Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Hivi ukitumia laptop yenye core 2duo inakuwa na kasi au
 
Inategemea na unachokifanya
Unapendekeza laptop au desktop zipi ?
Nataka run hii software hapa chini kwajili ya rendering

Lumion recommends the following minimum requirements:

OS: Windows XP, Vista, 7, 8 (32- and 64-bit) and DirectX 9.0c or later
System memory: 3 GB
Graphics card: NVIDIA GeForce GTS 450 or ATI/AMD Radeon HD 4890, with at least 1 GB dedicated memory (not shared system memory)
 
Mbona hakuna cpu?
 
Mbona hakuna cpu?
Nimezitoa kwenye website kama zilivyo, anyway nimeambatanisha screenshot


Ebu pendekeza desktop ambazo naweza pata kwa budget ya 300K to 500K

Laptop zipi zitafaa kwa hii software
 
Nimezitoa kwenye website kama zilivyo, anyway nimeambatanisha screenshot
View attachment 1144707

Ebu pendekeza desktop ambazo naweza pata kwa budget ya 300K to 500K

Laptop zipi zitafaa kwa hii software
Mkuu hio software ni demanding Sana. Kwa hio budget huwezi kupata Kila kitu. Graphics minimum ni passmark 2000, in maana ukikosa kabisa ni GT 1030 chini ya Hapo haitarun na recommended ni passmark point 8000 Ina maana Hapo ni gtx 1060 maana hadi 1050ti Ina point 6000.

Kutoka kwa 8th gen desktop za 7th na 6th gen zimeshuka Sana Bei, nimenunua i5 6500 desktop kwa laki 4 tu na nimeziona za 7th gen kwa laki 5 (i5 7500)

Ushauri wangu Kama utapata ya 7th gen yenye ram 8GB ama zaidi nunua, ila Kama Zina 4GB ram nunua 6th gen, kwenye 6th gen utaweza tumia ram za DDR3 ama DDR4 (tegemea na motherboard), hizi ram za DDR3 zinapatikana kirahisi kwa Bei nafuu hapa Tanzania, hivyo itakuwa rahisi ku Upgrade.

Ukipata 6th gen kwa laki 4, utai upgrade taratibu, inakuwa na slot 4 za ram moja wanakuwekea na tatu uta upgrade mwenyewe taratibu.

Weakness za hizi desktop ni power supply Ndogo hivyo itakulimit Sana kwenye graphics, utaweza tumia Nvidia 750ti, 1030 ama amd rx 550.

Graphics itabidi uweke mwenyewe baadae.

Kuhusu laptop hadi 940mx/940m hazifiki passmark 2000 hivyo itaku cost kuanzia 1m hivi.

Laptop ya rahisi ambayo inakidhi baadhi ya vigezo ni Lenovo IdeaPad 330s yenye Ryzen 5 2500u na yenyewe inauzwa dola 400 huko ughaibuni. Mpaka ije huku inazidi milioni.
 
Pia mkuu Soma hapa kuhusu graphics hio Ndogo ipo limited kwenye majengo madogo tu, majengo makubwa Kama viwanja vya mipira ama miji inataka passmark 10k level za kina 1080 na Titan.
 
Ok mkuu shukrani kwa maelezo mazuri
 
Core i5 4210u na i3 5005u ipi ipo vzuri kwa cpu na Gpu?
 
Ina maana pia kulingana na generation. Mabadriko kwa upande wa Gpu ni makubwa kuliko CPU?
 
Ina maana pia kulingana na generation. Mabadriko kwa upande wa Gpu ni makubwa kuliko CPU?
Ndio mkuu na siku zote kwa same generation i3/i5/i7 zinakuwa na GPU moja. Hivyo GPU ya i3 5005u ni sawa na i5 5200u au i7 5500u, ndio maana unaona japo i3 inapitwa performance ila GPU ipo vizuri.
 
Ndio mkuu na siku zote kwa same generation i3/i5/i7 zinakuwa na GPU moja. Hivyo GPU ya i3 5005u ni sawa na i5 5200u au i7 5500u, ndio maana unaona japo i3 inapitwa performance ila GPU ipo vizuri.

Nimekupata Mzee
 
Chief naomba niangalzie hii Dell
Processor akeView attachment 1182874
Processor yake inaitwa core M mkuu, na Hapo ameandika generation ya Saba.

Ila M3 6Y30 Kama alivyoandika yeye Ni generation ya 6 na sio Saba. Ingekuwa gen ya 7 ingekuwa m3 7y30

Ila nimeicheki online hio model Ina 7th generation, hivyo kimoja wapo Hapo juu amekosea, Ni vyema kabla hujanunua ukahakiki mwenyewe specification Hawa Jamaa hawaaminiki.

Kuhusu laptop yenyewe sababu Ina core m Ina maana itakula umeme kidogo Sana, core m inakula umeme kidogo Kushinda hata taa ya kawaida ya nyumbani just 4W tu.

Hivyo Kama unataka laptop yenye umbo Dogo na inayokaa na chaji, hio Ni laptop sahihi.

Kama unataka laptop yenye nguvu na ya kucheza games na kufanya kazi nzito achana nayo, tafuta laptop ya 8th gen, gape la performance baina ya 8th na 7th gen Ni kubwa Sana.
 
Nmeona insta jamaa wanaziuza....ila bei za kule siziamini mana pc ina specs kubwa afu bei chee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…