Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MUSA KWIKIMA NA UJAJI WA MAHAKAMA KUU KWA MARA YA PILI 1983
Marehemu Musa Kwikima aliapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu baada ya kutolewa kwenye nafasi hiyo na Mwalimu Julius Nyerere mwaka wa 1969.
Jaji Mkuu Nyalali alimfuata Tabora kwa mazungumzo na Kikwima akarudishwa kuwa jaji mwaka 1983.
Mwalimu Nyerere akamuapisha Kwikima kwa mara ya pili siku moja na majaji wengine wawili Jaji D'Souza na Jaji Kapoor.
Kwikima alishika nafasi hii kwa miaka miwili tu kisha akajiuzulu kwa hiari yake mwenyewe. Mara ya kwanza Mwalimu Nyerere alimwapisha Kwikima siku moja na Majaji Lewis Makame na Robert Kisanga katika miaka ya mwishoni 1960s.
Musa Kwikima alirudishiwa ujaji ili kusaidia kesi za uhujumu uchumi.
PICHA: Musa Kwikima alipoamishwa na Julius Nyerere kuwa Jaji mara ya kwanza.
Sent using Jamii Forums mobile app