwa nini kila mtu afanye matumizi yake wakati vipato vyote ni vya familia?
b) Pili nimesense communication ni ndogo sana hapa (Kwa sababu ikiwa kubwa lazima vitu vya msingi kuzungumzwa vitaisha na mtaanza kutaniana na hayo maneno unayoyataka yatatolewa! kama hamfiki huko ni ngumu sana kuyapata).
c) Binadamu yeyote akifanyiwa wema na ukamuingia moyoni lazima tu atajikuta anamtamkia maneno matamu mtenda inaonesha mumeo kavikosa hivyo.
d) Just remember kwamba tunasema 'I love you', 'I need you' lakini ujue haya maneno ni kama vile mshahara..usipoufanyia kazi huupati...
e) Tumia nguvu ya kike hasa...Ile nguvu iliyomfanya Adamu akala tunda ilhali kakatazwa...Ile nguvu iliyomfanya samsoni akasema kila kitu ilhali akijua inaweza pelekea kifo chake.
Hivi, Honestly-Unafikiri hao wanawake waliwafuata tu na kuwaambia fanya hivi!..wakafanya? think bibie.
 


Wewe huwa unamfanyia yapi?
Unamtamkia hayo unayopenda ayatamke?
Jaribu kuyaanzisha (kuyafufua) yale unayopenda yawepo..
Aweza kuwa anakupenda sana, ila mkawa mnaheshimiana kupitiliza...
 

Pole sana. Jaribu na wewe kwa upande wako kumjali na kumuonyesha mapenzi. Timiza wajibu wako kama mama mwenye nyumba then muwapo faragha, jaribu kumtamkia jinsi unavyompenda na kumjali na pia mnunulie zawadi uone reactions zake (kama atapokea kwa furaha, kama na yeye atakuletea zawadi nk). Pia mjaribu siku moja kutoka naye out umsikie. Inawezekana the way wewe unavyoona mapenzi yamepoa kwenu basi na yeye pia anaona vivyo hivyo!
Jaribu hilo then tuletee feedback tujue kama amebadilika au Laa ili tukushauri zaidi ...

Pole sana mpendwa.
 

Japo ni ukweli ambao watu wengi huwa hawauamini...lakini unabaki kuwa ukweli...MAPENZI HUISHA! Inaweza ikawa kwa sababu mbali mbali ambazo si rahisi kuzilist...lakini huisha, na yanapoisha kuna wengine waweza kuwa wavumilivu basi mkaendelea bila kuona tofauti kubwa...na wengine hawawezi vumilia basi ndio inakuwa kama wewe na mumeo, yaani tofauti ni dhahiri!

Japo kuna wanaosema mapenzi hayo yaliyoisha yanaweza yakarudi...binafsi siamini hilo, na kwa wenzetu ambao utamaduni wao hauwabani sana kwenye kutalikiana...huwa wanafanya hivyo. Moving on is the best alternative kwa situation yako kuliko kupoteza muda na maumivu kwa ndoa ambayo obviously is not working anymore!
 

mama ndoa ni uvumilivu mimi sijaona cha ajabu kama wewe unakipatokizuri ukatumia pesa yako sio baya,na mambo mengi ya ndoa mtayamaliza nyie wenyewe usimshirikishe mtu tena hasa wazazi bora wadhamini mara 100%
 
Du! nahisi huyo mwanaume ana tabia kama yangu, simpendi girlfriend wangu sijui kwanini, huku mpaka tumepata nae mtoto, sababu sina wala hajanikosea.
 

Piga keleleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!! mpende mumeo dada. Jipendekeze. Upande wako fanya yale uliyoahidi kufanya.

Mungu ni mwaminifu atamrejesha tu.
 
Haya bana,
heri mimi hapa sitasema kitu chochote.
 
Mhhhh............pole my dia. Mi nitakuombea Mungu afanye njia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…