Museveni amfuta Waziri Mkuu kazi

Museveni amfuta Waziri Mkuu kazi

weed

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
2,459
Reaction score
3,576
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na mwandani wake Amama Mbabazi.

Kwenye taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa mchango wake kwa nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi wake Ruhakana Rugunda ambaye sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge.

Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao.

Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama waziri mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara moja.

Mbabzi alikuwa mwandani wa karibu wa Rais Museveni.
Waziri mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa angemrithi rais Museveni lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa huo uhusiano kati yake na Museveni haujakuwa mzuri.

Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.

Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mumewe ameonewa.

Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.
 
africa democracy bado sana infact east africa demokrasia ndio wa mwisho kabisa angalia tu nchi 3 za east afrika, kenya rais muuaji ana kesi the hague ya kugombea madaraka, uganda ndo ivo rais king'ang'anizi hataki kutoka madarakan miaka 28, rwanda hali kadhalika rais miaka 17 madarakan, burundi rais nae anabadili katiba aendeleee, tanzania chama toka enzi za uhuru mpaka leo hakijabadilishwa no wonder people of the this part of the world ndio maskini kabisa!!!
 
Sijui hapa kwetu KJ anasubiri nini maana wananchi wanaona kabisa Wapigwe anapwaya!
 
Huyu Rais wetu sijui kazubaa au ni nini. Badala ya kuchukua fursa ya katiba mpya kubadili aendelee kukalia kiti kwa muda atakaoona unafaa, yeye eti anadai anamwandalia Rais ajaye aikute nchi ni tajiri.

Badili katiba utajiri uanze nao wewe mwanzo mpaka mwisho. Kulima ulime wewe kula wale wengine si majanga hayo.
 
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemfuta kazi waziri mkuu na mwandani wake Amama Mbabazi.

Kwenye taarifa yake Museveni alimshukuru bwana Mbabazi kwa mchango wake kwa nchi ya Uganda ambapo pia alimtangaza mrithi wake Ruhakana Rugunda ambaye sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge.

Bwana Mbabazi alikuwa anatarajiwa na wengi kuwa mpinzani wa Museveni katika uchaguzi ujao.

Rais Museveni ametangaza kuwa amemteua daktari Ruhakaan Rugunda kama waziri mkuu mpya ambaye ataaanza kushikilia wadhifa wake mara moja.

Mbabzi alikuwa mwandani wa karibu wa Rais Museveni.
Waziri mkuu anayeondoka Amama Mbabazi alionekana kuwa angemrithi rais Museveni lakini miaka mitatu ambayo amehudumu katika wadhifa huo uhusiano kati yake na Museveni haujakuwa mzuri.

Mapema mwaka huu chama kinachotawala kiliidhinisha azimio kikisema kuwa rais Museveni ambaye amekuwa uongozini kwa muda wa miaka 28 atakuwa mgombea wa pekee kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.

Hata hivyo mkewe Mbabazi ambaye pia ni afisa wa cheo cha juu chamani amesema kuwa mumewe ameonewa.

Waziri mkuu mpya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya afya awali alikuwa amehudumu kama waziri wa afya.

Museveni kaanza kufyeja matawi yanayo mtia hofu katikak auchguzi ujao 2016 aendelee na UFALME WAKE!!!! kikuweli hawatemdei haki Waganda
 
Miaka 28 anatawala mtu mmoja tu?katika watu zaidi ya mimillion 37 hakuna wa kumridhi
 
Wakati Byesige anachapwa virungu na polisi wakina Amama Mbabazi walikuwa wanachekelea , sasa hivi kibao kimegeuka na siku si nyingi unaweza sikia Mbabazi ametiwa ndani!!
 
udikteta kwenye nchi za kiafrika sijui utaisha lini mtu mmoja toka mwaka 1986 yupo madarakani mpaka leo kwa kifupi wananchi wote wa uganda kawaona mafala kwamba hawawezi kuongoz mwenye akili Ni yeye Tu.
 
yale yale ya Rwanda. Jamaa wanapunguza competition taratibu, muda wa uchaguzi ukifika wanabaki wao tu!
 
udikteta kwenye nchi za kiafrika sijui utaisha lini mtu mmoja toka mwaka 1986 yupo madarakani mpaka leo kwa kifupi wananchi wote wa uganda kawaona mafala kwamba hawawezi kuongoz mwenye akili Ni yeye Tu.
Aya sisi mwalimu alikaa miaka 28 madarakani ila akaamua kuachia na kuwaachia jamaa zake wene itikadi zanazoendana na zake. Imefika wanatoa sasa na APA kwetu tuongozwe na skills zingine
 
Yaani ananibiloa m7
Hivi wauganda kweli wameridhika na hali hii?

Anataka yamkute km ya gadafi!

Hivi umoja wa nchi za Afrika huwa hawaongelei haya!!!!
 
Back
Top Bottom