Museveni aamuru majangili wapigwe risasi

Museveni aamuru majangili wapigwe risasi

ng'wandu

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2011
Posts
333
Reaction score
105
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameriamuru jeshi la nchi hiyo (UPDF) pamoja na Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda (UWA) kuwapiga risasi jangili yeyote atakayeonekana katika mbuga za wanyama za nchi hiyo.

Rais Museveni anayeonekana kukerwa sana na tatizo la ujangili alitoa agizo hilo huko Kidepo wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini toka kuzinduliwa kwa mbuga hiyo ya wanyama. Ni hivi karibuni tu mbuga hiyo ilichaguliwa na CNN kama mbuga ya tatu Afrika kwa ubora kwa mwaka 2013.

"Inaonekana jeshi limelala. Inawezekana vipi mtu akashindwa kuheshimu nyumba ya mtu mwingine? Kama hao Watoposas na Waturkana wakija tena kuwasumbua wanyama wetu wapige risasi. Kama hamuwezi kuwapiga mimi mwenyewe nitakuja na kufanya hivyo" alikaririwa Museveni akisema.

"Yeyote atakayeingia hapa Uganda na bunduki ni lazima apigwe risasi", Museveni aliongeza.

Agizo hilo la rais Museveni limekuja wakati ambao kumekuwepo na malalamiko kutoka waziri wa nchi wa Karamoja kuwa ujangili bado ni tatizo kubwa linalozikumba mbuga za wanyama nchini humo ikiwemo Kidepo.

"Mheshimiwa rais hatujui tutafanyaje, Watoposa kutoka Sudan ya Kusini na Waturkana kutoka Kenya huingia nchini mwetu wakiwa na silaha, kasha huwasumbua raia wetu na kuendesha vitendo vya ujangili katika mbuza zetu za wanyama" alisema waziri huyo bwana Babra Nekasa Oudo.

Rais Museveni ana wasiwasi kuwa sekta ya utalii nchini humo, ambayo wmwaka jana iliingiza kiasi cha dola billion 1.3 kutokana na watalii million 1.5 waliofika Uganda, haiheshimiwi na majangili.

Museveni pia aliwataka wananchi wa Karamoja kujenga mahoteli zaidi na kukuza mimea ya chakula ili waweze kufaidika na sekta ya utalii inayokua kwa kasi nchini humo.

"Nchi ya Spain hupokea watalii wapatao million 50 kwa mwaka na hupata kiasi cha dola billion 23 kutoka kwenye sekta ya utalii lakini hawana vivutio vizuri kama tulivyonavyo hapa Uganda. Waganda wanapaswa wafungue macho na kuachana na ujangili", alisema rais Museveni.

MUSEVENI AAMURU MAJANGILI WAPIGWE RISASI
 
Vizuri hata mafisadi nao wapigwe risasi
 
Back
Top Bottom