Mussa Azzan Zungu: Serikali iangalie upya mikataba ya Wakandarasi wageni

Mussa Azzan Zungu: Serikali iangalie upya mikataba ya Wakandarasi wageni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ameishauri Serikali kuangalia mikaba na kusaidia Wakandarasi wazawa kupata nafasi pia katika miradi mbalimbali, ametoa ushauri huo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt.Festo Dugange wakati wa Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 13, leo Februari 13, 2025
 
Anawasemea wakandarasi wapi?

Hawa wanaojenga miradi chini ya kiwango hadi aibu? Hawa ambao wakipewa mradi ndo hawaonekani site?
 
Anawasemea wakandarasi wapi?

Hawa wanaojenga miradi chini ya kiwango hadi aibu? Hawa ambao wakipewa mradi ndo hawaonekani site?
Mkuu ukijenga Nyumba yako mwenyewe basi unaweza kumwambia fundi unavyotaka kujengewa. Nae fundi hujenga kwa malipo yako, uhuwezi kulipa million 200 halafu utegemee uimara wa Nyumba ya million 500.
 
Anawasemea wakandarasi wapi?

Hawa wanaojenga miradi chini ya kiwango hadi aibu? Hawa ambao wakipewa mradi ndo hawaonekani site?
tutafanyaje ndiyo tikiti bovu lipo shambani mwako!
Tutiane moyo na tukosoane kwa hekima huenda hawa makandarasi wetu wakafanya vizuri katika kujenga taifa letu.
 
Hizi kauli kila mwaka wa uchaguzi utazisikia uchaguzi ukisha tu utosikia tena kauli kama hizi.
Tuwakumbushe hawa viongozi wetu, kwani wao ni binadamu, wakizingua nasi tuwakumbushe wapiga kura kutokana na madudu yao.
 
Back
Top Bottom