Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Kuna kipindi nilipata tatizo kama lako, sema utofauti na wewe ilikuwa ni gaming laptop na tatizo lilikuwa ni adopter walinipa ya 65w badala ya 150w, cpu frequency ilikuwa haipandi zaidi ya 0.99 Ghz nilivypata adapter original mambo yakawa safi
Ngoja nijaribu hili la adopter kwanza maana natumia ya kichina
 
Chief nisaidie mashine hii inafaa kwa kucheza game.
je ni kwa budget ya sh gap inaweza uzwa
maana jamaa anaiuza kwa tsh 1200k.
 
Chief nisaidie mashine hii inafaa kwa kucheza game.
je ni kwa budget ya sh gap inaweza uzwa
maana jamaa anaiuza kwa tsh 1200k.View attachment 2257118
Achana nayo, kama budget inafika 1.2m nunua machine mpya gen ya 11, gpu ya ndani ya Gen 11 ni nzuri kuliko Geforce 940mx.

Na kama unaweza subiri gen ya 12 ziingie mtaani pentium 8505 ambayo utaipata kwa nusu ya hio bei ni nzuri kushinda hio machine kila idara.

Na i3 1215u itakua na nguvu kama mara 4 ya hio i5.

Kifupi mkuu kwa Hizi processor mpya za Intel na Amd hakuna haja ya kununua Laptop mtumba za zamani, end of an era.
 
hpa unazungumzia laptop ama desktop kwnye hyo gen 12??
 
hpa unazungumzia laptop ama desktop kwnye hyo gen 12??
Vyote laptop na desktop.

Pentium ya Generation ya 12 ya laptop ina nguvu kushinda i7 gen ya 10 zinazoishiwa na U.

I3 gen ya 12 ina nguvu kuliko i7 gen ya 11 kwenye laptop.

Kifupi 12th gen zikiingia sokoni kwa Wingi soko la used litapata shida sana,

Na hio pentium ina gpu kali equivalent ya Nvidia 230MX. Games za kawaida unacheza bila matatizo, na Bei za pentium unazijua laki 4 mpaka 7.
 
so hapa kipi kizuri zaidi kutafuta pentium ya gen 12 ama core i3 ya gen 12 kwa bajeti ya milion 1??
 
Habari zenu wakuu,kuna kitu sikielewi aisee naomba kueleweshwa wakuu
Hivi inawezekanaje i5 gen ya 6 au 5 ikawa na clockspeed kubwa kushinda i7 gen ya 8? Nimeambatanisha mfano wa picha hapo chini
 
Habari zenu wakuu,kuna kitu sikielewi aisee naomba kueleweshwa wakuu
Hivi inawezekanaje i5 gen ya 6 au 5 ikawa na clockspeed kubwa kushinda i7 gen ya 8? Nimeambatanisha mfano wa picha hapo chini
Kuna kitu kinaitwa base na Turbo clock speed.

Base ni clock ambayo uhakika Machine yako ita operate kwa power level zote.

Turbo machine ita operate inapohitajika ila ikiwa haihitajiki inarudi base.

Twende kwa mifano halisi
-i5 6300u base ni 2.4ghz na turbo ni 3ghz
-i7 8550u base ni 1.8ghz na turbo ni 4ghz

Lets say umefungua program nzito kama Adobe premier una render video, Basi i7 ita operate kwa 4ghz na i5 kwa 3ghz hio i7 itafanya kazi kwa ufanisi na itatumia umeme mwingi.

Then ukifungua program ndogo kama Vlc unacheki video hio i7 itakaa Clock ndogo kama hio 1.8ghz na i5 itakua around hio 2.4ghz hapa zitafanya kazi sawa na i7 itatumia umeme kidogo.

Processor za kisasa siku hizi zina scale vizuri sana, ukija Gen mpya kama ya 12 efficiecy core base ni 1.3ghz tu, na perfomance core turbo zinaenda hadi 4.8ghz.

Hii inasaidia kupata vyote viwili perfomance na ukaaji chaji.
 
Dah,bro umeeleza vizuri sana na nimekupata poa sana,Mungu akutunze mkuu,make hapa nilikuwa nataka kununua mashine ya video production ila hivyo vitu vikawa vinanichanganya sana
 
Dah,bro umeeleza vizuri sana na nimekupata poa sana,Mungu akutunze mkuu,make hapa nilikuwa nataka kununua mashine ya video production ila hivyo vitu vikawa vinanichanganya sana
Kwa video production hio i7 itakuwa nzuri, sababu ni Quad core na thread 8 pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…