Rahma Salum
Member
- Sep 7, 2020
- 30
- 59
Aliyewahi kuwa Kapteni wa timu ya Taifa India na mchezaji mashuhuri na mwenye rekodi nyingi zaidi wa kriketi kuwahi kutokea nchini humo Sachin Tendulkar amesema, leo machi 27, 2021 amepima virusi vya korona na kugundulika kuwa navyo.
Akieleza hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Sachin amesema amekuwa akifanya vipimo na kuchukua tahadhari mara zote kuhakikisha korona inakaa pembeni, hata hivyo amegundulika kuwa na virusi hivyo leo kufuatia dalili alizokuwa nazo.
Ameongeza kuwa hakuna mtu mwingine kwenye familia yake aliyegundulika na virusi hivyo zaidi yake na kwa sasa atajiweka katika karantini na kufuata taratibu zote na ushauri wa madaktari.
Sachin mwenye umri wa miaka 48 alistaafu rasmi mwaka 2013 akiwa na rekodi ya Kimataifa ya kufunga mabao 100 alimaarufu kama karne/century katika miaka 24 ya kazi yake. Sachin alipewa jina na "mungu wa kriketi" nchini humo baada ya kuwa na rekodi nyingi zaidi kuwahi kutokea katika mchezo wa kriketi.