Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Leo mheshimiwa rais Samia amesikika akisema kuwa hataki kuona rufaa ya mtumishi wa umma ikiletwa kwake baada ya kuwa imeshaamuliwa na Tume ya utumishi wa umma.
Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, kwa mujibu wa sheria yeye ni mkuu wa utumishi wa umma na pia ni sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa Umma na pia ana dhamana na mamlaka ya kusikiliza rufaa za watumishi zilizotolewa rufaa na chombo cha utumishi wa umma.
Kwa mujibu wa muongozo wa mashauri ya watumishi wa mwaka 2011, unaorejea kifungu namba 25(1) cha sheria namba 8 ya mwaka 2002 ikisomwa sambamba na kanuni ya 60(1) ya utumishi wa umma ya mwaka 2003, Rais ndiye mamlaka ya rufaa kwa watumishi ambao mamlaka ya nidhamu ni katibu mkuu kiongozi, Pia kifungu 25(1)(d) cha sheria ya utumishi wa umma namba 8 ya mwaka 2002, Mtumishi au mamlaka za nidhamu zinayo haki ya kukata rufaa kwa rais juu ya maamuzi yaliyotolewa na tume, na maamuzi ya rais yatakuwa ya mwisho!
Tunamtaka mheshimiwa rais atawale kwa mujibu wa sheria, na aache kutoa kauli ama za kutotaka kuwajibika au zinazoweza kuchanganya mamlaka za maamuzi juu ya haki juu ya watumishi wa umma.
Mheshimiwa Rais lazima ajue kuwa suala la ajira za watu na haki zao za kazi ni suala very sensitive, siyo sahihi kutolea kauli za kuchanganya kwa sababu ni suala linalogusa rizki za watu.
Kama mheshimiwa rais hataki kujihusisha na masuala ya watumishi basi huu ni muda muafaa wa yeye kukubali kubadili katiba inayompa mamlaka ya kuwa mkuu wa utumishi wa umma. Ifahamike miongoni mwa mambo ambayo wananchi wanayalalamikia ni mamlaka makubwa ya rais, Sasa ni wakati muafaka kwa Rais Samia kutupa sisi wananchi katiba bora nzuri ili haya anayojaribu kuyakwepa basi yafanywe na taasisi nyingine kikatiba na kisheria badala ya kumtupia rais
Hapa chini ni sehemu ya muongozo wa utumishi wa umma wa mwaka 2011 unaohusu rufaa za watumishi wa umma!