Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Katika mahojiano aliyofanya siku tano zilizopita Musiba alisema kuna vikundi ambavyo angependa kuishauri serikali ya Tanzania kwa jicho la tatu, kwani si wema na wameanza harakati za kuchafua na kuharibu taswira ya nchi yetu, ambapo kuna makachero wanaoshirikiana nao ili kukamilisha adhma yao.
Musiba amemtaja Jefrey Smith akishirikiana na Robert wakati uliopita akisema anaona sasa wamerudi tena, wanajiunga tena kwa kushirikiana na wakimbizi wa Tanzania akiwataja Kabendera, Sarungi na wengine, akishauri serikali iwalete nchini.
Musiba akauliza swali, kama ingekuwa Uganda, Rwanda, Urusi au Marekani wangeachwa? Kamtetea Kimambi, anasema sasa hivi amebadilika na kuwa mtu mwema!
Ni kwasababu sasa hivi amewakalia koo CCM?
Kwahiyo hapa Musiba ni kama amesema wote aliyowataja warestishwe in peace?!
Katika mahojiano aliyofanya siku tano zilizopita Musiba alisema kuna vikundi ambavyo angependa kuishauri serikali ya Tanzania kwa jicho la tatu, kwani si wema na wameanza harakati za kuchafua na kuharibu taswira ya nchi yetu, ambapo kuna makachero wanaoshirikiana nao ili kukamilisha adhma yao.
Musiba amemtaja Jefrey Smith akishirikiana na Robert wakati uliopita akisema anaona sasa wamerudi tena, wanajiunga tena kwa kushirikiana na wakimbizi wa Tanzania akiwataja Kabendera, Sarungi na wengine, akishauri serikali iwalete nchini.
Musiba akauliza swali, kama ingekuwa Uganda, Rwanda, Urusi au Marekani wangeachwa? Kamtetea Kimambi, anasema sasa hivi amebadilika na kuwa mtu mwema!
Ni kwasababu sasa hivi amewakalia koo CCM?Kwahiyo hapa Musiba ni kama amesema wote aliyowataja warestishwe in peace?!