Mume wangu na x-gf wake

Mom

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
708
Reaction score
31
Jamani najisikia wivu sana huyu x anavyozoeana na mume wangu, ameolewa ana mtoto, akihitaji ushauri lazima amconsult mr kwanza, hata kuapply kazi mr amsaidie kuandika barua. Ni wivu tu unanisumbua jamani
 
Mumeo anakosea kabisa. Kwa nini unaendekeza udhalilishwaji wa namna hiyo? Hivi wewe huna wako wa zamani? Kama huna tafuta na wewe rafiki mpya atakayekuwa anakushauri, kukusikiliza ukitaka sikio la kukusikiliza, na bega la kuinamia endapo utalihitaji. Au huwezi kufanya hivyo?

Kwa mengine zaidi niPM
 
Mom umejuaje yote hayo? Mumeo huwa anakuambia? Huy X unamfahamu?

Kama ni hivyo, mshukuru Mungu, hakuna ubaya wowote unaotokea kati yao....Punguza wivu!

Sisi wazee wa infidelity, wake zetu hawapati nafasi ya kuwajua ma-x wetu! Ni mwiko, hasa ukizingatia kuwa imani yetu kuu ni kuwa mahawara huwa hawaachani, kuna kitu kinaitwa baby come back ambacho ni msingi imara wa kanuni za chama chetu....!

Rest assured, mumeo hafanyi lolote kwa huyo X wake. Haya Gonga senksi kama ishara ya kunielewa!
 
Jamani najisikia wivu sana huyu x anavyozoeana na mume wangu, ameolewa ana mtoto, akihitaji ushauri lazima amconsult mr kwanza, hata kuapply kazi mr amsaidie kuandika barua. Ni wivu tu unanisumbua jamani

Duuh, pole sana.....lakini kuwa makini kidogo waungwana wanaweza kukumbushia enzi.
 
Kabla mambo hayajaharibika chukua hatua madhubuti na useme nae, naona huyu mumeo anakosea sana tena sana hapo, Je wewe X wako angekuwa anakuja kwako na unamsaidia kama anavyofanya wewe ingekuwaje? Angejisikiaje? Hebu sea naye nao X wake huyo mumeo yuko fasta sana angalia tu usije letewa mtoto mwingine, maana wasije wakasaidiana hadi kwenye biolojia zao
 
Jamani najisikia wivu sana huyu x anavyozoeana na mume wangu, ameolewa ana mtoto, akihitaji ushauri lazima amconsult mr kwanza, hata kuapply kazi mr amsaidie kuandika barua. Ni wivu tu unanisumbua jamani

Yaani umekaa kimya tu unailea hiyo hali ya hatari kiasi hicho? Haya weeee,...ukiendelea kucheka na nyani utavuna mabua.

Usipochukua mathubuti tena haraka sana (bila kuangalia nyuma au kumchekea mtu), usije kusema hatukukustua!

Retired Maj Gen DC (1947)
 
NN, wataka nifanye revenge? no pse
 
ah bibi weew acha habari zako dahh ..iweje unaacha hali iyo?
kemea tena ukemee haraka sana wenzako wanadinyana hao wala hawajaachana ni apo tu unakuta msg lakin wenzako wanaonana uko nje km kawa
bado wanapendana thou uyu kaoa na uyu kaolewa...si consultation ya mambo hayo tu bali ni HELP N CONSULTATION YA KILA KITU...
ongea nae bibi tena charuka utake maelezo ya kutosha lakin kwa kutumia akili ya darasa la pil b tu apo ao bado ni wapenz tena wapenz haswaa
dah wewe ebu amka umkemee shetan kungali asubuhi asije shetan akajenga makao apo mbwga ukabaki A WIFE BY TITLE BT WIFE BY LOVE NI UYO X WAKE
 
kile batani cha thanks sikioni,
huyu ni x wake b4 mi cjatawala hapa, my mr si mpenzi wa kukaa chini aanze kudraft application so aliomba nimsaidie maana mi ndie hua nafanya application zake nyingi nilipouliza yanani akajibu nikamwambia mwambie aniombe mwenye.
lakini huyu dada ataka nn wakati ana kwake?
 
NN, wataka nifanye revenge? no pse

Hapo ndo utakapojimaliza. Ukikamatwa unapigwa chini na jamaa anaendelea kutesa na X wake. Hebu jaribu kumsoma vizuri Rose ingawa mhhh, sisi wastaafu bado tunapata shida ku-assimilate hizo points zake tamu!
 
Jamani najisikia wivu sana huyu x anavyozoeana na mume wangu, ameolewa ana mtoto, akihitaji ushauri lazima amconsult mr kwanza, hata kuapply kazi mr amsaidie kuandika barua. Ni wivu tu unanisumbua jamani

Mimi namjua jamaa fulani baada ya kutoka kusoma masters Ulaya aliamua kuacha kazi ya serikali aliyokuwa anafanya akatafuta kazi kwenye NGO. Alipoipata, alikuta bosi wake ni jamaa aliyekuwa boyfriend wa mkewe, tena anamfahamu vizuri. Jamaa alikuwa very uncomfortable na situation ile, lakini bosi alikuwa anamchukulia kawaida na tena anampa assignment nyingi zenye pesa ya maana. Siku moja ikatokea vacancy pale kwenye NGO, bosi akamshauri jamaa amwambie mkewe aombe ile kazi, tena ilikuwa na mshiko mzuri, na akamhakikishia kuwa angempa hiyo kazi. Jamaa haku-comment, lakini alipofika nyumbani akakuta mkewe tayari ana taarifa hizo na amesha-draft barua ya kuiomba hiyo kazi. Huo mtiti uliofuatia ilikuwa balaa! Wivu mbaya jamani!
 
Ukipata jibu la hilo swali utakuwa umemaliza mchezo. Kwake kwake lakini kwako kwenu....mhhhhh. Hebu kuwa mbayu wayu haraka sana.
 
Unanikosha sana jinsi unavypanga mipoint yako (na kuchomekea vistori vitamu vitamu) ila inabidi nitafute microscope kupitia maelezo yoote bila kuacha hata herifu moja.

Kwenye red...hiyo ndiyo nini?

Retired Maj Gen DC (1947)
 
Hayo ndiyo watu wanayoyakwepa. Ni bora ma-X wawasiliane lakini wenzi wao wasijue. Ikifikia hapo inakuwa mtu unafanya kazi ya kutunza mali za mwenzio.

Retired Maj Gen DC (1947)
 
Unikosha sana jinsi unavypanga mipoint yako (na kuchomekea vistori vitamu vitamu) ila inabidi nitafute microscope kupitia maelezo yoote bila kuacha hata herifu moja.

Kwenye red...hiyo ndiyo nini?

Retired Maj Gen DC (1947)
mbwiga ni neno la kiswahili hasa pwani ya afrika mashariki katika tz hasa utumika na wazaramo,wamatumbi,wakwere na wengneo katika upande wa pwani
likimaanisha bibi lakini pia linamanisha
mbwiga=shoga,rafiki,
 
Jamani najisikia wivu sana huyu x anavyozoeana na mume wangu, ameolewa ana mtoto, akihitaji ushauri lazima amconsult mr kwanza, hata kuapply kazi mr amsaidie kuandika barua. Ni wivu tu unanisumbua jamani

AnakudharaU..mwambie mumeo hupendi hiyo tabia, ukiendelea kuangalia tu utazidi kudharauliwa..pole
 
Unanikosha sana jinsi unavypanga mipoint yako (na kuchomekea vistori vitamu vitamu) ila inabidi nitafute microscope kupitia maelezo yoote bila kuacha hata herifu moja.

Kwenye red...hiyo ndiyo nini?

Retired Maj Gen DC (1947)

Lugha ya rose ngumu! najaribu kulewa labda nitaelewa
 
mbwiga ni neno la kiswahili hasa pwani ya afrika mashariki katika tz hasa utumika na wazaramo,wamatumbi,wakwere na wengneo katika upande wa pwani
likimaanisha bibi lakini pia linamanisha
mbwiga=shoga,rafiki,

Hapa sasa tunaanza kwenda pamoja. Mi point yako inatisha sana ila sema tu basi....sisi tulipitwa na dot com tunasota. Hata hivyo naona unakaribu karibia.

Retired Maj Gen DC (1947)
 
Lugha ya rose ngumu! najaribu kulewa labda nitaelewa
mmh sasa leo ndiyo nimejitahidi kukisimamisha kiswahili sanifu sasa mom km ngumu kunielewa tena apo ahh sjuii nfanyaje sasa?
ni ivi
1.mumeo na x wake ni wapenzi bado
2.kitendo icho kinaonyesha dharau uyo mumeo anakudharau
3.ongea na mumeo that haupend tabia iyo
umenielewa mama?apo nimetumia lugha ya bikira maria sasa km ngumu tena mmh basi mi sfai!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…