Mume wangu hapendi kula nyumbani

miss chuga

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2019
Posts
303
Reaction score
660
Habari zenu wapendwa?

Naombeni msaada Mume wangu amekuwa pasua kichwa hapendi kula nyumbani, najua kupika nampikia vyakula vizuri lakini akija anakula tu kidogo anaacha wakati mwingine hali kabisa ukimuliza hana sababu.

Mwanzo nilijua labda napika vibaya lakini siyo maana watu wengine wakila hata wageni wanakifurahia sana chakula mpaka wananisifia najua kupika Ila mme wangu ndo tatizo anaweza akala hata vijiko 5 akasema ameshiba.

Hii hali kwakweli inaniumiza sana akili na uzuri ana mwili nahisi labda atakuwa anakula uko nje akija anakuwa labda ameshiba maana kwa jinsi anavyokula hapa ndani alitakiwa awe hana hata afya yani kwa kifupi ni kama tu hali Ila anagusagusa, kuna wakati hadi nawaza sijui kalogwa.
 
Hao wageni wanakula free meal lazima wakusifie tu hata kama kibaya. Chunguza ujue kama anakula nje ama la. Kwani huwa hamtoki OUT uone huko anakula vipi?

Kwenye sherehe mkienda ulaji wake upoje? Je wakati wa uchumba alikuwa anafurahia mapishi yako? Mbona kama vile humjui kabisa mumeo?
 
To Cut the story short "amekuchoka anapikiwa na kuogeshwa na kukojoa njee hivyo Kaa chonjo asije akabaki huko huko 👻 ongeza utundu au kubali kuibiwa"
 
Mumeo kama ni mnywaji wa pombe mpikie vyakula vya kilevi.

Cheza na vitu vya kukaanga.. kama ndizi za kukaanga;, viazi na nyama za kukaanga.

Pia mpikie michemsho chemsho kama ndizi za kuchemsha na masupu supu ya nyama nyama za kuchemsha .

Kutegemea mtu alietoka kunywa bia ale wali maharage kisa umeunga na nazi ni upumbavu.

Hata mpishi atoke mbinguni kuna vyakula mtu alietoka kunywa pombe hawezi kula
 
Itakuwa pombe... malalamiko kama haya alikuwa anayatoa mama yangu...

Enzi hizo alikuwa anampikia dingi minyama mizuri, halafu mzee anakuja huko kashapiga pombe zake, anagusagusa.. mkiamka asubuhi unakuta chakula chote kimechacha... amakula vijiko nne kaacha hapo
 
Alikuwa anakula vizuri tu hii tabia imeanza tu sahivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…