Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametoa matamshi makali dhidi ya Rais Barack Obama wa Marekani akimtaka akome kungilia masuala ya ndani ya Uganda.
Matamshi hayo makali yamekuja baada ya Rais wa Marekani kutishia kuwa uhusiano wa nchi yake
na Uganda utaharibika iwapo Rais Museveni atasaini na kuufanya kuwa sheria muswada wa
kupinga vitendo vichafu vya kujamiiana watu wa jinsia moja.
Rais Museveni amesema, atashirikiana na Russia iwapo Marekani itaendelea kuingilia masuala ya
ndani ya Uganda na kuongeza kama ninavyomnukuu:
"Russia imekuwa ikifanya shughuli zake barani Afrika tangu mwaka 1917 yaani kwa zaidi ya miaka
100. Ninataka kushirikiana na Russia kwa sababu hawachanganyi siasa zao na siasa za nchi
nyingine." Mwisho wa kunukuu.
Ameongeza kuwa: "Ukiona mtu anaingia ndani ya nyumba ya mtu mwingine basi jua kuna tatizo.
Hapa ni nyumbani petu. Huwezi kumuona mtu mwenye upaa kama mimi hivi ndani ya nyumba yake
na kuanza kumpangia afanye unavyotaka wewe. Rudi kwenu!" Mwisho wa kunukuu.
CHANZO.http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/38388-museveni-amtolea-uvivu-obama,-amwambia-akome
Rais Museveni Amkomalia kichwa Rais Obama Kasheshe kweli jamani.
