Baada ya kupata nafasi na kuipitia tena stori yako, naona hapo tatizo ni tamaa yako. Mwache baba afaidi. Wacha na hao wanawe wengine wafaidi. Mama hajaja na mali yake hapa duniani na anaondoka yeye tu, hivyo-hivyo kwako wewe, kwa baba yako, kwangu mimi na mwingine yeyote yule.
Kama umewahi kuona raha kupokea, basi jaribu kutoa, si kutoa nauli, si kutoa kilo ya sukari, kutoa kitu ambacho unakipenda kama vile nusu ya mali yako, ukampe mwenye kuihitaji, raha yake haina mfano.
Wacha ubahili na roho mbaya, umetoka kwa udongo utarudi kwa udondo, Hizi mali zipo na zitaendelea kuwepo milele na milele. Wewe Jee?