Mungu ni punguani?

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286




1. Nimezama fikirani,
Kumsaka Punguani,
Aliyezua tafrani,
Mbinguni na duniani,
Nimemjua jamani,
Huyo Bwana Punguani.

2. Huyo Bwana Punguani,
Kaacha mkewe ndani,
Kajikunyata chumbani,
Mito yake ubavuni,
Yuko mpweke jamani,
Yeye kaenda kuzini.

3. Yeye kaenda kuzini,
Mumewe yuko kazini,
Watoto wako shuleni,
Uchafu upo chumbani,
Paka kalala jikoni,
Huyu pia punguani,

4. Huyu pia punguani,
Mshinda mtandaoni,
Mtu mvivu kazini,
Mwenye kibli moyoni,
Kapanga watu foleni,
Dharau iso kifani.

5. Dharau iso kifani,
Kwa walimu mashuleni,
Kushinda maofisini,
Na visimu mikononi,
Hawaogopi jamani,
Hawaendi darasani.

6. Hawaendi darasani,
Wanatoroka shuleni,
Wanashinda vijiweni,
Na msuba mkononi,
Hawafuzu mitihani,
Hawa ni mapunguani.

7. Hawa ni mapunguani,
Wasoenda shambani,
Hivi waja vuna nini?
Mikono yao laini,
Macho yao utosini,
Vya wenzao watamani.

8. Vya wenzao watamani,
Wawapore mkononi,
Hawana utu asilani,
Wamekuwa mahayawani,
Watoa roho mwilini,
Kama simba wa nyikani.

9. Kama simba wanyikani,
Wanasiasa nchini,
Kondoo wa zizini,
Mwenye ngozi laini,
Wameivaa mwilini,
Wamekuwa mafanani,

10. Wamekuwa mafanani,
Wapate kula maini,
Ni warongo si utani,
Wakiingia bungeni,
Wanaiponda ilani,
Hawa ni mapunguani.

11. Hawa ni mapunguani,
Imethibiti jamani,
Vikongwe wako shakani,
Tena wako hatarini,
Kwa hila zao jamani,
Roho zao zi shakani,

12. Roho zao zi shakani,
Hawana tena amani,
Wenye wekundu machoni,
Kwa moshi wa jikoni,
Eti waruka angani,
Wachawi wa kilingeni,

13. Wachawi wa kilingeni,
Wanga wapaa angani,
Watabana mafundoni,
Watia nuksi mwilini,
Hivi wana cheo gani?
Kama si mapunguani?

14. Kama si mapunguani?
Basi ni mahayawani,
Uchawi ni kitu gani,
Mwenyewe hasa n' nani?
Wa kuzuka uzeeni,
Asotoka ujanani?

15. Asotoka ujanani,
Namtafuta jamani,
Alofika baharini,
Bila kupita mtoni,
Wachawi wa utotoni,
Mbona hawaonekani?

16. Mbona hawaonekani?
Wachawi wa utotoni,
Tieni ndimi puani,
Utimu uhayawani,
Waso zama fikirani,
Mahala pao bomani,

17. Mahala pao bomani,
Mavuno yao jaani,
Waende mbio porini,
Na wagagae upwani,
Ni jaza ya punguani,
Wali mkavu chanoni,

18. Wali mkavu chanoni,
Wa kunata kiganjani,
Ni jaza ya punguani,
Alo muasi Manani,
Mchora nyota baoni,
Naye pia punguani?

19. Naye pia punguani,
Mchora nyota baoni,
Mjenzi wa kisirani,
Mweledi wa ufatani,
Watu hawaelewani,
Kisa huyu maluuni.

20. Kisa huyu maluuni,
Mjaza chuki moyoni,
Mke kalala chumbani,
Mume wake varandani,
Ndoa ziko hatarini,
Hawaishi kwa amani.

21. Hawaishi kwa amani,
Wenye kufanya udini,
Ukabila ni tufani,
Kimbunga kiso kifani,
Hatujafika fukweni,
Utalazi wafaani?

22. Utalazi wafaani,
Nawaomba zindukeni,
Yako mawili jueni,
Ni matatu tambueni,
Myashike akilini,
Myapambe ukutani.

23. Myapambe ukutani,
Yalo tutia kashani,
Mosi damu ya mwilini,
Asiliye viunoni,
Inapitia tumboni,
Kisha yaja duniani.

24. Kisha yaja duniani,
Na ng'aa ng'aa chumbani,
Sishangae aliani,
Ndio uzima eleweni,
Naomba nitajieni,
Asozaliwa jamani.

25. Asozaliwa jamani,
Hayupo duniani,
Jambo la pili shikeni,
Ni kuzaliwa jueni,
Mama huwa taabani,
Baba yuko furahani.

26. Baba yuko furahani,
Kapata mwana jamani,
Mtoto kitu thamani,
Ila si kwa punguani,
Ata mkana hadharani,
Alelewe umamani.

27. Alelewe umamani,
Kwa simanzi na huzuni,
Baba aranda njiani,
Wajomba na usukani,
Huno ni upunguani,
Mahala pake jaani.

28. Mahala pake jaani,
Zile chuki za kidini,
Popote ulimwenguni,
Naomba tafuteni,
Alafu nitajieni,
Aso na damu mwilini.

29. Aso na damu mwilini.
Mtajeni wenzanguni,
Watu toka Marekani,
Na hata wa Arabuni,
Walo juu aridhini,
Wana damu mishipani.

30. Wana damu mishipani,
Yenda mbio tambueni,
Hino damu ya thamani,
Imetuunga jamani,
Waja waso ithamini,
Wana matobo kichwani.

31. Wana matobo kichwani,
Wataka kwenda vitani,
Hupenda zua tafrani,
Waivuruge amani,
Tuwashinde wenzanguni,
Popote ulimwenguni.

32. Popote ulimwenguni,
Mwenye kwenda kanisani,
Biblia yake kwapani,
Na rozali mkononi,
Ana kitu cha thamani,
Damu yake ya mwilini.

33. Damu yake ya mwilini,
Yule wa msikitini,
Ina tafauti gani?
Na ya mwenda kanisani?
Hata asiye na dini ,
Yuko na damu mwilini.

34. Yuko na damu mwilini,
Mhindu na mpagani,
Watu walio na dini,
Na wale waso na dini.
Imewatia kashani,
Hino damu ya thamani.

35. Hino damu ya thamani,
Tunu toka kwa Manani,
Mwiko kuimwaga chini,
Kwa sababu za kihuni,
Mja sifanye utani,
Roho kutoka mwilini,

36. Roho kutoka mwilini,
Muosha awe kazini,
Asikose mkafini,
Aswaliwe kanisani,
Mwili ubebwe tusini,
Ukazikwe kaburini,

37. Ukazikwe kaburini,
Urejee mavumbini,
Uwe na hila tisini,
Kifo hakiwezekani,
Kifo la tatu jamani,
Yale mambo kumbukeni.

38. Yale mambo kumbukeni,
Yano tutia kashani,
Hata uwe kama nani,
Huto dumu maishani,
Matano yalo kashani,
Kifo la tatu jamani.

39. Kifo la tatu jamani,
La nne lipo njiani,
Tunu toka kwa Manani
Utanzania jamani,
Utaifa ni thamani,
Umeuzidi marijani.

40. Umeuzidi marijani,
Na vito vya Merelani,
Semeni wa visiwani,
Twawatazama usoni,
Na mseme kwa yakini
Kipi chenye thamani?

41. Kipi chenye thamani?
Kati ya hivi jamani,
Zanzibar ya Sultani,
Na Tanzania Amani,
Msiwe mapunguani,
Tanzania ni thamani.

42. Tanzania ni thamani,
Thamani kubwa jamani,
Tanganyika itupeni,
Ni zao la mkoloni,
Waliishinda Berlini,
Kambarage na Amani.

43. Kambarage na Amani,
Waliishinda Berlini,
Wakaipata thamani,
Ilo kubwa duniani,
Tuitunze kwa makini,
Tusiufanye utani.

44. Tusiufanye utani,
Kutunza hino thamani,
Utanzania jamani,
Ni la nne tambueni,
Mkumbuke ya thamani,
Yanotutia kashani,

45. Yanotutia kashani,
Yale matano jamani,
Rangi isitufitini,
Ukanda tuutupeni,
Ukabila na udini,
Mahala pake chooni.

46. Mahala pake chooni,
Yanotutenga jamani,
Na tuyabebe tusini,
Tuyazike kaburini,
Si mwajua visirani,
Vita wanaitamani?

47. Vita wanaitamani,
Hawa mapunguani,
Wallahi siwatukani,
Sindano tuwadungeni,
Hawajatimu kichwani,
Mkamilifu ni nani?

48. Mkamilifu ni nani,
Aloumbwa na Manani,
Aishiye Duniani,
Asiye na walakini,
Upungufu mwilini,
Ni la tano tambueni.

49. Ni la tano tambueni,
La kututia kashani,
Endapo tukiamini,
Sote tuna walakini,
Tutakumbuka hisani,
Tupuuze visirani.

50. Tupuuze visirani,
Wasokinai moyoni,
Wanamshinda shetani,
Kwa silaha za ghalani,
Hivi kuwe na amani
Watamuuzia nani?

51. Watamuuzia nani?
Silaha zao ghalani,
Dunia yetu jamani,
Yatikisika jueni,
Viumbe vya duniani,
Hakika vi hatarini.

52. Hakika vi hatarini,
Viumbe vya baharini,
Maji taka ya mjini,
Na yale ya viwandani,
Huingizwa baharini,
Huu si upunguani?

53. Huu si upunguani?
Kuua faru jamani,
Magogo ya msituni,
Na ndovu wa hifadhini,
Rasilimali hatarini,
Kupotezwa hifadhini.

54. Kupotezwa hifadhini,
Na hawa mapunguani,
Kikulacho maungoni,
Cha ishi mwako nguoni,
Tunalala nao ndani,
Hawa mapunguani.

55. Hawa mapunguani,
Tuna lala nao ndani,
Shime tuwafichueni,
Tulinde ndovu jamani,
Tuwatie kituteni,
Ahmadi kibindoni.

56. Ahmadi kibindoni,
Silaha i mkononi,
Mdharau majirani,
Naye pia punguani,
Ataanza fika nani,
Ashikwapo chumbani?

57. Ashikwapo chumbani?
Aanguke upenuni,
Awe na maiti ndani,
Au awe na tafrani,
Wa kwanza kufika nani?
Kama si wake jirani?

58. Kama si wake jirani,
Silaha ya kibindoni,
Awe na ndugu Manyoni?
Naye yu Mkanyageni?
Watotongwa fikirini,
Tusidharau jirani.

59. Tusidharau jirani,
Ninawaasa jamani,
Tumuepuke fatani,
Aso ipenda amani,
Mdharau hasa nani?
Kama si punguani?

60. Kama si punguani,
Niimpe cheo gani?
Mwenye ulevi kichwani,
Na miraa mkononi,
Ameshika usukani,
Abiria hatarini

61. Abiria hatarini,
Roho zao zi shakani
Alama barabarani,
Hazioni si utani,
Dereva ni majinuni
Ana wazimu rasini.

62. Ana wazimu rasini,
Mtumishi ofisini,
Hivi haki bei gani?
Anainadi sirini,
Hana haki masikini,
Penye rushwa si utani

63. Penye rushwa si utani,
Hakuna haki asilani,
Tia kura sandukuni,
Mtu aende bungeni,
Kura itapigwa chini,
Mkwasi hawezekani.

64. Mkwasi hawezekani,
Hata hospitalini,
Penye rushwa tambueni,
Katu hapangi foleni,
Mkwasi hawezekani
Hata pale bandarini,

65. Hata pale bandarini,
Mkwasi hana foleni,
Hili la rushwa jamani,
Ni sifa ya punguani,
Tuipinge hadharani,
Nawaasa jamani.

66. Nawaasa jamani,
Vijana wa vijijini,
Msiwe mapunguani,
Mkaamia mjini,
Mali nyingi za thamani,
Mtazipata shambani.

67. Mtazipata shambani,
Mlizoota ndotoni,
Kubwa muwe na imani,
Na subira mtimani,
Kazi adimu mjini,
Wasomi wako jiweni.

68. Wasomi wako jiweni,
Na vyeti toka chuoni,
Kazi adimu jamani
Hutangatanga njiani,
Huu si upunguani?
Kwa wa'lo madarakani?

69. Kwa wa'lo madarakani,
Watunga sera nchini,
Wakuu serikalini,
Na viongozi bungeni,
Wanafanya kazi gani?
Vijana wako shakani.

70. Vijana wako shakani,
Wenye kupenda kuzini,
Tena hawako makini,
Ni wazembe uwanjani,
Wana kiatu mguuni,
Hawana kinga kinywani.

71. Hawana kinga kinywani,
Tena wana jiamini,
Wazee wamo kundini,
Wenye ashiki jununi,
Hawa pia wana nini?
Kama si upunguani?

72. Kama si upunguani,
Sasa wana kitu gani,
UKIMWI upo jamani,
Nawambia si utani,
Ninyi mpo hatarini,
Vijana muwe makini.

73. Vijana muwe makini,
Mliokuwa vyuoni,
Wale wa makazini,
Na mlio mashambani,
Joka litawashikeni,
Msipokuwa makini.

74. Msipokuwa makini,
Uchumi u hatarini,
Hujiwezi kitandani,
Kazini aende nani?
Kijana aso makini,
Naye pia punguani.

75. Naye pia punguani,
Mzazi aso imani,
Mtupa mwana jaani,
Tumuweke kundi gani?
Mama huyu maluuni,
Hafai msikitini.

76. Hafai msikitini,
Kisalata maluuni,
Hatakiwi kanisani,
Mtu mwenye kisirani,
Watu hawaelewani,
Sababu upunguani.

77. Sababu upunguani,
Mtu huweza kubini,
Mtu mwenye ukunguni,
Shibe kwake yafaani?
Hawa ni mapunguani,
Wenye matobo kichwani.

78. Wenye matobo kichwani,
Wako wengi tambueni,
Wanasinzia bungeni,
Hawafiki majimboni,
Ngazi za ghorofani,
Wamezifanya katuni.

79. Wamezifanya katuni,
Hazina tena thamani,
Wamezitupa jaani,
Wasubiri kampeni,
Hawa nao wana nini?
Si bure upunguani.

80. Si bure upunguani,
Kutenda uso amini,
Mchana atangaza dini,
Usiku yu kilingeni,
Viongozi wa dini,
Wanatufundisha nini?

81. Wanatufundisha nini?
Kumbikumbi toka chini,
Kutamani vya angani,
Kavaa mbawa mwilini,
Kuwa ndege katamani,
Mchwa tamaa za nini?

82. Mchwa tamaa za nini?
Cha mno hasa nini?
Kikutoe chuguuni,
Uranderande angani,
Windo la nyoka nyikani,
Mchwa umepata nini?

83. Mchwa umepata nini?
Kwa hizo mbawa mwilini,
Tamaa huwa kichwani,
Mauti ni ya mkiani,
Mchwa naye punguani,
Mwenye matobo rasini.

84. Mwenye matobo rasini,
Ndiye bwana punguani,
Jambo haliwezekani,
Kwanini walitamani?
Waja juta maishani,
Ya mchwa kuyatamani.

85. Ya mchwa kuyatamani,
Kupata vuno angani,
Bandika mbawa begani,
Ka ndege wa angani,
Gundi iishe mwilini,
Puu uanguke chini.

86. Puu uanguke chini,
Sijue ufanye nini,
Njano nawausieni,
Masikio yategeni,
Uwezo uwe shinani,
Tamaa iwe tawini.

87. Tamaa iwe tawini,
Uwezo uwe shinani,
Mtafuzu mitihani,
Tamaa ikiwa chini,
Jamani upunguani,
Hivi kauumba nani?

88. Hivi kauumba nani?
Huu upunguani,
Nacho kiumbe jamani,
Kilichopo duniani,
Nimezama vitabuni,
Nimeisoma Qurani.

89. Nimeisoma Qurani
Biblia kwa makini,
Kila kitu duniani,
Kimeumbwa na Manani,
Hivi upunguani,
Ameuumba nani?

90. Ameuumba nani?
Huno upunguani,
Huwezi umba tufani,
Na usiwe majinuni,
Muumba upunguani,
Tuumpe cheo gani?

91. Tuumpe cheo gani,
Muumba upunguani,
Nimezama methalini,
Kwa mfalme Sulemani,
Mungu kafanya shetani,
Kwa siku ya ushetani,

92. Kwa siku ya ushetani,
Mungu kaumba shetani,
Kula upepo kinywani,
Ziwe timamu kichwani,
Kama kifo kinjiani,
Akili zatufaani?

93. Akili zatufaani,
Kama moja la zamani,
Lamfika punguani,
Mwenye akili makini,
Na mwenye jeshi makini,
Kifo humpiga chini,

94. Kifo humpiga chini,
Mganga hospitalini,
Aso kufa ni Manani,
Ukweli utambueni,
Kuwa kaumba Manani,
Huu upunguani.

95. Huu upunguani,
Hakuwa nao shetani,
Akatiwa ujununi,
Ibilisi rasini,
Akazua tafrani,
Mbinguni na duniani.

96. Mbinguni na duniani,
Muumba ni Manani,
Kilichopo rasini,
Mwa Ibilisi jamani,
Amekiumba nani?
Tafauti na Manani.

97. Tafauti na Manani,
Sasa kauumba nani?
Mungu ni punguani?
Baba wa huo jamani?
Naomba jibu makini,
Hasa kwa wanazuoni

98. Hasa kwa wanazuoni,
Wenye ilimu za dini,
Malenga wa wazamani,
Na wa sasa sogeeni,
Tutoe tongo machoni,
Tumjue punguani.

99. Tumjue punguani,
Mwenye matundu kichwani,
Pia kamuumba nani,
Huyo bwana punguani,
Mungu ana cheo gani?
Kama si punguani?

100. Wino wa zafarani,
Umeisha chupani,
Ya manjano zafarani,
Iliyokwisha si utani,
Sasa niko mwishoni,
Ninasema kwahereni.


Njano5.
0784845394
 
MUNGU NI PUNGUANI?

1. Nimezama fikirani,
Kumsaka Punguani,
Aliyezua tafrani,
Mbinguni na duniani,
Nimemjua jamani,
Huyo Bwana Punguani.

2. Huyo Bwana Punguani,
Kaacha mkewe ndani,
Kajikunyata chumbani,
Mito yake ubavuni,
Yuko mpweke jamani,
Yeye kaenda kuzini.

3. Yeye kaenda kuzini,
Mumewe yuko kazini,
Watoto wako shuleni,
Uchafu upo chumbani,
Paka kalala jikoni,
Huyu pia punguani,

4. Huyu pia punguani,
Mshinda mtandaoni,
Mtu mvivu kazini,
Mwenye kibli moyoni,
Kapanga watu foleni,
Dharau iso kifani.

5. Dharau iso kifani,
Kwa walimu mashuleni,
Kushinda maofisini,
Na visimu mikononi,
Hawaogopi jamani,
Hawaendi darasani.

6. Hawaendi darasani,
Wanatoroka shuleni,
Wanashinda vijiweni,
Na msuba mkononi,
Hawafuzu mitihani,
Hawa ni mapunguani.

7. Hawa ni mapunguani,
Wasoenda shambani,
Hivi waja vuna nini?
Mikono yao laini,
Macho yao utosini,
Vya wenzao watamani.

8. Vya wenzao watamani,
Wawapore mkononi,
Hawana utu asilani,
Wamekuwa mahayawani,
Watoa roho mwilini,
Kama simba wa nyikani.

9. Kama simba wanyikani,
Wanasiasa nchini,
Kondoo wa zizini,
Mwenye ngozi laini,
Wameivaa mwilini,
Wamekuwa mafanani,

10. Wamekuwa mafanani,
Wapate kula maini,
Ni warongo si utani,
Wakiingia bungeni,
Wanaiponda ilani,
Hawa ni mapunguani.

11. Hawa ni mapunguani,
Imethibiti jamani,
Vikongwe wako shakani,
Tena wako hatarini,
Kwa hila zao jamani,
Roho zao zi shakani,

12. Roho zao zi shakani,
Hawana tena amani,
Wenye wekundu machoni,
Kwa moshi wa jikoni,
Eti waruka angani,
Wachawi wa kilingeni,

13. Wachawi wa kilingeni,
Wanga wapaa angani,
Watabana mafundoni,
Watia nuksi mwilini,
Hivi wana cheo gani?
Kama si mapunguani?

14. Kama si mapunguani?
Basi ni mahayawani,
Uchawi ni kitu gani,
Mwenyewe hasa n’ nani?
Wa kuzuka uzeeni,
Asotoka ujanani?

15. Asotoka ujanani,
Namtafuta jamani,
Alofika baharini,
Bila kupita mtoni,
Wachawi wa utotoni,
Mbona hawaonekani?

16. Mbona hawaonekani?
Wachawi wa utotoni,
Tieni ndimi puani,
Utimu uhayawani,
Waso zama fikirani,
Mahala pao bomani,

17. Mahala pao bomani,
Mavuno yao jaani,
Waende mbio porini,
Na wagagae upwani,
Ni jaza ya punguani,
Wali mkavu chanoni,

18. Wali mkavu chanoni,
Wa kunata kiganjani,
Ni jaza ya punguani,
Alo muasi Manani,
Mchora nyota baoni,
Naye pia punguani?

19. Naye pia punguani,
Mchora nyota baoni,
Mjenzi wa kisirani,
Mweledi wa ufatani,
Watu hawaelewani,
Kisa huyu maluuni.

20. Kisa huyu maluuni,
Mjaza chuki moyoni,
Mke kalala chumbani,
Mume wake varandani,
Ndoa ziko hatarini,
Hawaishi kwa amani.

21. Hawaishi kwa amani,
Wenye kufanya udini,
Ukabila ni tufani,
Kimbunga kiso kifani,
Hatujafika fukweni,
Utalazi wafaani?

22. Utalazi wafaani,
Nawaomba zindukeni,
Yako mawili jueni,
Ni matatu tambueni,
Myashike akilini,
Myapambe ukutani.

23. Myapambe ukutani,
Yalo tutia kashani,
Mosi damu ya mwilini,
Asiliye viunoni,
Inapitia tumboni,
Kisha yaja duniani.

24. Kisha yaja duniani,
Na ng’aa ng’aa chumbani,
Sishangae aliani,
Ndio uzima eleweni,
Naomba nitajieni,
Asozaliwa jamani.

25. Asozaliwa jamani,
Hayupo duniani,
Jambo la pili shikeni,
Ni kuzaliwa jueni,
Mama huwa taabani,
Baba yuko furahani.

26. Baba yuko furahani,
Kapata mwana jamani,
Mtoto kitu thamani,
Ila si kwa punguani,
Ata mkana hadharani,
Alelewe umamani.

27. Alelewe umamani,
Kwa simanzi na huzuni,
Baba aranda njiani,
Wajomba na usukani,
Huno ni upunguani,
Mahala pake jaani.

28. Mahala pake jaani,
Zile chuki za kidini,
Popote ulimwenguni,
Naomba tafuteni,
Alafu nitajieni,
Aso na damu mwilini.

29. Aso na damu mwilini.
Mtajeni wenzanguni,
Watu toka Marekani,
Na hata wa Arabuni,
Walo juu aridhini,
Wana damu mishipani.

30. Wana damu mishipani,
Yenda mbio tambueni,
Hino damu ya thamani,
Imetuunga jamani,
Waja waso ithamini,
Wana matobo kichwani.

31. Wana matobo kichwani,
Wataka kwenda vitani,
Hupenda zua tafrani,
Waivuruge amani,
Tuwashinde wenzanguni,
Popote ulimwenguni.

32. Popote ulimwenguni,
Mwenye kwenda kanisani,
Biblia yake kwapani,
Na rozali mkononi,
Ana kitu cha thamani,
Damu yake ya mwilini.

33. Damu yake ya mwilini,
Yule wa msikitini,
Ina tafauti gani?
Na ya mwenda kanisani?
Hata asiye na dini ,
Yuko na damu mwilini.

34. Yuko na damu mwilini,
Mhindu na mpagani,
Watu walio na dini,
Na wale waso na dini.
Imewatia kashani,
Hino damu ya thamani.

35. Hino damu ya thamani,
Tunu toka kwa Manani,
Mwiko kuimwaga chini,
Kwa sababu za kihuni,
Mja sifanye utani,
Roho kutoka mwilini,

36. Roho kutoka mwilini,
Muosha awe kazini,
Asikose mkafini,
Aswaliwe kanisani,
Mwili ubebwe tusini,
Ukazikwe kaburini,

37. Ukazikwe kaburini,
Urejee mavumbini,
Uwe na hila tisini,
Kifo hakiwezekani,
Kifo la tatu jamani,
Yale mambo kumbukeni.

38. Yale mambo kumbukeni,
Yano tutia kashani,
Hata uwe kama nani,
Huto dumu maishani,
Matano yalo kashani,
Kifo la tatu jamani.

39. Kifo la tatu jamani,
La nne lipo njiani,
Tunu toka kwa Manani
Utanzania jamani,
Utaifa ni thamani,
Umeuzidi marijani.

40. Umeuzidi marijani,
Na vito vya Merelani,
Semeni wa visiwani,
Twawatazama usoni,
Na mseme kwa yakini
Kipi chenye thamani?

41. Kipi chenye thamani?
Kati ya hivi jamani,
Zanzibar ya Sultani,
Na Tanzania Amani,
Msiwe mapunguani,
Tanzania ni thamani.

42. Tanzania ni thamani,
Thamani kubwa jamani,
Tanganyika itupeni,
Ni zao la mkoloni,
Waliishinda Berlini,
Kambarage na Amani.

43. Kambarage na Amani,
Waliishinda Berlini,
Wakaipata thamani,
Ilo kubwa duniani,
Tuitunze kwa makini,
Tusiufanye utani.

44. Tusiufanye utani,
Kutunza hino thamani,
Utanzania jamani,
Ni la nne tambueni,
Mkumbuke ya thamani,
Yanotutia kashani,

45. Yanotutia kashani,
Yale matano jamani,
Rangi isitufitini,
Ukanda tuutupeni,
Ukabila na udini,
Mahala pake chooni.

46. Mahala pake chooni,
Yanotutenga jamani,
Na tuyabebe tusini,
Tuyazike kaburini,
Si mwajua visirani,
Vita wanaitamani?

47. Vita wanaitamani,
Hawa mapunguani,
Wallahi siwatukani,
Sindano tuwadungeni,
Hawajatimu kichwani,
Mkamilifu ni nani?

48. Mkamilifu ni nani,
Aloumbwa na Manani,
Aishiye Duniani,
Asiye na walakini,
Upungufu mwilini,
Ni la tano tambueni.

49. Ni la tano tambueni,
La kututia kashani,
Endapo tukiamini,
Sote tuna walakini,
Tutakumbuka hisani,
Tupuuze visirani.

50. Tupuuze visirani,
Wasokinai moyoni,
Wanamshinda shetani,
Kwa silaha za ghalani,
Hivi kuwe na amani
Watamuuzia nani?

51. Watamuuzia nani?
Silaha zao ghalani,
Dunia yetu jamani,
Yatikisika jueni,
Viumbe vya duniani,
Hakika vi hatarini.

52. Hakika vi hatarini,
Viumbe vya baharini,
Maji taka ya mjini,
Na yale ya viwandani,
Huingizwa baharini,
Huu si upunguani?

53. Huu si upunguani?
Kuua faru jamani,
Magogo ya msituni,
Na ndovu wa hifadhini,
Rasilimali hatarini,
Kupotezwa hifadhini.

54. Kupotezwa hifadhini,
Na hawa mapunguani,
Kikulacho maungoni,
Cha ishi mwako nguoni,
Tunalala nao ndani,
Hawa mapunguani.

55. Hawa mapunguani,
Tuna lala nao ndani,
Shime tuwafichueni,
Tulinde ndovu jamani,
Tuwatie kituteni,
Ahmadi kibindoni.

56. Ahmadi kibindoni,
Silaha i mkononi,
Mdharau majirani,
Naye pia punguani,
Ataanza fika nani,
Ashikwapo chumbani?

57. Ashikwapo chumbani?
Aanguke upenuni,
Awe na maiti ndani,
Au awe na tafrani,
Wa kwanza kufika nani?
Kama si wake jirani?

58. Kama si wake jirani,
Silaha ya kibindoni,
Awe na ndugu Manyoni?
Naye yu Mkanyageni?
Watotongwa fikirini,
Tusidharau jirani.

59. Tusidharau jirani,
Ninawaasa jamani,
Tumuepuke fatani,
Aso ipenda amani,
Mdharau hasa nani?
Kama si punguani?

60. Kama si punguani,
Niimpe cheo gani?
Mwenye ulevi kichwani,
Na miraa mkononi,
Ameshika usukani,
Abiria hatarini

61. Abiria hatarini,
Roho zao zi shakani
Alama barabarani,
Hazioni si utani,
Dereva ni majinuni
Ana wazimu rasini.

62. Ana wazimu rasini,
Mtumishi ofisini,
Hivi haki bei gani?
Anainadi sirini,
Hana haki masikini,
Penye rushwa si utani

63. Penye rushwa si utani,
Hakuna haki asilani,
Tia kura sandukuni,
Mtu aende bungeni,
Kura itapigwa chini,
Mkwasi hawezekani.

64. Mkwasi hawezekani,
Hata hospitalini,
Penye rushwa tambueni,
Katu hapangi foleni,
Mkwasi hawezekani
Hata pale bandarini,

65. Hata pale bandarini,
Mkwasi hana foleni,
Hili la rushwa jamani,
Ni sifa ya punguani,
Tuipinge hadharani,
Nawaasa jamani.

66. Nawaasa jamani,
Vijana wa vijijini,
Msiwe mapunguani,
Mkaamia mjini,
Mali nyingi za thamani,
Mtazipata shambani.

67. Mtazipata shambani,
Mlizoota ndotoni,
Kubwa muwe na imani,
Na subira mtimani,
Kazi adimu mjini,
Wasomi wako jiweni.

68. Wasomi wako jiweni,
Na vyeti toka chuoni,
Kazi adimu jamani
Hutangatanga njiani,
Huu si upunguani?
Kwa wa’lo madarakani?

69. Kwa wa’lo madarakani,
Watunga sera nchini,
Wakuu serikalini,
Na viongozi bungeni,
Wanafanya kazi gani?
Vijana wako shakani.

70. Vijana wako shakani,
Wenye kupenda kuzini,
Tena hawako makini,
Ni wazembe uwanjani,
Wana kiatu mguuni,
Hawana kinga kinywani.

71. Hawana kinga kinywani,
Tena wana jiamini,
Wazee wamo kundini,
Wenye ashiki jununi,
Hawa pia wana nini?
Kama si upunguani?

72. Kama si upunguani,
Sasa wana kitu gani,
UKIMWI upo jamani,
Nawambia si utani,
Ninyi mpo hatarini,
Vijana muwe makini.

73. Vijana muwe makini,
Mliokuwa vyuoni,
Wale wa makazini,
Na mlio mashambani,
Joka litawashikeni,
Msipokuwa makini.

74. Msipokuwa makini,
Uchumi u hatarini,
Hujiwezi kitandani,
Kazini aende nani?
Kijana aso makini,
Naye pia punguani.

75. Naye pia punguani,
Mzazi aso imani,
Mtupa mwana jaani,
Tumuweke kundi gani?
Mama huyu maluuni,
Hafai msikitini.

76. Hafai msikitini,
Kisalata maluuni,
Hatakiwi kanisani,
Mtu mwenye kisirani,
Watu hawaelewani,
Sababu upunguani.

77. Sababu upunguani,
Mtu huweza kubini,
Mtu mwenye ukunguni,
Shibe kwake yafaani?
Hawa ni mapunguani,
Wenye matobo kichwani.

78. Wenye matobo kichwani,
Wako wengi tambueni,
Wanasinzia bungeni,
Hawafiki majimboni,
Ngazi za ghorofani,
Wamezifanya katuni.

79. Wamezifanya katuni,
Hazina tena thamani,
Wamezitupa jaani,
Wasubiri kampeni,
Hawa nao wana nini?
Si bure upunguani.

80. Si bure upunguani,
Kutenda uso amini,
Mchana atangaza dini,
Usiku yu kilingeni,
Viongozi wa dini,
Wanatufundisha nini?

81. Wanatufundisha nini?
Kumbikumbi toka chini,
Kutamani vya angani,
Kavaa mbawa mwilini,
Kuwa ndege katamani,
Mchwa tamaa za nini?

82. Mchwa tamaa za nini?
Cha mno hasa nini?
Kikutoe chuguuni,
Uranderande angani,
Windo la nyoka nyikani,
Mchwa umepata nini?

83. Mchwa umepata nini?
Kwa hizo mbawa mwilini,
Tamaa huwa kichwani,
Mauti ni ya mkiani,
Mchwa naye punguani,
Mwenye matobo rasini.

84. Mwenye matobo rasini,
Ndiye bwana punguani,
Jambo haliwezekani,
Kwanini walitamani?
Waja juta maishani,
Ya mchwa kuyatamani.

85. Ya mchwa kuyatamani,
Kupata vuno angani,
Bandika mbawa begani,
Ka ndege wa angani,
Gundi iishe mwilini,
Puu uanguke chini.

86. Puu uanguke chini,
Sijue ufanye nini,
Njano nawausieni,
Masikio yategeni,
Uwezo uwe shinani,
Tamaa iwe tawini.

87. Tamaa iwe tawini,
Uwezo uwe shinani,
Mtafuzu mitihani,
Tamaa ikiwa chini,
Jamani upunguani,
Hivi kauumba nani?

88. Hivi kauumba nani?
Huu upunguani,
Nacho kiumbe jamani,
Kilichopo duniani,
Nimezama vitabuni,
Nimeisoma Qurani.

89. Nimeisoma Qurani
Biblia kwa makini,
Kila kitu duniani,
Kimeumbwa na Manani,
Hivi upunguani,
Ameuumba nani?

90. Ameuumba nani?
Huno upunguani,
Huwezi umba tufani,
Na usiwe majinuni,
Muumba upunguani,
Tuumpe cheo gani?

91. Tuumpe cheo gani,
Muumba upunguani,
Nimezama methalini,
Kwa mfalme Sulemani,
Mungu kafanya shetani,
Kwa siku ya ushetani,

92. Kwa siku ya ushetani,
Mungu kaumba shetani,
Kula upepo kinywani,
Ziwe timamu kichwani,
Kama kifo kinjiani,
Akili zatufaani?

93. Akili zatufaani,
Kama moja la zamani,
Lamfika punguani,
Mwenye akili makini,
Na mwenye jeshi makini,
Kifo humpiga chini,

94. Kifo humpiga chini,
Mganga hospitalini,
Aso kufa ni Manani,
Ukweli utambueni,
Kuwa kaumba Manani,
Huu upunguani.

95. Huu upunguani,
Hakuwa nao shetani,
Akatiwa ujununi,
Ibilisi rasini,
Akazua tafrani,
Mbinguni na duniani.

96. Mbinguni na duniani,
Muumba ni Manani,
Kilichopo rasini,
Mwa Ibilisi jamani,
Amekiumba nani?
Tafauti na Manani.

97. Tafauti na Manani,
Sasa kauumba nani?
Mungu ni punguani?
Baba wa huo jamani?
Naomba jibu makini,
Hasa kwa wanazuoni

98. Hasa kwa wanazuoni,
Wenye ilimu za dini,
Malenga wa wazamani,
Na wa sasa sogeeni,
Tutoe tongo machoni,
Tumjue punguani.

99. Tumjue punguani,
Mwenye matundu kichwani,
Pia kamuumba nani,
Huyo bwana punguani,
Mungu ana cheo gani?
Kama si punguani?

100. Wino wa zafarani,
Umeisha chupani,
Ya manjano zafarani,
Iliyokwisha si utani,
Sasa niko mwishoni,
Ninasema kwahereni.

Njano5.
0784845394
 
Kuna watu mna vipaji... Du! Jipe moyo huenda ukaamsha waliolala na kutiwa mifukoni.
^^
 
96. Mbinguni na duniani, Muumba ni Manani, Kilichopo rasini,
Mwa Ibilisi jamani, Amekiumba nani? Tafauti na Manani.

97. Tafauti na Manani, Sasa kauumba nani? Mungu ni punguani? Baba wa huo jamani?
Naomba jibu makini, Hasa kwa wanazuoni
Well mimi si mwanazuoni hila ni hivi

God is a Predicate in philosophy while politics exists; thus using reduction ad absurdum in god as a logic to govern our every day lives is close to insanity; we are better of concentrating on a posteriori that someone decisions or comments in our society might have huge implications in our daily lives than the notion of god wisdom in guiding us.

No wonder the bible says "Render unto Caesar the things that are Caesar's, and unto God the things that are God's" na sisi kama raia tuna wajibu wa ku-promote a secular society kwasababu kutumia dini kwenye siasa is merely an escape route in explaining challenges faced or just lack of conviction on what ones sells. Thus using the god's people to achieve goals is just a short cut of not having to persuade people in politics.

Mungu ausiki na siasa.
 
badilisha heading mkuu mungu anawezaje kuwa punguani? ulimaanisha Mungu???
 
1.tukiwa na watu makini, kama huyu mghani,
Rushwa itakuwa taabani,
yatakonda mapunguani.
2.Yatakonda mapunguani,
yasojua maana ya amani,
wanaotegemea wageni,
kuondolewa umaskini.
3.wanaotegemea wageni,
kuondolewa umaskini,
tusiwape kura mwakani,
bali tuwapige chini.
4.Bali tuwapige chini,
wote wenye akili duni,
kutwa kucha angani,
na mabakuli mkononi,
eti wapunguziwe madeni!
5.Eti wapunguziwe madeni,
wakati hapa nchini,
kuna utajiri jamani,
kama si upunguani,
basi ni upumbavu pipani.
 
Heading yako hata kama imekaa kama swali lakini tayari unamdhihaki our creator.unaweza ukawa una kitu kizuri cha kuwafikishia wanajamii ujumbe lakin jinsi unavyo uwasilisha ujumbe inakuwa ujuha,ukichaaa,unakuwa kama huja-elimika,next time uwe na adabu na heshima kwa kuleta mada hapa maana unakera na vichwa visivyo na mantiki
 

Kweli aisee huyu jamaa anamkosea heshima kabisa MUNGU.
Mijitu mingine bhana akili zao sidhani kama zipo sawa.
 
ACT wameshakubali yaishe mmeamua kujikita kwenye kazi ya sanaa.
 
mods kama jukwaa la mashahir lipo mpeleken huyu muumin wa kitliya mkumbo huko mana anatukera na ghani zake zinazo muambatanisha mungu na thihaka!
 
Kweli aisee huyu jamaa anamkosea heshima kabisa MUNGU.
Mijitu mingine bhana akili zao sidhani kama zipo sawa.

USIWE UNAONGEA TU, ACHA UVIVU, SOMA HOJA ZILIZOIBULIWA NA SHAIRI KISHA ZIJIBU.

Hivi kauumba nani?
Huu upunguani,
Nacho kiumbe jamani,
Kilichopo duniani,
Nimezama vitabuni,
Nimeisoma Qurani.

89. Nimeisoma Qurani
Biblia kwa makini,
Kila kitu duniani,
Kimeumbwa na Manani,
Hivi upunguani,
Ameuumba nani?

90. Ameuumba nani?
Huno upunguani,
Huwezi umba tufani,
Na usiwe majinuni,
Muumba upunguani,
Tuumpe cheo gani?

91. Tuumpe cheo gani,
Muumba upunguani,
Nimezama methalini,
Kwa mfalme Sulemani,
Mungu kafanya shetani,
Kwa siku ya ushetani,

 
mods kama jukwaa la mashahir lipo mpeleken huyu muumin wa kitliya mkumbo huko mana anatukera na ghani zake zinazo muambatanisha mungu na thihaka!

acha chuki za kike wewe,,,,, kwani siasa haiwezi kuzungumzwa kwa kutumia lugha ya picha au kishairi???
 
Rejea maneno yko niliyoyatia rangi ya buluu, huenda hujui maana ya siasa ndio maana ukasema mungu hausiki na siasa, soma shairi hili chini hasa zingatia maneno ya wino mwekundu huenda utajua maana ya siasa na kwa kiwango gani huwezi kumtenganisha mungu na siasa.


SIASA MJUE NJIA, MAAMUZI KUFIKIA.
SIASA MNYAMA GANI(JIBU)

Nimezama mwituni, kumtafuta mnyama,
Mwenye nguvu duniani, leo na keshokiama,
Atajwa msikitini, kanisani wa msema,
Haliwi jambo mwituni, bila ya huyomnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Naanzia shuleni, watoto wanaposoma,
Wanao soma vyuoni, na shahada za heshima,
Ngumbaru ipo kundini, unyago akina mama,
Elimu yetu nchini, huongozwa na mnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Uende hospitalini, na walipo wakulima,
Kwenye sekta ya madini, na kwa wapiga ngoma,
Utalii wa mbugani, na uchezaji wa sinema,
Kote huko tambueni, mratibu ni mnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Siasa ndio mnyama, Lutumbo katuambia,
Siasa ni kitu chema, katika yetu dunia,
Siasa njia ya umma, maamuzi kufikia,
Siasa si kama sima, bali maji nawaambia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Siasa kitu lazima, katu huwezi kimbia,
Waweza ikacha sima, maji huwezi susia,
Hata ngazi ya boma, siasa waitumia,
Siasa ukiitema, jua umeangamia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Kuna siasa ya chama, kimoja nawaambia,
Kila shauri la umma, chama hujiamulia,
Bunge huwa maamuma, muhuri hushikilia,
Jambo lipite kwa Chama, bunge lalishadidia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Zipoza demokrasia, vyama vingi nawambia,
Mfano za Tanzania, na uingereza pia,
Vyama hushindania, magogoni kuingia,
Rais kwa Tanzania, waziri kwa malikia
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Siasa ndani ya vyama, huko hazikuanzia,
Ilianza toka zama, kabla ya hino dunia,
Furkani nimeisoma, sikuiacha biblia,
Malaika na Karima, pia wanaitumia,
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Siasa za huko ahera, kiongozi ni Jalia,
Huongoza msafara, waja wakafuatia,
Mwenye kufanya harara, jeuri akajitia,
Atakuwa ni asira, wa shetani nawambia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Muumba ndio kinara, wa mbinguni nadunia,
Maisha huyachora, na njia hutupangia,
Hupata njema ijara, mwenye kumsujudia,
Hupata kubwa hasara, mwenye kupuuzia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Muumba ndio kinara, wa mbinguni nadunia,
Maisha huyachora, na njia hutupangia,
Hupata njema ijara, mwenye kumsujudia,
Hupata kubwa hasara, mwenye kupuuzia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Nani alipiga kura? Munguwe kumchagua,
Mjibu pasi kufura, kweli mpate ijua,
Hapana si masihara, si punde mtagundua,
Tena sifanye papara, siasa kuchambua.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.


Siasa za kifalme, mfano za Saudia,
Mwana hasa wa kiume, kiti ndio hukalia,
Koo iloshika kome, dola huishikilia,
Mfalme ndio sime, na pia huwa pazia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Zipo za kidikteta, kama zile za Mobutu,
Wengine panga huzifuta, pia wapo wa mtutu,
Umma wote hufyata, mbele ya miungu watu,
Kila mwenye kutukuta, ni mbwa mbele yachatu.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Dikteta awe katili, mbona mtaumwa sana,
Siombe awe jahili, mtapoteza amana,
Tena akiwa bahili, wananchi hukondeana,
Kiongozi bahaluli, asiaminiwe tena.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Samaki awape nyoka, mkate awape mawe,
Nani kashindwa ondoka, kisa halina mauwe?
Ya msingi wanataka, viongozi waelewe,
Wakichoka kuboboka, watawapopoa mawe.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Dikteta awe rahimu, ndipo mtanufaika,
Rasini awe timamu, na tena mshaurika,
Mtakula keki tamu, mafurushi mtashika,
Tripoli yajilaumu, Gaddafi kudondoka.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.

Nikitazama chupani, sioni kitu jamani,
Wino wangu wa thamani, ya manjano zafarani,
Niko mengi rasini, wino umetufitini,
Mwenye nao sinihini, naomba niuzieni
Mmeshindwa nidhamini, kwa kifupi kwaherini.

Njano5
0784845394

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/719485-siasa-mjue-njia-maamuzi-kufikia.html

 

Sina tatizo na verse zako za siasa isipokuwa kwenye metaphysical za mungu hapo ndio kuna unmediated argument kwenye shairi lako.

The analogy of god and politics is a forced issue kwa sababu humans shape their politics everday and you have'nt proved any cause of effect kwenye shairi lako kiasi kwamba argument isimame yenyewe kuna mungu kwenye siasa. Isitoshe the premises are mainly ontological arguments lacking scholastism and subjectivism making it a good read to uninformed audience which is not inclined to question in a transcendent god even in poetic semantics.

Contrary to today demands whereby even poets (not that I am) are also forced to consider epistemology; that being the case I know politics is ever evolving, politics is never the same in every society as you have mentioned it too, it is humans who debate, decide and build the mechanism of politics the variety of it makes it justifiable it is a human act depending on their understanding.

Thus a theodicy argument is no longer accepted in justifying causes of politics rather the realism of acts which are visible to mankind and could be justified.

That is to say mungu hausiki na siasa and if we are to evolve, deism is the answer which might help us make better judgements and demand on the bases facts; same way many developed nations have done instead of adding this transcendent thinking in politics which have no justification.
 
Hili la kumdhihaki Mungu hata mimi limenikera. Mkuu aliyeleta uzi ana ujumbe mzuri sana ila hili la kumdhihaki Mungu amechemka kwa kweli, imeondoka ladha nzima ya maudhui

 
Hili la kumdhihaki Mungu hata mimi limenikera. Mkuu aliyeleta uzi ana ujumbe mzuri sana ila hili la kumdhihaki Mungu amechemka kwa kweli, imeondoka ladha nzima ya maudhui

Hapa mungu hajadhiakiwa,, bali nimeibua swali si kama hoja yenye kuhitaji majibu,,,,,

rejea methali 16:4

Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…