MURANG'A: Auawa na Shangazi yake kwa kipigo kisa alikula mkate

MURANG'A: Auawa na Shangazi yake kwa kipigo kisa alikula mkate

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714


Mtoto mmoja amefariki huku mwengine akiuguza majeraha baada ya kupigwa na shangazi yao kwa kula mkate katika kijiji cha Kiganjo kaunti ya Murang'a nchini Kenya.

Kulingana na runinga ya NTV nchini Kenya, Mtoto huyo wa miaka mitatu alifariki kutokana na majeraha aliyopata kwenye kichwa huku ndugu yake wa miaka 5 akiwa amelazwa katika hospitali ya Nyeri.

Wawili hao wanadaiwa kupigwa na shangazi huyo ambaye amedaiwa kuwa ana matatizo ya akili

Majirani wanasema kuwa waliwasikia wavulana hao wakipiga kelele na kuelekea kuwaokoa kabla ya kuwapata wamelala ardhini wakiwa hawana fahamu.

Runinga hiyo inasema kuwa kulingana na mkazi mmoja wa eneo hilo wavulana hao walikuwa wameachwa nyumbani na bibi yao ili kukaa na shangazi yao.

Nilikuwa nimeenda kununua dawa ya mvulana mmoja kati yao baada ya ngozi yake kukumbwa na upele kabla ya kupata simu kutoka kwa mmoja wa jirani zangu akinielezea kilichotokea, alisema.

Kulingana na wakazi wa eneo hilo Shangazi huyo aliwapiga wavulana hao baada ya kula mkate ambao ulikuwa wake.
 
Nilikuwa nadhani kenya hamna waliowehuka! Dalili ya n jirani, may that innocent soul RIP, Sammuel999 say Amen.

Hili la akili timamu kwenye lugha tunaita "kivumishi" wanataka kuaema kichwa cha aunt akiko sawa wakati hapo inshu ni njaa iliyo pitiliza.

Du mkate? Ukute hao watoto wakula slice mbili tu.

Kenya kweli nchi ya manyang'au mkate wanakurudisha kwa muumba.
 
Nilikuwa nadhani kenya hamna waliowehuka! Dalili ya njaa kwa jirani, may that innocent soul RIP, Sammuel999 say Amen.

Hili la akili timamu kwenye lugha tunaita "kivumishi" wanataka kuaema kichwa cha aunt akiko sawa wakati hapo inshu ni njaa iliyo pitiliza.

Du mkate? Ukute hao watoto wakula slice mbili tu.

Kenya kweli nchi ya manyang'au mkate wanakurudisha kwa muumba.


Hii ni njaa au ukatili tu?

Hiyo njaa aisee, uchumi wao umeshikiliwa na watu wachache especially foreigners lakini wengi wao ni kapuku kwelikweli.hahaaa
 
Back
Top Bottom