Music production studios - test mpya ya muziki

Superman

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2007
Posts
5,693
Reaction score
1,702
Tumefungua Music Studio ya Kisasa.

Kama una kipaji cha kutunga na kuimba nyimbo na unadhamira ya kufanya kazi nzuri sana basi unakaribishwa.

Interest yetu ni kutengeneza Muziki utakaopendwa na watu wa rika zote watoto, wazee na vijana na kudumu kwa miaka mingi. Muziki unaokusudiwa utakuwa katika kiwango cha juu na pia utaibua vipaji vipya. Yupo Producer ambaye ni kijana mdogo na anayeijua kazi vyema.

Tupo Tancot House; Sokoine Drive/Pamba Road; Ground Floor; City Centre; Opposite Luther/Life House.

Mawasiliano yote yapitie barua pepe:
jasonsltd@gmail.com
 
big up sana wakuu, napenda na najua music sema npo arusha, all the best.
 

Interest yetu ni kutengeneza Muziki utakaopendwa na watu wa rika zote watoto, wazee na vijana na kudumu kwa miaka mingi. Muziki unaokusudiwa utakuwa katika kiwango cha juu na pia utaibua vipaji vipya.

Mkuu is that possible ?, mi nilidhani hizo category zina interest tofauti:-

Wazee wanapenda miziki ya kuwakumbusha enzi zao
Vijana wanakwenda na wakati (whats hot now)
Watoto (well watoto wanapenda vitu rahisi rahisi na laini laini)..

Sasa mkuu kujaribu ku-intermix hizo different taste huoni kwamba unaweza uka-compromise na kutoka na kitu ambacho hakuna anayekipenda ?

Mi naona ni bora kugawa market zako katika different segments (market segmentation) vijana, wazee na watoto na kuwalenga wateja wako kwa kile wanachotaka kwa kutoa product catered for every category
 

Mkuu, kwa ubunifu inawezekana kabisa. Mfano angalia kuna baadhi ya nyimbo za miaka mingi zinapendwa na wengi wa kila rika hadi leo mfano za akina Jim Reeves; "Rangi ya Chungwa"; "Vundela"; "Umkombochi" nk nk. Inaweza ikawa si katika maana hiyo strictly lakini inawezekana ku-improve.

yapo malalamiko kuwa Bongo Fleva imepoteza mwelekeo. Nyimbo nyingi zinafanana, beats wanaibiana; zinachuja haraka; mashairi yanafanana. styles, dressing nk nk.

Tunaangalia namna ya kuleta tofauti.
 
Bro Superman kina jamaa hapa mtaani kwetu ana kipaji cha kutunga na kuimba. Ila bahati mbaya hana hela za kuingia studio. Je unaweza kumsaidiaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…