Muongozo kuhusu muundo, utaratibu wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba

Muongozo kuhusu muundo, utaratibu wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba

Wilawela

Member
Joined
Nov 16, 2011
Posts
92
Reaction score
32
Tume ya mabadiliko ya katiba inawaomba wananchi wote kupitia mwongozo huu uliotolewa na Tume na kuwasilisha maoni/Mapendekezo yao katika kipindi cha wiki mbili (2) baada ya tarehe ya kutolewa tangazo hili(14 Februari 2013).Maoni hayo yawasilishwe Tume

kupitia : Makao Makuu

Mtaa wa Ohio,S.L.P 1681,
DAR ES SALAAM
Simu:+25522 2133425
Nukushi(Faksi):+255 22 2133442
Tovuti:Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Au

Ofisi Ndogo
Jengo la Ofisi ya Mfuko wa Barabara,
Mtaa wa Kikwajuni Gofu
S.L.P 2775
ZANZIBAR
Simu: +255 224 3220768
Nukushi: +255 224 2230769
Jaji Joseph S. Warioba
Mwenyekiti

My take;

1.Wadau tunaendelea na Mabadiliko ya Katiba Tanzania Kama ilivyotolewa na tume ya Mabadiliko ya Katiba. Shime Watanzania naomba tuwe ni sehemu ya kuleta mabadiliko chanya ya katiba ya nchi yetu. Naomba watanzania wenzangu tutumie fursa hizi na kuacha tabia ya kulalamikia pembeni. Wasiwasi wangu ni wajumbe Kuchaguliwa na Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kata(WDC) Ambao wajumbe wake ni:
1.Mheshimiwa Diwani wa Kata- Mwenyekiti
2,Mtendaji wa Kata(WEO)- Katibu
3.Madiwani wa Viti Maalum wanaoishi kwenye Kata Hiyo:
4. Wenyeviti wote wa Mitaa/vijiji ndani ya Kata Hiyo

Kuhusu kuchaguliwa Mtaani sawa lakini kwenye WDC kuna Tatizo Naomba Tupendekeze WDC ianadae mkutano tu na wananchi/wakazi wote wa Kata wawapigie kura wawakilishi wao wanne(4) ili wawe wawakilishi wa Kata na si wa WDC!


2.Sifa za Kuomba Ujembe wa Baraza ni hizi hapa chini sote tuombe:
.4.1. Awe Raia wa Tanzania.
4.2. Awe na umri wa miaka 18 au zaidi.
4.3. Awe na uwezo wa kusoma na kuandika.
4.4. Awe mkazi wa kudumu wa Kijiji/ Mtaa / Shehia husika.
4.5. Awe Mtu mwenye hekima, busara na uadilifu.
4.6. Awe Mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo

3.Utaratibu wa Kuomba:Huu hapa chini tuutumie:

6.1.1. Kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0, kila
Mwananchi wa Kijiji / Mtaa husika anayependa kuwa mjumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa atawasilisha jina lake kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa. Uwasilishaji huo uambatane na taarifa zifuatazo:

6.1.1.1. Majina kamili ya mwombaji.
6.1.1.2. Jinsi yake.
6.1.1.3. Umri wake.
6.1.1.4. Elimu yake.
6.1.1.5. Kazi yake.
6.1.1.6. Sehemu anayoishi katika Kijiji / Mtaa husika.
6.1.2. Orodha ya majina ya Wananchi wote wanaotaka kuwa Wajumbe yatabandikwa kwenye maeneo ya wazi / matangazo ya kila Ofisi za Kijiji / Mtaa siku saba (7) kabla ya Mkutano ili wananchi wapate fursa ya kuyapitia na kujiridhisha kama walioomba wana sifa zilizoanishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0.


Aidha Mwongozo umeambatanishwa kwa rejea na unapatikana kwenye tovuti ya tume.
 

Attachments

Mkuu Wilawela,
Unatoa Tangazo kama mjumbe wa Tume vile! Umeeleweka mkuu, ubarikiwe!
 
Last edited by a moderator:
madiwani(ambao wengi ni ccm) watakuwa ni wajumbe wa mabaraza ya katiba!hapa tumeingizwa choo cha kike!
 
Mkuu Buchanan! Mimi si Mjumbe wa tume ni mpiga zumari(Whistle Blower) tu na Mtakia mema nchi. Nimeliona kwenye Webu ya Tume na Gazeti la Raia mwema Toleo Na.281 la 6-12 Februari 2013. Nina wasiwasi na muda 14 Februari 2014 ni Alhamisi ijayo tuu Tufanyeni halahala!
Mkuu Wilawela,
Unatoa Tangazo kama mjumbe wa Tume vile! Umeeleweka mkuu, ubarikiwe!
 
madiwani(ambao wengi ni ccm) watakuwa ni wajumbe wa mabaraza ya katiba!hapa tumeingizwa choo cha kike!

Mkuu meningitis;
Kwa Mujibu wa Mwongozo Mikoa yote Bara ispokuwa Dsm watachagua wajumbe wanne na Dar wajumbe wanane (8) Wakati kila kata inawakilishwa na diwani mmoja tu! Hivyo tukichangamkia nafasi tutawazidi madiwani zaidi ya mara 4 na mara nane kwa mikoa ya bara na dar! Naomba tusilalamike tutumie fursa hizi kuomba nafasi hizo!

Pia kama hii haifai toa maoni mbadala.
Naambatanisha Sections za Mwongozo kwa Rejea.

6.2.5. Utaratibu wa kupiga kura za kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa
kuwachagua Wananchi wanane wanaopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya utakuwa kama ifuatavyo:
6.2.5.1. Kwanza, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa watapiga kura ya siri ya kuwachagua Watu Wazima Wawili [wanaweza kuwa Wanawake au Wanaume].
6.2.5.2. Pili, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa watapiga kura ya siri kuwachagua Wanawake wawili.
6.2.5.3. Tatu, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa watapiga kura ya siri kuwachagua Vijana wawili
[wanaweza kuwa Wanaume au Wanawake].
6.2.5.4. Nne, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa watapiga kura za siri kuwachagua Watu wengine wowote wawili.


6.1.8. Afisa Mtendaji wa Kata baada ya kupokea majina yaliyopendekezwa kutoka kwenye Mikutano Mikuu Maalum ya Vijiji / Mitaa ya Kata husika, ataitisha Kikao Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata, ambacho kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0 kitachagua majina manne kwa kura ya siri kwa utaratibu ufuatao:
6.1.8.1. Kwanza, Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapigia kura ya siri ya kumchagua Mtu mzima mmoja [anaweza kuwa mwanamke au mwanaume].
6.1.8.2. Pili, Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kumchagua Mwanamke mmoja.
6.1.8.3. Tatu, Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kumchagua Kijana mmoja [anaweza kuwa Mwanaume au Mwanamke].
6.1.8.4. Nne, Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kumchagua Mtu mwingine yeyote.
 
Hizi mambo za uchaguzi wa hao wajumbe wa kata zitafanyika lini? Kuna kugombea? Nataka nirudi kata ya kwetu maana huko wananifahamu kama njaa.
 
Hizi mambo za uchaguzi wa hao wajumbe wa kata zitafanyika lini? Kuna kugombea? Nataka nirudi kata ya kwetu maana huko wananifahamu kama njaa.

Mkuu Nyalotsi Heshima Kwako! Kuna Uchaguzi utakaofanyika by June 2013 ambao utazingatia Kanuni zifuatazo hapa chini!

4.0. SIFA ZA WATAKAOCHAGULIWA KUWA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA NGAZI YA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA.

Wajumbe wanne kutoka kila Kata kwa Tanzania Bara na wanane kutoka kila Kata katika Mkoa wa Dar es Salaam na Wajumbe watatu kutoka kila Shehia kwa Zanzibar wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

4.1. Awe Raia wa Tanzania.
4.2. Awe na umri wa miaka 18 au zaidi.
4.3. Awe na uwezo wa kusoma na kuandika.
4.4. Awe mkazi wa kudumu wa Kijiji/ Mtaa / Shehia husika.
4.5. Awe Mtu mwenye hekima, busara na uadilifu.
4.6. Awe Mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kupambanua mambo.


5.0. MAMBO YA KUZINGATIWA
Utaratibu wa kuwapata Wajumbe kwa Tanzania Bara na Zanzibar uzingatie mambo yafuatayo:-

5.1. Uwakilishi wa watu wazima.
5.2. Uwakilishi wa wanawake.
5.3. Uwakilishi wa vijana.
5.4. Jiografia ya Kata/ Wadi / Kijiji / Mtaa / Shehia husika.


6.0. UTARATIBU WA KUWAPATA WAJUMBE KWENYE MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA NGAZI YA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

6.1. Kwa upande wa Tanzania Bara utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:
Kwa Mikoa yote isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam.

6.1.1. Kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0, kila Mwananchi wa Kijiji / Mtaa husika anayependa kuwa mjumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa atawasilisha jina lake kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa. Uwasilishaji huo uambatane na taarifa zifuatazo:

6.1.1.1. Majina kamili ya mwombaji.
6.1.1.2. Jinsi yake.
6.1.1.3. Umri wake.
6.1.1.4. Elimu yake.
6.1.1.5. Kazi yake.
6.1.1.6. Sehemu anayoishi katika Kijiji / Mtaa husika.

6.1.2. Orodha ya majina ya Wananchi wote wanaotaka kuwa Wajumbe yatabandikwa kwenye maeneo ya wazi / matangazo ya kila Ofisi za Kijiji / Mtaa siku saba (7) kabla ya Mkutano ili wananchi wapate fursa ya kuyapitia na kujiridhisha kama walioomba wana sifa zilizoanishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0.
6.1.3. Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa ataitisha Mkutano Mkuu wa Kijiji / Mtaa ambao utakuwa na agenda moja tu ya kuwapendekeza kwa kuwapigia kura watu wanne ambao majina yao yatawasilishwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata. Mkutano huu utaendeshwa na Mwenyekiti wa Kijiji / Mtaa, ambapo Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa atakuwa Katibu wa Mkutano huo na ndiye atakayewasilisha majina ya wananchi wote walioomba kuingia kwenye Baraza la Katiba la Wilaya.

6.1.4. Kwa kuzingatia Sifa zilizoainishwa katika aya za 4.0. na 5.0, Mkutano Mkuu wa Kijiji / Mtaa utayapigia kura ya siri majina ya wananchi walioomba kuwa Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

6.1.5. Utaratibu wa kupiga kura za kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa kuwachagua Wananchi wanne wanaopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya utakuwa kama ifuatavyo:

6.1.5.1. Kwanza, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa watapiga kura ya siri ya kumchagua Mtu mzima mmoja [anaweza kuwa mwanamke au mwanaume].
6.1.5.2. Pili, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa watapiga kura ya siri kumchagua Mwanamke mmoja.
6.1.5.3. Tatu, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa watapiga kura ya siri kumchagua Kijana mmoja [anaweza kuwa Mwanaume au Mwanamke].
6.1.5.4. Nne, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji /Mtaa watapiga kura ya siri kumchagua Mtu mwingineyeyote.
6.1.6. Orodha ya majina ya wananchi wanne waliopigiwa kura nyingi za kupendekezwa kuwa Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, yatabandikwa kwenye maeneo ya wazi/ matangazo ya kila Ofisi ya Serikali ya Kijiji / Mtaa.
6.1.7. Majina ya watu wanne yatakayokuwa yamepata kura nyingi kuliko mengine yatawasilishwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji / Mtaa kwa Afisa Mtendaji wa Kata yakiwa yameambatanishwa na Muhtasari wa Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji / Mtaa uliosainiwa na Mwenyekiti wa Kijiji /Mtaa pamoja na orodha ya wananchi waliohudhuria.
6.1.8. Afisa Mtendaji wa Kata baada ya kupokea majina yaliyopendekezwa kutoka kwenye Mikutano Mikuu Maalum ya Vijiji / Mitaa ya Kata husika, ataitisha Kikao Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata,ambacho kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa kwenye aya za 4.0 na 5.0
kitachagua majina manne kwa kura ya siri kwa utaratibu ufuatao:
6.1.8.1. Kwanza, Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapigia kura ya siri ya kumchagua Mtu mzima mmoja [anaweza kuwa mwanamke au mwanaume].
6.1.8.2. Pili, Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kumchagua Mwanamke mmoja.
6.1.8.3. Tatu, Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kumchagua Kijana mmoja [anaweza kuwa Mwanaume au Mwanamke].
6.1.8.4. Nne, Wajumbe wote wa Kamati ya Maendeleo ya Kata watapiga kura ya siri kumchagua Mtu mwingine yeyote.
6.1.9. Jina la Mwananchi atakayekuwa amepata kura nyingi kutoka kila kundi
[Mtu mzima, Mwanamke, Kijana na Mtu mwingine] yatawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa yakiwa na Muhtasari uliosainiwa na Mwenyekiti na Katibu wa Kikao Maalum cha Kamati ya Maendeleo ya Kata kilichoyapigia kura majina hayo pamoja na orodha ya wajumbe waliohudhuria.
6.1.10. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sifa na utaratibu ulioainishwa kwenye aya ya 4.0 na 5.0, atawasilisha majina kwa Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa Uteuzi.
6.1.11. Endapo Diwani wa kata ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata hatakuwepo [Kwa sababu zozote ikiwa ni pamoja na kuwa safarini kwa kipindi ambacho Mabaraza ya Katiba yatafanyika, kuwa mgonjwa na kutoweza kutekeleza majukumu ya Udiwani, Kifo au sababu nyingine], utaratibu wa kawaida wa kumpata mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata
wakati diwani hayupo utatumika, ambapo Mwenyekiti wa Kijiji atakayependekezwa na Wajumbe wenzake wa Kamati ya Maendeleo ya Kata kuendesha Kikao hicho ndiye atawakilisha kata badala ya Diwani.
 
Asante sana mkuu wilawela. Ngoja nianze kujiandaa kwa ajili ya mchakato huo.
 
Asante sana mkuu wilawela. Ngoja nianze kujiandaa kwa ajili ya mchakato huo.
Poa mkuu Nyalotsi Pamoja sana.

Lakini ukipata fursa tusaidiane kupinga wajumbe kuchaguliwa na WDC, kata yote iitwe ,WDC ianadae mkutano tu na wananchi/wakazi wote wa Kata wawapigie kura wawakilishi wao wanne(4) ili wawe wawakilishi wa Kata na si wa WDC!
 
Wadau Just a reminder!
Mwisho wa kuboresha Mwongozo huu ni 14 Februari 2014,bado siku moja tu! Naomba kwa kusukumwa na uzalendo tuboreshee mwongozo huu siamini kama uko perfect!
 
Wadau Just a reminder!
Mwisho wa kuboresha Mwongozo huu ni 14 Februari 2014,bado siku moja tu! Naomba kwa kusukumwa na uzalendo tuboreshee mwongozo huu siamini kama uko perfect!
 
Wadau nilihamasisha maoni Nimetoa Kama ifuatavyo(We must live the talk).Nimetimiza wajibu wangu Kazi kwenu.

Mapendekezo ya Kuboresha Mwongozo wa Muundo ,Utaratibu wa Kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Uendeshaji wake

Tume ya Mabadiliko ya Katiba Katika Awamu ya Kwanza ilikuwa na kazi ya Kukusanya maoni kutoka kwa:

  1. Kila Mtanzani
  2. Kila Mhimili wa Dola na Taasisi zake
  3. Makundi maalum nk.
Katika awamu ya Pili Tume ya Mabadiliko inawajibu wa kuunda Mabaraza ya Katiba kwa ajili ya kupitia na kutoa maoni juu ya Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume.
Kutakuwa na Mabaraza katika Mamlaka 163 Bara na 13 Zanzibar za Serikali za Mitaa na kufanya Jumla ya Mabaraza 176 tu.

Kumbe jumla ya Wahusika (respondents) awamu ya kwanza ilikuwa zaidi ya milioni 45 wakati awamu ya pili Wahusika (respondents) ni Wahusika 176 tu.

Hoja:
Kama tume iliweza kuwaona na kuwafikia wananchi wote zaidi ya milioni 45 kwa nini ishindwe kuratibu Mabaraza 176 tu? WDC Haikuchaguliwa kwa ajili ya Kuchagua wajumbe wa Baraza wanaowakilisha Kata.

Hofu:

Watendaji/Wenyeviti wa Mitaa/Vijiji /Shehia na Madiwani Hawaaminiki kwenye Jamii. pia Jukumu kubwa kama la katiba kuliachia kwa Kamati za Maendeleo za Kata (WDC) ni Hujuma kwa Katiba mpya!
Kama ndivyo ni afadhali hata tume isingeundwa tukatumia mamlaka zilizopo (existing structures) kama baadhi walivyo toa hoja. Kamati ya Maendeleo ya Kata haikuchaguliwa kwa ajili ya Kuchagua wajumbe wa Katiba.

Pendekezo:
1. Tume Yenyewe Ijigawe na Kuratibu zoezi hili ili iwajibike kwa Mema na Mabaya yatakayojitokeza.
2. Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) Iaandae tu Mkutano (Kuwatangazia, kufanya maandalizi nk) wa wakazi wote wa kata ili wananchi wa kata wawachague wawakilishi wao wanne (4) wa baraza la Katiba.
3. Kuwe na sehemu ya Kutia sahihi Wananchi wote watakaowasilisha Maombi ya Kuwa wajumbe wa Baraza la Katiba la Kata ili kuepusha kukatwa majina kinyemela.
4. Majina yatakayopigiwa kura na Mkutano mkuu wa wananchi wa kata husika yabandikwe na wananchi wapewe fursa ya kuyahakiki majina hayo kabla.
5. Wananchi walio tuma maombi wapewe muda wa Kukata rufaa iwapo majina yao yatakuwa yamekatwa/kufutwa Kabla ya Mchakato kuendelea.
6. Wananchi Wawachague Mwenyekiti na katibu wa Mkutano mkuu wa Kata na awajibike kama ilivyo kwa Zanzibar(rejea 6.3.4 na 6.3.5-6.3.8)
7. Matokeo ya Uchaguzi yatolewe waziwazi papo hapo mara baada ya kupiga na kuhesabu kura.
8. Uchaguzi wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ufanyike siku moja kata zote ili kuepusha wakazi wa kata "A" kwenda kupiga kura leo Kata "B".

Muhimu:
Mapendekezo haya yataathiri: Fungu 6.1.8,6.2.8 Hii itakuwa kama Zanzibar ambapo Wananchi wenyewe wananachagua.
 
Najua nimechelewa sana, lakini nimeona si vibaya kujua nani anaweza kuwa mjumbe wa baraza la katiba! Je, mtumishi wa umma anaweza kuwa mjumbe wa baraza hili, provided sifa zingine anazo, na utaratibu umefuatwa? Maana naona kama tume haijaweka wazi hapo.
 
Back
Top Bottom