Murtaza Mangungu, nakushauri mtafute Wakili Msomi Lloyd Nchunga akueleze aliondokaje Simba

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Njia wanazotumia wanasimba kukutaka ujiuzulu ni kelele za chura tu, pressure imekuwa kubwa kukufosi uachie uenyekiti kwa sababu umeshindwa kuleta furaha kwa wanasimba.

Halafu umewaongezea machungu sana pale ulipokuwa ukihojiwa na waandishi wachovu wa Mawingu kwani ulikuwa ukiongea na jeuri, ubishi, kujiamini kulikopitiliza.

Sikikiza Mangungu, wanasimba ndio walikuchagua uwaongoze, ulianza kushindana na Juma Nkamia na baadae Wakili Msomi Mosses Kaluwa ukamshinda kwa kile wanachokidai ni hila.

Sasa hao waliokuchagua wanakuona wewe hufai kwanini unang'ang'ania Bw.Mangungu.

We unapata nini hapo unapopang'ang'ania wakati unaowaongoza hawakutaki?

Utafanya kazi na nani sasa wakati wanachama wote hawakutaki, hawakutaki.

Mtafute Lloyd Nchunga Wakili Msomi ambaye alikuwa na michongo kama yako, akajifanya mjuaji siku tulipokutana na Yanga mzee Akilimali akatangaza kabisa kuwa simba hafungwi hiyo mechi na kweli tukaibamiza yanga mabao 5 kwa nunge.

Nchunga aliondoka kwa aibu Yanga, mambo aliyotendewa hadi akadiriki kujiuzulu hayakuwa mazuri.

Nchunga hana hamu hadi leo.Wewe unaposema huwezi kujiuzulu unawakosea heshima wanachama.Hao hao ndio walikuona wewe unafaa na ss hv wameona hapana, wajibika tu ili kuiokoa Simba.

Nikikumbuka ya Nchunga naona yale yale yanajirudia tena kwetu.Wape wengine waendeleze kijiti baba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…