Mungu anaweza kutumia mabaya kuleta Mema katika maisha ya Watu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
557
Reaction score
858
Zab 105:17-21 SUV
[17] Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani. [18] Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma. [19] Hata wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya BWANA ilimjaribu. [20] Mfalme alituma watu akamfungua, Mkuu wa watu akamwachia. [21] Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake, Na mwenye amri juu ya mali zake zote.

Safari ya Yusufu kuifikia ndoto yake haikuwa nyepesi, alipita katika maeneo tofautitofauti magumu, maeneo ambayo kwa hali ya kawaida hayakuwa madogo, mateso yake yalitosha kabisa kumfanya achukie hata Mungu na kufanya mambo yanayomkosea.

Kutoka kunusurika kuuwawa, kisha kuuzwa utumwani, baadaye akasingiziwa kubaka, kisha kufungwa gerezani, haikuwa safari yenye raha, ilikuwa imejaa masumbuko mengi ya kuumiza moyo na mwili wake.

Mapito yote aliyokabiliana nayo Yusufu, Mungu alikuwa pamoja naye, alimlinda katika hayohayo mapito magumu aliyopitia, ambapo kwa akili zetu tungesema atuepushe nayo, kupitia mabaya hayo ilikuwa ni njia ya Yusufu kufikia ndoto yake ya kuwa mtu mkuu katika taifa.

Mungu alimpa hekima ya kumtumikia Farao na taifa la Misri, akawa amewekwa kwenye nafasi ya juu sana, nafasi iliyompa uwezo wa kuwasaidia ndugu zake wale wale waliotengeneza njama ya kutaka kumuua na baadaye kumuuza utumwani.

Tunajifunza mambo mengi sana ya msingi katika kisa hichi cha kusikitisha, inaonyesha wazi Mungu anaweza kutumia mateso yetu, au hali ngumu tunazopitia, au uchungu mwingi tunaoupata katika safari yetu ya wokovu, ili kutuweka imara tuweze kufiti katika nafasi anazotaka tukae.

Tunajifunza pia kuhusu uvumilivu na imani, Yusufu alikuwa mvumilivu na mtu wa imani katika mapito hayo yote magumu, jambo lililoweza kumsaidia kufikia hatima yake njema. Wakati mwingine tunapopita katika hali hizi huwa tunapoteza imani, na uvumilivu huwa unakosekana kabisa na kufanya maamuzi ya hovyo kabisa.

Ikiwa Mungu anaweza kubadilisha mabaya kuwa mema kwa wale wanaompenda na kumtegemea yeye nyakati zote za maisha yao, hata kwako anaweza kufanya hivyo. Huna haja kuona Mungu hakuoni au hakupendi au hasikii maombi yako.

Endelea kumcha Mungu kwa uaminifu, endelea kumtegemea siku zote, bila kujalisha mazingira hayakutii moyo katika kumtegemea kwako Mungu, ipo siku uchungu wako, maumivu yako, mateso yako, yatageuzwa mambo makubwa na mazuri kwako.

Ukiwa kwa Mungu wa kweli huna haja ya kujuta, upepo unaweza kubadilika wakati wowote, machozi yako ya huzuni yanaweza kugeuka wakati wowote kuwa machozi ya furaha, amini haya, Mungu kwako ni zaidi ya vile unaweza kuona wewe na kusema kwako.

Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukaribisha kwenye kundi hili zuri la wasap la kusoma biblia kila siku na kutafakari, ni moja ya kundi linaloweza kukusaidia kumjua Mungu wako vizuri kupitia neno lake. Ukipenda hili wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye kundi hili zuri.

Mwisho, nikukaribishe kwenye channel ya wasap kupata maarifa mbalimbali bonyeza link hii kujiunga=>>Samson Ernest | WhatsApp Channel

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana

Noma sana!
 
Back
Top Bottom