Jo Africa Tz
Member
- Jul 23, 2019
- 10
- 10
Kwa wale ambao wamesoma historia ya falme za zamani na tamaduni za watu wa kale hususan mashariki ya kati, basi jina hili "Hammurabi" haliwezi kuwa geni. Katika zama hizo za ufalme wa Babeli, alikuwako kiongozi wa ngazi ya juu kabisa katika dola hiyo iliyoitikisa dunia ya enzi hizo kwa miaka mingi.
Kiongozi huyo alitengeneza sheria kali ambazo kwake yeye aliamini na kuaminisha watu kuwa ametumwa na Mungu na kwamba uwepo wake duniani ilikuwa ni kutimiza amri na maagizo ya Mungu moja kwa moja kwa mwanadamu. Sheria zake nyingi zilizungumzia habari ya kutoa hukumu ya kifo kwa mtu aliyekutwa na kosa.
Mataifa mengi baada ya karne nyingi kupita, na kutuma wasomi wao kwenda vyuo vikuu vya zamani nje ya nchi kupata elimu, wasomi hao walisoma habari za kiongozi huyu mashuhuri na sheria zake, na hivyo kupelekea mataifa mengi kutengeneza katiba za nchi zao kulingana na sheria zile ambazo kwa kitaalam zinaitwa "Hammurabi's Codes of Law".
Japo yapo mataifa ambayo yalitengeneza katiba zao kufuata amri kumi za Mungu almaarufu kama "Mosaic Laws", ama "The Ten Commandments", yapo mataifa mengi ambayo takriban asilimia 80 ya sheria zao ni zile ambazo zilitengenezwa na Hammurabi. Kwa namna moja ama nyingine, ukisoma sheria hizo za Hammurabi, zinaweza kukupa "Solutions" za matatizo yako na watesi wako, tena zingine ni nzuri kabisa na ukizitafakari zimejaa hekima. Lakini nyingi zinatoa adhabu ya kifo.
Utofauti kati ya amri kumi za Mungu na zile ambazo alizitengeneza Hammurabi ambaye pia alisema ametumwa na Mungu, kwenye suala la kifo, Mungu wa Musa anasema "Usiue", ila Mungu wa Hammurabi anasema "Ua".
Ni kweli mambo ya serikali za kidunia tangu enzi hizo na hata enzi hizi, zinafuata amri ya Mungu wa Hammurabi. Hakuna hata serikali moja katika dunia hii ambayo inafuata AMRI KUMI ZA MUNGU, karibia zote zinafuata kwa asilimia kubwa amri alizotengeneza Hammurabi.
Polisi, Jeshi, Magereza, Sheria, Mahakama, Mahakimu, Wanasheria, Pingu, Silaha za Kivita na Watawala, vyote kwa pamoja ni ishara ya kuwepo kwa tabaka la kinyonyaji, tabaka la kikatili, tabaka la kibabe, tabaka la wenye nguvu, na mwisho wa yote, tabaka la waoga, wasioweza kutembea wakiwa huru na kujiamini bila ya jeshi na silaha. Tabaka la wachoyo na wabinafsi wasioweza kutumia mali za umma na umma wenyewe, wao wakiwa hata barabarani, barabara ambayo ni mali ya umma, wao hupenda wasipishane na mtu, mara wakitaka kupita, basi hutuma jeshi na polisi kufukuza umma wapishe njiani, kisha hupita kwa mwendo kasi kana kwamba ni wagonjwa mahututi. Wao hupenda kutukuzwa kwa vyeo vikubwa na kunyenyekewa, ni tabaka linalolala rasi ya tumaini jema na kuamkia uri ya wakaldayo. Wana mikono mirefu na matumbo mapana. Mara uonapo uwepo wa mambo hayo mbele yako, ujue Hammurabi na Babeli yake haijafa, bali iko hai na inafanya kazi usiku na mchana.
Mtu mmoja aliwahi kuuliza, ya kwamba haiwezekani watu wakaishi bila ya serikali? Hakuwahi kupata majibu maana mtu huyo hakuweza kupata nafasi ya kuzaliwa. Historia inatufundisha mambo mengi, ndiyo maana wale wasioijua historia hawana budi kuirudia.
Issa bin Mariam ama Yesu Kristo hata siku moja hakuweza kuonesha nia ya kuwania kiti chochote cha uongozi katika serikali ya kidunia, japo utawala wake ulikuwa ni ule wa kiroho ambao alipotangaza kuwa yeye ni mfalme, wafalme wa kidunia hawakumwelewa maana hawakuweza kuona akiwa na jeshi, polisi, silaha za kivita, gereza wala katiba. Hakuwa na ikulu wala watumishi wengi kama walivyo watawala wa dunia ambao wao wanao watumishi hadi wa kuwatawaza mara watokapo maliwatoni. Lakini mambo haya ya kiserikali na jeshi na sheria na mahakimu hata peponi yapo. Na ndiyo maana watu wanahubiriwa habari za hukumu na zile za jeshi la malaika na kifungo cha miaka 1000. Lakini sheria za mwanadamu wa tabaka la juu si kama zile za Mwenyezi Mungu.
Jambo la kujiuliza ni kwamba, katika sheria za nchi yako, ni ngapi ambazo ni za Mungu wa Musa na ngapi ni za Mungu wa Hammurabi? Unaweza kutafuta katika mtandao "Hammurabi's Codes of Law" kisha ukazilinganisha na zile amri za Mungu na hizo za taifa lako, hapo unaweza kujua pale kiongozi anapotangaza ya kwamba yeye katumwa na Mungu, utaweza kujua ni Mungu yupi anamzungumzia.