Cattigo
Senior Member
- Nov 12, 2016
- 193
- 393
Baada ya kumshukuru Mungu kwa ulinzi wa Usiku uliopita, na kumwomba akuongoze Leo, HEBU tutafakari pamoja neno hili fupi;
Luka 16: 20-22
20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
TAFAKARI:
"...maskini akafa akachukuliwa kifuani kwa Ibrahimu,,,tajiri akazikwa".
Tunaona ama kuhudhuria misiba mbalimbali na kisha mazishi hufanyika. Mfano huu wa maskini na tajiri unatuthibitishia kwamba maisha baada ya kifo yapo na ni kweli, lakini pia unathibitisha kwamba kuzimu, jehanamu na adhabu ya milele ipo na ni kweli.
Wakati wa mazishi, kwa macho huwa tunaona marehemu wetu wamezikwa, lakini mambo mawili hutokea katika ulimwengu wa Roho:
1. Wenye haki huenda moja kwa moja mbinguni, na
2. Wasio haki ni kweli hushukia kuzimu katika adhabu iliyo sawa na hatia zao (Mstari wa 23).
Ni matendo na mienendo yetu inayoamua hatima yetu hapo badae. Ukitenda vema utapata haki yako. Na kinyume chake utapata pia unachostahili.
Unapoelekea kwenye majukumu yako ya Leo, tafadhali kumbuka kutenda na kuenenda vema kwa ajili ya Kristo na kwa ajili ya uzima wako wa milele. Amina!
Nakutakia BARAKA.