Museveni akimbia mdahalo wa wagombea Urais Uganda

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ambaye anagombea kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa Januari 2026, hakujitokeza kushiriki mdahalo wa televisheni wa wagombea urais uliofanyika usiku wa kuamkia leo.

Kwenye mdahalo huo, wagombea watano pekee kati ya wanane ndio walihudhuria, akiwemo mpinzani mkuu wa Museveni, mwanamuziki aliyeingia kwenye siasa, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine.

Akinukuliwa katika mdahalo huo, Bobi Wine alisema alikuwa na matarajio ya kumkuta Rais Museveni akishiriki mdahalo huo ili “kusikia moja kwa moja kuhusu mafanikio anayodai kuyatetea.” Aliongeza kuwa, “Museveni hayupo hapa kwa sababu yuko zamani, wakati sisi tunajadili mustakabali wa Uganda.”

Kulingana na chama tawala cha NRM, Rais Museveni hakushiriki mdahalo huo kutokana na ratiba ngumu ya kampeni
Your browser is not able to display this video.



​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…