Museveni aeleza kisa cha Katiba kurekebishwa

Museveni aeleza kisa cha Katiba kurekebishwa

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
pic+museven.jpg


Rais Yoweri Museveni amefichua siri kwamba uamuzi wa kurekebisha Ibara ya 102 (b) ya Katiba kwa dhati ulifanywa baada ya kuchokozwa na wanasiasa wa upinzani.

Museveni amesema chama cha National Resistance Movement (NRM) hakikuwa kinakerwa na kifungu cha Katiba kilichoweka ukomo wa umri wa rais kuwa kati ya miaka 35 na 75 hadi wanasiasa wa upinzani walipozindua kampeni yao waliyoiita Togyikwatako (yaani usiguse hiyo)

"Isitoshe, ni wapinzani waliochokonoa. Walisema kitu kile Togikwatako ... na tulisema aahh ... Togikwatako!" Museveni amekumbusha katikati ya shangwe za watu.

Ameongeza hivi: "Sasa wanafanya kazi ya kutishia vijana wapambanaji 317 katika jitihada za kubadili nchi yao, lakini hatutakubali hilo. Napenda kuwaambia, ninyi (wabunge 317) ni wanahistoria wapya," amesema.

Amesema hayo Jumapili alipokuwa wilayani Kiboga wakati wa sherehe za NRM kwa kufanikisha marekebisho ya Katiba.

Mwaka jana, wabunge wa NRM 317 walipiga kura ya kurekebisha Katiba ili kuondoa ukomo wa umri wa rais, kubadilisha muda wa viongozi wa Serikali za mitaa kutoka miaka mitano hadi saba na kurejesha ukomo wa mihula miwili

Hoja binafsi ya Mbunge wa Igara Magharibi, Raphael Magyezi ilivutia shangwe na lawama huku wabunge wa upinzani wakipinga kwa madai imefungua milango ya urais wa maisha.

Rais Museveni, ambaye atakuwa na umri zaidi ya miaka 75 kufikia uchaguzi mkuu ujao, sasa atakuwa huru kugombea uchaguzi huo.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom