Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Kweli ivumayo haidumu. Hakuna kiumbe alikuwa akikera kwa kujikomba kwa mwendazake kama huyu jamaa aitwaye Cyprian Musiba Rugarabamu wa Rugaimukamu. Sasa yupo hoi ndembe ndembe akikabiliwa na tishio la kufilisiwa uchache wote aliokuwa akipewa kuwakashfu wapinzani wa mwendazake.
Kama kuna sehemu inamfaa Musiba si pengine bali kaburini tena karibu na mwendazake. Musiba sasa ni msiba si chochote si lolote. Uanaharakati huru usio huru bali udhuru uliyeyuka kilipotangazwa kifo cha mwendazake.
Hata hivyo, hapa kuna somo. Magu alikuwa akitumia mapandikizi kuwaumiza wabaya wake asijue kila kitu kina mwisho. Musiba, Makonda na manyang'au wengine sasa wanalia na kusaga meno. Hili ni somo kuwa hata walioko kwenye madaraka sasa wajue yana mwisho.
Nani alidhani watu kama Msiba, Dk Bushiri Ali aliyekuwa akigawiwa vyeo kila uchao, Hamfulei Polopolo, Daud Bashite na washenxxzi wengine waliokuwa wanajidai kana kwamba kaya ilikuwa yao. Ama kweli aliyeko juu mngojeni chini. Nani alijua kuwa Bashite aliyeweza kuvamia hata studio na kufukuzisha mawaziri angekuwa sasa anaficha jiuso lake kwa aibu kama sengxxe?