mwaki pesile
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 340
- 487
Muongo (decade of action )wa hatua za kuimarisha usalama barabarani wa 2021-2030.
Utangulizi
Leo tunawaletea makala kuhusu Mpango wa Utekelezaji (Global Plan of Action) wa Mkakati wa miaka 10 wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na vifo na majeruhi kutokana na ajali ambao unajulikana kama Muongo wa Hatua za Kuimarisha Usalama Barabarani wa mwaka 2021-2030 au kwa Kiingereza Decade of Action for Road Safety 2021-2030.
RSA Tanzania kama mdau mkubwa wa usalama barabarani inaungana na Umoja wa Mashirika yasiyo ya kiserikali duniani kushawishi Serikali kupokea na kuchukua hatua za makusudi kutekeleza Mkakati huo kwa kuwa na Mpango Mkakati wa Nchi wa Kupunguza ajali na hivyo kuunga mkono juhudi za kimataifa za kuzuia ajali. Mpango Mkakati huo wa kidunia Utazinduliwa rasmi tarehe 28.10.2021, lakini nchi mbalimbali zinaweza kuendelea na uzinduzi wake hadi tarehe 03.12.2021.
RSA Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine tunategemea kukabidhi kwa serikali nyaraka za mpango huo wakati wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani. Lakini kuelekea tarehe 28.10.2021 tunataka kuwapa elimu kidogo kuhusu mpango huo kama ifuatavyo.
Kuhusu Mpango wa Kidunia wa Utekelezaji wa Muongo.
Mwaka 2021-2030 ni Muongo wa Kuchukua Hatua zaidi Kuimarisha Usalama barabarani. Mwezi Septemba 2020, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio Nambari A/RES/74/299 “Kuimarisha Usalama Barabarani Ulimwenguni”, na Kutangaza Hatua za kimuongo za Kuimarisha Usalama Barabarani, kwa malengo yenye shauku ya Kupunguza Vifo na Majeruhi kwa walau Asilimia Hamsini (50%) kufikia mwishoni mwa mwaka 2030. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na Kamisheni za Kikanda za Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na washirika wengine kwenye Ubia wa Usalama Barabarani kwenye Umoja wa Mataifa (UN Road Safety Collaboration), wametengeneza Mpango wa Kidunia wa Utekelezaji wa Muongo unaozinduliwa tarehe 28.10.2021.
Mpango huo unafungamana na Tamko la Stockholm la Mkutano wa Mawaziri wa Usalama Barabarani lililotolewa Februari 2020, kwa kusisitiza yafuatayo:
1. Umuhimu wa kuwa na Mtazamo wa Jumla kwa Usalama barabarani (Hollistic Approach to Road Safety)
2. Kutoa mwito wa kuendelea kuboresha ubunifu wa barabara na magari;
3. Kuboresha sheria na usimamizi wake;
4. Utoaji wa huduma za dharura kuokoa maisha ya waliojeruhiwa na ajali
Mpango huu pia una akisi Tamko la Stockholm wa kuhamasisha sera zenye kuhimiza Kutembea kwa Miguu, Usafiri wa Baiskeli, na Kutumia Usafiri wa Umma kama usafiri wa asili wenye kulinda afya na mazingira.
Mojawapo ya mafanikio ya Muongo UliopitMa
Mafanikio yaliyopatikana kwenye Muongo uliopita wa Hatua za Kuimarisha Usalama Barabarani (Decade of Action for Road Safety) wa 2011-2020 yameweka msingi wa kuendeleza mafanikio kwa miaka ijayo. Mojawapo ya mafanikio hayo ni:
1. Kuingizwa kwa usalama barabarani kwenye Agenda ya kidunia ya Afya na Maendeleo;
2. Kusambaza kwa upana miongozo ya kisayansi ya Mambo yanayoweza Kufanyika kwa Ufanisi Kuimarisha Usalama Barabarani;
3. Kukuza ubia na mtandao wa wabia wa usalama barabarani;
4. Uhamasishaji wa rasilmali za kufadhili shughuli za usalama barabarani.
Muongo huu mpya unatoa fursa ya kuendeleza mafanikio na mafunzo ya miaka iliyopita na kwa kuzingatia hayo kuokoa maisha zaidi.
Maeneo Yanayoangaziwa na Mpango huu
Mpango wa kidunia unaelezea nini kinapaswa kufanywa ili kufikia malengo, na unatoa mwito kwa nchi na wabia kutekeleza Mtazamo Jumuishi wa Mfumo Salama wa Usalama Barabarani (Integrated Safe System Approach). Hii inahusisha:
1. Kuwepo kwa usafiri wa aina tofauti tofauti na mipango ya matumizi bora ya ardhi(Multimodal transport and land use planning);
2. Miundo mbinu salama ya barabara(Safe road infrastructure);
3. Magari salama(safe vehicles);
4. Matumizi salama ya barabara(safe road use);
5. Huduma za dharura baada ya ajali (post crash response).
Yanayopaswa Kufanyika ili kufikia malengo.
Ili kufikia malengo ya Mpango huu, lazima tujikite katika:
1. Kuboresha sheria na kutekeleza kikamilifu
2. Kudhibiti mwendokasi
3. Kutenga fedha zaidi kwaajili ya usalama barabarani
4. Kujenga uwezo wa watendaji, sekta binafsi, mashirika ya kiraia, na taasisi za tafiti
5. Kuzingatia masuala ya kijinsia katika mipango ya usafirishaji.
6. Kutumia teknolojia mbalimbali katika kuimarisha usalama barabarani
7. Kuzisaidia zaidi kimsaada nchi zenye uchumi wa chini na zenye uchumi wa kati
8.Uwajibikaji wa pamoja wa usalama barabarani.
Ni matumaini yangu makala hii imesaidia kukufungua macho kuhusu Global Plan of Action for Road Safety
RSAadmin1
RSA Tanzania
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote