Musonda kumpisha Dube

Musonda kumpisha Dube

Analog

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2024
Posts
323
Reaction score
618
WAKATI Yanga ikiwa kwenye mchakato wa kusaka mbadala wa Joyce Lomalisa ambaye anatajwa kuachwa mwisho wa msimu huu, imebainika kuwa mshambuliaji Keneddy Musonda pia anampisha mtu.

Musonda anamaliza msimu wake wa pili mwishoni mwa msimu huu na hakuna mazungumzo yoyote baina yake na uongozi kwa ajili ya mkataba mpya na inatajwa kuwa atampisha Prince Dube ambaye anapambana kumaliza utata wake na waajiri wake wa zamani, Azam FC.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Mwanaspoti kuwa uongozi umefanya uamuzi wa kuachana na Musonda mwisho wa msimu na kuendelea na Joseph Guede ambaye ameanza kuonyesha uwezo huku akikiri kuwa wataongeza mshambuliaji mmoja.

"Mkataba wa Musonda unamalizika mwisho wa msimu ni kweli hakuna mazuingumzo mapya hii ni kutokana na uamuzi uliopitishwa na benchi la ufundi kuwa bora kubaki na Guede na kuongeza mshambuliaji mmoja mwenye jicho la kuona goli," kimesema chanzo hicho

"Tayari uongozi umeanza kufanyia kazi suala la kuongezwa kwa mchezaji eneo la ushambuliaji nafikili muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi sio wakati sahihi kuzungumza masuala ya usajili wakati bado tuna mechi za ligi ambazo kwetu ni muhimu zaidi ili kutetea taji."

Mwanaspoti linafahamu kuwa Yanga wamekuwa wanafukuzia saini ya Dube ili aweze kufanya kazi sambamba na Guede ambaye gari limewaka akitupia mabao kwenye kila mchezo na sasa amefikisha matano akimuacha Musonda mwenye mabao matatu, huku taarifa zingine zikidai tayari nyota huyo Mzibambwe ameshamalizana na Yanga na amekabidhiwa mkataba wa miaka miwili.

Dube amefikisha sakata lake la kutaka kuachana na Azam FC katika Kamati ya Sheria na Haki za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akipiga kuwa ana mkataba na timu hiyo wa miaka miwili ambao umebaki, huku akitaka mkataba uliobaki usiofika mwaka uvunjwe.

Wakati huohuo, mchezaji kiraka ndani ya Yanga, Farid Mussa anatajwa pia kuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika.

Farid hana namba chini ya kocha Miguel Gamondi tofauti, lakini alipokuwa chini ya Nasreddine Nabi alikuwa anamtumia katika maeneo mbalimbali kama winga na beki, na akawa anafanya vizuri.

Mwanaspoti lilipomtafuta Gamondi kuzungumzia ishu za usajili ndani ya kikosi hicho amesema sio muda sahihi wa kuzungumza nani anabaki au nani anaondoka kwa sababu ligi bado inaendelea na ana imani na wachezaji wake kuwa watatetea ubingwa.

"Tuna mechi zaidi ya tano unataka nizungumzie suala la kuondoka kwa wachezaji, sio sahihi na haiwezi kuwa na afya kwangu hasa kipindi hiki tunapambana kusaka matokeo ili tuweze kutetea taji la ligi," amesema.
 
Naomba kuuliza! Mbali na ufungaji dube anazo skills za kukaba? Anaweza kucheza namba tofauti na hiyo anayocheza ? Kama hajui kukaba basi aishie huko huko atachezea sana benchi.

Kocha Gamondi ni mtu wa mbinu nyingi sana hasa hasa timu pinzani ikipaki bus, si umeona jana kamtoa beki Job akaingia mzize acheze kama beki pia kama mshambuliaji, kamtoa Pacome kamuingiza mudathir kiungo mkabaji na mshambuliaji na timu ikapata matokeo!

Huyo Dube anazo skills za kupata namba Yanga? anamzidi nini musonda? Vipi kuhusu nguvu anazo? Humuoni Yao yao akisukumwa anapeperuka kama karatasi.

Dube ni soft sana, ni onana aliyechangamka spana mkononi.

Alafu Yanga usajili wake huwa ni wa kimya kimya angalieni msije mkawahi tena airport
 
Naomba kuuliza! Mbali na ufunhaji dube anazo skills za kukaba? Anaweza kicheza namba tofauti na hiyo anayocheza ? Kama hajui kukaba basi aishie huko huko atachezea sana benchi.

Kocha Gamondi ni mtu wa mbinu nyingi sana hasa hasa timu pinzani ikipaki bus, si umeona jana kamtoa beki Job akaingia mzize acheze kama beki pia kama mshambuliaji, kamtoa Pacome kamuingiza kiungo mkabaji na mshambuliaji na timu ikapata matokeo!

Huyo Dube anazo skills za kupata namba Yanga? anamzidi nini musonda? Vipi kuhusu nguvu anazo? Humuoni Yao yao akisukumwa anapeperuka kama karatasi.

Dube ni soft sana, ni onana aliyechangamka spana mkononi.

Alafu Yanga isajili wake huwa ni wa kimya kimya angalieni msije mkawahi tena airport
Yeah.... Musonda wasimwache.
 
Naomba kuuliza! Mbali na ufungaji dube anazo skills za kukaba? Anaweza kucheza namba tofauti na hiyo anayocheza ? Kama hajui kukaba basi aishie huko huko atachezea sana benchi.

Kocha Gamondi ni mtu wa mbinu nyingi sana hasa hasa timu pinzani ikipaki bus, si umeona jana kamtoa beki Job akaingia mzize acheze kama beki pia kama mshambuliaji, kamtoa Pacome kamuingiza mudathir kiungo mkabaji na mshambuliaji na timu ikapata matokeo!

Huyo Dube anazo skills za kupata namba Yanga? anamzidi nini musonda? Vipi kuhusu nguvu anazo? Humuoni Yao yao akisukumwa anapeperuka kama karatasi.

Dube ni soft sana, ni onana aliyechangamka spana mkononi.

Alafu Yanga usajili wake huwa ni wa kimya kimya angalieni msije mkawahi tena airport
Dube ana skills kuliko Musonda hii iko wazi...
Dube anaweza kufunga Goli kwenye angle ngumu rejea Goli alilowafunga Simba last season ni Outer moja matata Sana sijui Kwann alikua Goli Bora la msimu labda Kwa sababu wanaogawa tuzo n walevi.!

Kazi ya forward ni kufunga sio kukimbia kimbia hovyo kama swala aliyemuona Chui... Pamoja na Dube kua nje ya uwanja Kwa muda mrefu lakini hadi sahivi Dube ana Goli Saba ligi kuu huku Musonda ana Goli 3... Kumbuka Hadi msimu unaanza Musonda ndo alikua foward wa kutegemewa Yanga lakini Hadi alipokonywa namba na Mzize....

Dube n striker anayekupa uhakika wa Goli 15+ kwanini asiwe Bora kuliko Musonda asiyeweza kufunga Hata Goli tano Tu...

Naunga mkono hoja Musonda out Dube in...
 
WAKATI Yanga ikiwa kwenye mchakato wa kusaka mbadala wa Joyce Lomalisa ambaye anatajwa kuachwa mwisho wa msimu huu, imebainika kuwa mshambuliaji Keneddy Musonda pia anampisha mtu.

Musonda anamaliza msimu wake wa pili mwishoni mwa msimu huu na hakuna mazungumzo yoyote baina yake na uongozi kwa ajili ya mkataba mpya na inatajwa kuwa atampisha Prince Dube ambaye anapambana kumaliza utata wake na waajiri wake wa zamani, Azam FC.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Mwanaspoti kuwa uongozi umefanya uamuzi wa kuachana na Musonda mwisho wa msimu na kuendelea na Joseph Guede ambaye ameanza kuonyesha uwezo huku akikiri kuwa wataongeza mshambuliaji mmoja.

"Mkataba wa Musonda unamalizika mwisho wa msimu ni kweli hakuna mazuingumzo mapya hii ni kutokana na uamuzi uliopitishwa na benchi la ufundi kuwa bora kubaki na Guede na kuongeza mshambuliaji mmoja mwenye jicho la kuona goli," kimesema chanzo hicho

"Tayari uongozi umeanza kufanyia kazi suala la kuongezwa kwa mchezaji eneo la ushambuliaji nafikili muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi sio wakati sahihi kuzungumza masuala ya usajili wakati bado tuna mechi za ligi ambazo kwetu ni muhimu zaidi ili kutetea taji."

Mwanaspoti linafahamu kuwa Yanga wamekuwa wanafukuzia saini ya Dube ili aweze kufanya kazi sambamba na Guede ambaye gari limewaka akitupia mabao kwenye kila mchezo na sasa amefikisha matano akimuacha Musonda mwenye mabao matatu, huku taarifa zingine zikidai tayari nyota huyo Mzibambwe ameshamalizana na Yanga na amekabidhiwa mkataba wa miaka miwili.

Dube amefikisha sakata lake la kutaka kuachana na Azam FC katika Kamati ya Sheria na Haki za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akipiga kuwa ana mkataba na timu hiyo wa miaka miwili ambao umebaki, huku akitaka mkataba uliobaki usiofika mwaka uvunjwe.

Wakati huohuo, mchezaji kiraka ndani ya Yanga, Farid Mussa anatajwa pia kuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika.

Farid hana namba chini ya kocha Miguel Gamondi tofauti, lakini alipokuwa chini ya Nasreddine Nabi alikuwa anamtumia katika maeneo mbalimbali kama winga na beki, na akawa anafanya vizuri.

Mwanaspoti lilipomtafuta Gamondi kuzungumzia ishu za usajili ndani ya kikosi hicho amesema sio muda sahihi wa kuzungumza nani anabaki au nani anaondoka kwa sababu ligi bado inaendelea na ana imani na wachezaji wake kuwa watatetea ubingwa.

"Tuna mechi zaidi ya tano unataka nizungumzie suala la kuondoka kwa wachezaji, sio sahihi na haiwezi kuwa na afya kwangu hasa kipindi hiki tunapambana kusaka matokeo ili tuweze kutetea taji la ligi," amesema.
Siamini kama Yanga watamuacha Musonda. Bora wamuache Gift wasajili beki mzawa, wapo mabeki wazuri zaidi yake. Wamuache Skudu pia.
 
Dube ana skills kuliko Musonda hii iko wazi...
Dube anaweza kufunga Goli kwenye angle ngumu rejea Goli alilowafunga Simba last season ni Outer moja matata Sana sijui Kwann alikua Goli Bora la msimu labda Kwa sababu wanaogawa tuzo n walevi.!

Kazi ya forward ni kufunga sio kukimbia kimbia hovyo kama swala aliyemuona Chui... Pamoja na Dube kua nje ya uwanja Kwa muda mrefu lakini hadi sahivi Dube ana Goli Saba ligi kuu huku Musonda ana Goli 3... Kumbuka Hadi msimu unaanza Musonda ndo alikua foward wa kutegemewa Yanga lakini Hadi alipokonywa namba na Mzize....

Dube n striker anayekupa uhakika wa Goli 15+ kwanini asiwe Bora kuliko Musonda asiyeweza kufunga Hata Goli tano Tu...

Naunga mkono hoja Musonda out Dube in...
Huyo dube ameisaidia nini Azam? Miaka yote ni ya tatu na pia tuambie msimu uliopita alikuwa na magoli mangapi?
 
Nyie jichanganyeni tu yaani mumuache Musonda kisa Dube? mmerogwa na nani ? ndio yale yale ya kumuacha Moloko mkachukua Okra
 
Mimi binafsi katika wachezaji sioni kama wanafaa kuja Yanga ni Dube naona Yuko overated sana. Na kwa level za kariakoo tunahitaji watu wa maana sana sasahivi
 
Kivyovyote Musonda sio wa kuachwa, msimu umemkataa ila ni striker mkali.
Apewe nafasi.
 
Atoke okrah abaki musonda.
Okrah hajatoa mchango wowote ndani ya yanga zaidi ya kukimbia tu bila plan na krosi za hovyo.
Musonda bado Ana mchango mkubwa kwa yanga angalia pressing yake dhidi ya Al ahly, simba 5-1 na mamelodi .
Mchango wa musonda unazidi wa okrah .
 
Back
Top Bottom