Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Kwa hii ni kundi gani
Intel(R) Pentium(R) CPU N3540 @ 2.16GHz 2.16GHz

hizi ni processor mpya za braswell zenyewe hazina nguvu sana ila zinatumia umeme mdogo sana kama watts 7 hivi, hivyo kifaa chake kitakuwa kinakaa sana na charge.
 
hio ni before hata generation za i3,i5,i7 ni processor za zamani sana sema kipindi chake zilikuwa zina nguvu. hio ni equivalent na pentium za generation ya 4

Ntaiuza hiiii maana kwa kuchemka ni balaa
 
Kuna wataalamu wengine wanasema upo ujuzi wa kubadilisha Processor, kwa maana unaweza kutoa ndogo na kuweka kubwa kwenye Laptop au Desktop. Hili likoje.
 
Kuna wataalamu wengine wanasema upo ujuzi wa kubadilisha Processor, kwa maana unaweza kutoa ndogo na kuweka kubwa kwenye Laptop au Desktop. Hili likoje.

yap processor inabadilishwa
1.kwa desktop nafikiri zote zinabadilishika
2. kwa laptop inabidi ufungue halafu uangalie kama ipo socketed (inachomoka) kuna nyengine zinachomelewa humo humo huwa hazitoki.

kwa desktop unaangalia tu aina ya motherboard mfano motherboard inaitwa lga-1150 basi hii inakubali processor zote za haswell (4th generation) iwe ni pentium, i3, i5, i7, xeon nk zote zitakubali cha muhimu tu uwe na cooler (feni) ambalo litapulizia vizuri. mfano computer ilikua na processor ya pentium ambayo thermal design power (TDP) yake ni 54 watts na kafeni kadogo ukabadili ukaeka i7 ambayo TDP yake ni 88W basi kale kafeni hakatapuliza vizuri hii i5 na computer itapata moto sana itabidi ueke feni kubwa kubwa

kwa laptop kubadilisha sio tu unaangalia motherboard bali pia unatakiwa uangalie na TDP (sababu huwezi kubadilisha mafeni ya laptop ukaeka makubwa) kuna processor za aina mbili hapa ambazo unatakiwa uzijue
-zinazoishiwa na u mbele
-zinazoishiwa na m mbele

hizi zinazoishiwa na u mbele nyingi zina TDP ya 15w zinatumia umeme mdogo hivyo ukibadili processor yake itabidi utafute u mwenzake. mfano unabadili i3 4010u kwenda i7 4600u

zinazoishiwa na m mbele nyingi zina TDP ya 35-37w ambayo ni kubwa kwa laptop hivyo ukibadilisha processor yabidi utafute yenye m kwa mbele. mfano i3 4000m ibadili iwe i7 4600m.

si kazi ngumu sana ni rahisi sana,
 
Ntaiuza hiiii maana kwa kuchemka ni balaa

yah processor za zamani zilikuwa zinatumia umeme mwingi sana, ila sasa hivi hasa hizi mpya za broadwell/braswell zinatumia umeme mdogo kama simu tu
 
Sawa elimu tosha hii.
 
chief, samahani. hivi kuna uwezekano wa kubadili mashine yako kutoka grade moja kwenda nyingine? mfano unakuta mashine yako ni i3 then una upgrade to i5 na je vipi kama utabadili pamoja na ram kutoka 1g kwenda zaidi
 
Yap inawezekana kabisa
 
Mkuu Chief-Mkwawa, nina simu ya Zenfone 5 (ASUZ) Intel Atom Z2580, Dual core 2ghz. Unaweza kuilinganisha na processor gani ya snapdragon?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Chief-Mkwawa, nina simu ya Zenfone 5 (ASUZ) Intel Atom Z2580, Dual core 2ghz. Unaweza kuilinganisha na processor gani ya snapdragon?

Kama snapdragon 600 hv. Lakin intel yupo vizuri cpu tu na kwenye simu cpu tupu haina maana inatakiwa soc nzima iwe ya ukweli vitu kama gpu, bluetooth, modem za network, wifi nk
 
Last edited by a moderator:
Shukrani Mkuu.
Kama snapdragon 600 hv. Lakin intel yupo vizuri cpu tu na kwenye simu cpu tupu haina maana inatakiwa soc nzima iwe ya ukweli vitu kama gpu, bluetooth, modem za network, wifi nk
 
Kama snapdragon 600 hv. Lakin intel yupo vizuri cpu tu na kwenye simu cpu tupu haina maana inatakiwa soc nzima iwe ya ukweli vitu kama gpu, bluetooth, modem za network, wifi nk

Mkuu naomba unijulishe hii processor iko kundi gani na pia vipi inaweza stahimili game nzito(maana mi ni mpenzi wa gaming)

PROCESSOR : AMD A4 - 3300 APU with Radeon(tm) HD Graphics 1.9 Ghz

RAM : 4.00 GB (2.24 GB usable)

SYSTEM TYPE : 32-bit operating system, x64-based processor
 
kabla hatujaenda kuangalia hii processor unatakiwa ubadili windows kwenye hii machine eka 64bit windows ili uweze kutumia ram yako yote na perfomance itaongezeka.

kuhusu nguvu ya processor nikukatishe tu tamaa hii processor ni dhaifu, utaweza cheza game ndogo ndogo kama za mpira ila ukija games nzito itachemka. ila zipo games za zamani siku zote hivyo hutakosa games za kucheza
 
Ahsante mkuu VP huwa kuna uwezekano wa kubadili processor na kuweka ambayo iko more powerful? Kama inawezekana vp gharama zake zikoje?
 
Ahsante mkuu VP huwa kuna uwezekano wa kubadili processor na kuweka ambayo iko more powerful? Kama inawezekana vp gharama zake zikoje?

kwanza inavyoonekana cpu yako ni a4 3300m na sio 3300.

ipo kwenye kifaa gani hio cpu? laptop au desktop?

mara nyingi cpu za laptop kubadili inakuwa ngumu zipo zinazokubali na zipo zisizokubali
 
kwanza inavyoonekana cpu yako ni a4 3300m na sio 3300.

ipo kwenye kifaa gani hio cpu? laptop au desktop?

mara nyingi cpu za laptop kubadili inakuwa ngumu zipo zinazokubali na zipo zisizokubali

Hii ipo kwenye laptop mkuu .na nashukuru kwa elimu yako
 
kwanza inavyoonekana cpu yako ni a4 3300m na sio 3300.

ipo kwenye kifaa gani hio cpu? laptop au desktop?

mara nyingi cpu za laptop kubadili inakuwa ngumu zipo zinazokubali na zipo zisizokubali

Mkuu naomba unifahamishe unapoamua kununua RAM au processor ili uireplace ile ya mwanzo ,unanunua tu yeyote au kuna vitu vya kuzingatia? ukizingatia pia zina kuwa na muonekano na size tofautitofauti kdogo sasa je mafundi huwa wanazifix vipi katika kifaa chako?
 
njia rahisi zaidi ni kwenda website ya kifaa chako kilipotengenezewa halafu uangalie full specification ya hicho kifaa, hapo ndo utajua ni ram za aina gani na processor za aina gani unaweza badili.

ram za computer so far zipo kuanzia ddr1, ddr2, ddr3 na ddr4 hivyo kuna chance kubwa computer yako inatumia moja wapo kati ya hizo, lakini huishii hapo hizo ddr nazo zimegawanyika hasa kwa vifaa ambavo si desktop kama simu,tablet, laptop, mini desktop nk zenyewe viram vyake vinakuwa vidogo huwezi tu ukaweka ukubwa wa kawaida hivyo tunarudi pale pale juu itabidi ukaangalie specs za mashine yako

na processor nayo ni motherboard ndio itakayoamua unaweza kuweka processor gani, ili kuijua motherboard yako itabidi uangalie specs zake kwa manufacture, pia itabidi uifungue uangalie kama processor inatoka au imechomelewa, kama imechomelewa hakuna njia ya kui upgrade
 
vipi kuhusu bei kama ya processor za i5 na i7 kwa Dar zinakuwa ni kiasi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…