Musoma: Afungwa miaka 30 jela kwa kumbaka mlemavu

Musoma: Afungwa miaka 30 jela kwa kumbaka mlemavu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma Mkoa wa Mara imemhukumu kwenda jela miaka 30, mkazi wa Kijiji cha Kibubwa Wilaya ya Butiama, Juma Ligamba (40) baada ya kupatikana na kosa la kubaka kinyume cha sheria.

Mahakama hiyo imemtia hatiani, Ligamba baada ya kuthibitika kuwa alimbaka binti mwenye umri wa miaka 19 ambaye pia ni mlemavu wa akili na viungo (aliyepooza).

Akitoa hukumu hiyo mahakamani hapo leo, Jumatano Novemba 9, 2022 hakimu mkazi mwadamizî wa mahakama hiyo, Stanley Mwakihaba amesema kuwa mahakama hiyo imejiridhisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo na hivyo anastahili kutumikia kifungo hchò kwa mujibu wa sheria.

Mwakihaba amesema kuwa Ligamba ametiwa hatiani kupitia kifungu cha 130 (2) (c) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

"Ķutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa ni dhahiri kuwa mshtakiwa alitenda kosa hili tena mbaya zaidi kwa mtu ambaye ana matatizo ya ulemavu wa viungo na akili, mahakama hii inakuhukumu kutumikia miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda vitendo vya kikatili kama hivi," amesema Mwakihaba.

Hata hivyo mshatikiwa huyo alipotakiwa kujitetea kabla ya kutolewa kwa hukumu katika kesi hiyo namba 91 ya mwaka 2022, amesema kuwa hana cha kusema hivyo kuiachia mahakama kutoa hukumu kadri itakavyoona inafaa.

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Monica Hokororo pamoja na Mwendesha Mashtaka na Mkaguzi wa Polisi, Denis Bigambo ambao kwa pamoja waliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali hasa ikizingatiwa kuwa pamoja na kuwa mshtakiwa amebainika kubaka lakini pia kitendo hicho alimfanyia mtu ambaye hakuwa na uwezo wa kujitetea kutokana na ulemavu alio nao.

Akitoa maelezo ya kesi hiyo, Bigambo amesema kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Septemba, 20, 2022 majira ya jioni katoka kijiji cha Kibubwa wilayani Butiama.

Amesema kuwa siku ya tukio mshtakiwa ambaye pia alikuwa ni jirani wa mwathirika alifika nyumbani kwao baada ya kubaini kuwa mama wa binti huyo hakuwepo na hivyo kuingia ndani moja kwa moja alipokuwa amelala binti huyo kisha kuanza kumbaka.

"Wakati anamaliza kufanya tendo hilo mama wa mwathirika naye akawa amerejea nyumbani ambapo alipiga kelele kuomba msaada. Hata hivyo, mshatkiwa aliweza kukimbia na kutokomea hadi alipokamatwa kesho yake eneo la Makutano akiwa anajiandaa kutoroka," amesema

Amesema kuwa katika shauri hilo jumla ya mashahidi watano akiwepo mama mzazi wa binti huyo pamoja na daktari aliyempima waliweza kufika mahakamani hapo na kutoa ushahidi ambao umeweza kumtia hatiani mtu huyo.

MWANANCHI
 
Angeenda Musoma vijijini kwa budget ya 150,000/ angerudi na mabinti watatu mabikira amewaoa

Kupanga ni kuchagua
 
SAFI SANA MAHAKAMA, KOSA LA MWEZI WA 9, KISHA HUKUMU IMETOKA MWEZI WA 11.
HUU NDIO UTENDAJI ULIOTUKUKA.

KWENYE MIAKA YA 2037, ATARUDI URAIANI
 
Back
Top Bottom