- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Salaam Wakuu,
Jana kupitia mitandao ya kijamii kumezunguka nukuu mbalimbali za Mwenyekiti wa sasa wa Simba Sports Club Murtaza Mangungu.
Miongoni mwa nukuu iliyonipa mashaka na kutaka kujua ukweli wake ni ile inayosema Mangungu amesema Simba haiwezi kuvunja Mkataba na Jobe na nyingine kwamba yeye atatoa pesa za usajili.
Je kuna ukweli hapa?
Jana kupitia mitandao ya kijamii kumezunguka nukuu mbalimbali za Mwenyekiti wa sasa wa Simba Sports Club Murtaza Mangungu.
Miongoni mwa nukuu iliyonipa mashaka na kutaka kujua ukweli wake ni ile inayosema Mangungu amesema Simba haiwezi kuvunja Mkataba na Jobe na nyingine kwamba yeye atatoa pesa za usajili.
Je kuna ukweli hapa?
- Tunachokijua
- Murtaza Mangungu ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Simba Sports Club ya Tanzania. Jana Juni 12, 2024 katika anga la wapenda soka nchini kuliibuka hoja mbalimbali kumhusu Mwenyekiti huyu huku Wanachana wengi wa Klabu ya Simba wakishinikiza kiongozi huyo ajiuzulu. Shinikizo hili linatokana na Salim Abdallah Muhene (Try Again) kufanya uamuzi wa kujiuzulu.
Jana katika mitandao ya kijamii kumeenea taarifa mbalimbali zikimnukuu Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu akiongelea mambo mbalimbali kuhusu Simba. Miongoni mwa nukuu hizo, nukuu iliyohusu mustakabali wa mchezaji Par Omar Jobe (hii) na ile iliyodai Mangungu atatoa pesa ya usajili iligusa hisia za mashabiki wengi.
Upi ukweli kuhusu nukuu hizo?
JamiiCheck imefanya mawasiliano na Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu ambaye amekanusha kutamka kauli yoyote kuhusu Par Omar Jobe na pia kufanya usajili.
Mangungu ameifafanualia JamiiCheck kuwa siku ya Juni 12, 2024 alizungumza na taasisi mbili tu ambazo ni TBC na Clouds Media Group na sauti zote zipo bayana lakini hakutamka kauli hizo zilizonukuliwa toka kwenye ukurasa unaotumia jina la SportsArenaTz.
Akiifafanulia JamiiCheck kuhusu jambo hili Mangungu anasema:
Jambo hili ningesema mgesikia hata sauti. Mimi sijawahi kutoa kauli hiyo. Mimi nimezungumza na Taasisi mbili TBC juzi (Juni 11, 2024) na audio yangu ikisikika, baadhi ya vyombo wakaichukua na kusema wao ndiyo walikuwa wananihoji na wakaongezea maneno mengine ambayo Mimi sikusema na pia jana Clouds Media Group.Zaidi ya hayo, JamiiCheck imepitia ukurasa rasmi wa Instagram ya Meneja wa Habari wa Simba Ahmedy Ally ambaye naye ametoa taarifa maalumu kukanusha ujumbe uliobebwa na nukuu hizo.
Katika andiko lake Ahmedy anasema:
Hizi nukuu za Uongo, Hakuna mahala Mwenyekiti Murtaza Mangungu amezungumza maneno haya.Wana Simba tuwe makini na taarifa za mitandaoni zenye lengo la kuzua taharuki ndani ya klabu yetu na kutugombanisha baina yetuHivyo, kutokana na vyanzo hivinJamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa iliyobenwa na nukuu hizo kuhusu Murtaza Mangungu haina ukweli