Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 557
- 858
Zab 103:10 SUV
[10] Hakututenda sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
Kupitia mstari huu tunaona kitu kikubwa sana kwa Mungu anachokifanya kwetu, inaonyesha wazi vile rehema na huruma zake kwa mwanadamu zilivyo nyingi.
Yale mambo mabaya tunayotenda kwake, hayamfanyi asitupe pumzi yake, bado anaendelea kutupa fursa mbalimbali, tunaweza kujiona tupo sawa na wale wanaomcha katika roho na kweli.
Kama ni jua anatupa sote, kama ni mvua anatupa sote, kama ni uhai tunao wote, wakati mwingine unaweza kumkuta mtu anatenda dhambi haswa ila ana mafanikio makubwa ya kimwili. Kama ni mali anazo za kutosha na mafanikio mengine ya dunia hii.
Mtu mwingine pasipo kujua anaweza kuanza kuongea maneno ya kufuru, na yule aliye mwaminifu mbele za Mungu anaweza kujiona huenda kuna mahali anamkosea Mungu ndio maana hana hayo mafanikio.
Tunapaswa kuelewa kuwa upendo wa Mungu ni mkubwa mno, pamoja na yale makosa tunayoyafanya kila siku kwake na wakati mwingine hatutaki kutubu na kuacha, bado anatupa nafasi ya kubadilika.
Uvumilivu huu wa Mungu kwetu kutokana na upendo wake, utuondoe usingizini na kuona Mungu wetu anaona vizuri yale mabaya tunayoyatenda isipokuwa ametupa nafasi ya kujirekebisha na kumrudia Yeye.
Kupuuza kwetu nafasi tuliyopewa na Mungu, itatugharimu, kabla haijatugharimu turekebishe njia zetu mbaya, tumgeukie Yesu, Yeye yupo tayari kutusamehe dhambi zetu zote.
Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukaribisha kwenye kundi hili zuri la wasap la kusoma biblia kila siku na kutafakari, ni moja ya kundi linaloweza kukusaidia kumjua Mungu wako vizuri kupitia neno lake. Ukipenda hili wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uweze kuunganishwa kwenye kundi hili zuri.
Mwisho, nikukaribishe kwenye channel ya wasap kupata maarifa mbalimbali bonyeza link hii kujiunga=>>Samson Ernest | WhatsApp Channel
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana