Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Muonekano mpya wa simu ya Google Pixel 6a umetoka, na inaonekana Google imeamua kuweka design mpya kama Google Pixel 6. Itakuwa ni style moja katika simu zake zote.
Simu hii mpya ya gharama ya wastani (mid-ranger), itakuwa na design mpya, kamera zitakuwa katika style ya mstari mmoja (style ya Visor); na itakuwa na kamera mbili na LED Flash. Pixel 5a ilikuwa na kamera upande wa kushoto.
Upande wa mbele, kamera ya selfie Pixel 6a itakuwa katika style ya hole-puch katikati ya kioo, tofauti na Pixel 5a ambayo ilikuwa na kamera ya selfie upande wa kushoto.
Another sad news kwa watumiaji wa Headphones ambazo sio Wireless: haitakuwa na sehemu ya kuchomeka pin ya Headphones kama ilivyo katika Pixel 5a.