BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Bwanku M Bwanku
Licha ya Tanzania kubarikiwa na kila aina ya madini lakini kwa muda mrefu sana madini hayo wala yalikuwa hayawanufaishi Watanzania kwasababu ya kukithiri kwa vitendo vya ufisadi kwenye madini, utoroshaji wa madini, mikataba mibovu na sheria za hovyo zilizoisababishia nchi yetu kupoteza Mabillion kwa Mabillion ya mapato ya madini.
Mfano tu mdogo, huko nyuma madini ya Tanzanite ambayo hupatikana Tanzania tu dunia nzima lakini kwenye orodha ya nchi zilizokuwa zinazouza sana madini hayo nchi yetu wala haikuwemo licha ya sisi tu duniani kumiliki madini hayo. Hapo ungeikuta India, Kenya na Thailand ambao wala hawana Tanzanite wala mgodi mmoja wa Tanzanite. Kwakweli nchi ilikuwa shamba la bibi na ungeweza kuionea huruma nchi hii namna ilivyokuwa inaibiwa.
Kuingia madaraka kwa Serikali ya awamu ya 5 chini ya Dkt John Pombe Magufuli mwaka 2015 ghafla kukabadirisha upepo wa mambo. Rais Magufuli akafanya mabadiriko ya sheria ikiwemo kutunga sheria mpya ya The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act 2017 ambayo ndio ikabana wizi na ulinzi wa madini yetu, kujenga ukuta mkubwa wa Km zaidi ya 25 kuzunguka mgodi wa madini ya Tanzanite kule Mererani na kudhibiti utoroshaji wa madini.
Leo ndani ya miaka mitano tu ya Rais Magufuli baada ya mageuzi hayo makubwa kwenye madini ikiwemo kubana mafisadi waliokuwa wanagawana hela za madini, kudhibiti utoroshaji wa madini na ulinzi wa madini kila mahali, Sekta ya madini imedouble mapato yake kutoka Bil 200 tu mpaka Bil 470. Yani maana yake zaidi ya Bil 270 ambayo ni nusu ya mapato yalikuwa yanaishia kwenye midomo ya mafisadi. Hivi Mtanzania gani ambaye hajaona haya? #Mitano tena.