Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,788
- 2,690
Habarini wanajamvi!
Kumekuwa na Mada nyingi ambazo zimekuwa zikionyesha na wakati mwingine kuthibitisha ya kuwa Mungu alitenda makosa. Aidha wengine wameenda mbali kwa kuyaorodhesha kwa kadri walivyoona.
Pengine hii aina ya bin adam inaweza kuwa na mantiki katika kuelezea hoja zao lakini kuna mambo huwa hawayaelewi ndio sababu ya kuongea mambo wasio yajua.
Mungu hakufanya Makosa ya aina yoyote Yale, wale hatoweza kufanya makosa kwa namna yoyote ile. Japokuwa ukisoma baadhi ya vitabu vinavyoelezea habari zake pengine ufahamu wa kibinadamu huweza kugundua upungufu mkubwa katika utendaji wake. Pamoja na hayo lakini bado Mungu hakufanya Makosa yoyote.
Wengi hufikiri uwepo wa Shetani hutokana na udhaifu wa Mungu jambo ambalo si kweli hata kidogo.
Shetani yupo kutokana na uwepo wa kanuni huru ya Uungu wenye Upendo. Kanuni hii ndio hata mwanadamu amepewa kuwa na Utashi huru wa kuamua Yale ayatakayo ambayo Mungu alimpangia.
Kila kiumbe kinaukomo, ndio ukomo wa kufanya lolote lile, Ukomo wa Kufikiri, kuona, kuhisi,na hata kuonja n.k.
Mungu ndie aliyeweka ukomo kwa kila kiumbe, huyu atafika hapa wakati yule atafika kule kadhali Mimi nitaishia sehemu Fulani.
Ukomo ndio humfikirisha mwenye hekima naam miisho ya mtu mwenyewe.
Kosa kubwa alolifanya Shetani ni kutokuutambua ukomo wake. Pengine hakusadiki yupo katika mpango asioupanga ndio maana akachagua upande aliodhani alichagua asijue aliyemuwekea.
Watu wengi hudhani kuwa Mungu anakosea kwa uchache wa kufikiri. Pia hudhani kwa Mungu kuna kanuni ya uwili pekee yake Kumbe hujidanganya wenyewe. Viumbe pekee ndio wenye kanuni ya uwili yaan wema na Ubaya, Ukubwa na udogo, juu na chini nakadhalika.
Sasa mtu akiichagua njia mbaya na kupata matokeo yafananayo na ubaya japo wakati mwingine hufanana na uzuri basi huja na kusema Mungu kakosea.
Mungu aliwawekea njia mbili yaani ya wema na ubaya, japo wapo viumbe waliopewa njia zaidi ya hapo au pungufu ya mbili.
Kusema Mungu alikosea ni sawa kwani akili yako ndio imefikia ukomo.
Makosa mengi anayosakaziwa Mungu huhusishwa moja kwa moja na matatizo makubwa yaliyoshindikana yaikabiliayo dunia na viumbe kwa ujumla. Lakini makosa hayo hayahusishwi na mazuri kwani wanadamu hudhani mazuri siku zote si makosa jambo ambalo si kweli.
Pengine nikazua mjadala lakini ukweli ni kuwa Mungu hakuwahi kukosea na hatakuja kukosea. Kinachofanyika ni uzushi uliokosa mashiko utolewayo na wenye akili ndogo ambao hutaka na kuilezea akili kubwa.
Nao hupenda kuelezea mambo wasioyajua kwa kujiona wenye hekima kumbe wapo katika njia panda ya utambuzi wao.
Je akili ndogo itaielezea akili kubwa?
Asomaye na Afahamu.
~Michaelray22