Mustakabali wa benki ya Barclays

Governor of Bettors-GB

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
10,568
Reaction score
9,710
Wakuu hembu wenye kujua hili watupe habari.
Hili nimeliona muda mrefu na pia Kuna updtae nimezipata hivi karibu nazimekuwa zikiendelea kutokea

.
Kwanza ni Miongoni mwa BANK ninazozikubali sana kwenye huduma,na msaada kwenye tataizo.Wanasaidia sana pindi mteja anapokuwa na Tatizo.Pongezi sana kwa Staffs wa Barclays bank hili mpo vizuri sana.Hili pia nimeliona pale CRDB

a)Matawi Kufungwa


Matawi mengi sana yalifungwa na accounts kuhamishwa matawi mengine,kwa Zanzibar kisiwa cha Pemba kama sikosei nako tawi lilifungwa nakufanya Pemba kutokuwa na Bank hii na wakati watu walifungua accounts zao,sasa kwa maana hiyo wakitaka kutoa pesa mpaka wapande ndege au boat kuja Zanzibar,hii kali.
Upande wa Unguja ipo vizuri tawi la Darajani na Kinazini makao makuu wapo safi,kufungwa kwa tawi la Mwanakwerekwe sio tatizo maana sio mbali na matawi mengine.

b)Wafanyakazi kupunguzwa


Wafanyakazi wengi sana wamepunguzwa kazi,hii imekuwa ikiendelea kila kukicha,maana kuna sehem unakuta umeenda mwezi uliopita ukirudi mtu amepungua na mwingine kahamishwa kuziba gepu kwingine.Tunajua kwamba Teknolojia ya Ma Bank imekuwa kwa kasi sana na kufanya kutokuhitaji wafanyakazi wengi,lakini hapa kuna kitu.

c)Kuhusu ku deposit
Hii imekuwa tata baadhi ya Branches na hata Kenya niliiona pia kwamba wanataka mtu awe na account kwao ili afanye transfers na sio Cash Deposit,ila baadhi ya matawi au hata baadhi ya wafanyakazi pia huweza kumsaidia mtu na kumruhusu ku deposit kwa mtu mwingine bila kuwa na account kwao ili iwe transfered.Hapa Tata kidogo

d)Mfumo unaokuja wa malipo.
Hii nimeipata,kwamba wanaanzisha mfumo wa Cheques,yaani hata kama unatoa lazima utumie cheque,sasa hii kwa sasa inapotezewa ila nasikia kwamba ikifika muda itazuiliwa ili ukitaka kutoa hata kama ni wewe mwenyewe unaandika cheque.
Sasa najiuliza hiyo bank si itajaa makaratais?na ile Leaf moja ya bank inalipiwa pesa.Hapo vipi

e)Mikopo

Habari zilizoo ni kwamba wamezuia Mikopo kipindi kirefu sana,yaani hakuna mikopo tena.Sijui kwa wakumbwa mlango wa nyuma

f)Overdrafts
Hii ilikuwa kwa watu maalum tu,na imezuiliwa tena hakuna tena,ila kwa masharti ya kuwa na zaidi ya 50m na uiweke kwao kwa muda wa miezi sita ndio upate access ya overdraft na kwa muda maalum.
Maana nasikia overdrafts ilikuwa na ni kwa majeshi ila na wao pia wameziwiliwa kitambo sana.So,hakuna huduma hii

Wakuu hizi issue nimezisikia na kufuatili muda kiasi,ila bado kila muda utata unazidi.


Wenye kujua zaidi wafunguke
 
Kwa maelezo uliyo yatoa hayo yote, hashwa la kupunguza wafanyakazi, kuzuia overdraft, na kufunga baadhi ya branch, naomba nikutume yafutayo utuletee apa janvini tutapata jibu zuri.

1.Tafuta kama unaweza kupata Current Financial report angalau ya mwaka jana ya benk yao. sijajua kama waliitoa gazetin au la, ukituletea hiyo. Tuta angalia kwenye BALANCE SHEET tuone liabilities zao zina uiano gan na Asset zao.
Lakini pia tuta angalia walipata profit au loos!!!

Kwa mtazamo wa haraka naona kama siyo mabadiriko ya tecknologia nahisi wana operate under loss!! na hii wanavyo fanya uenda ni recomandation za auditor waweze ku-minize cost na angalau ku-max mize profit. Jaribu kufanya hivyo mimi binafusi nikiiona hiyo report nitapata cha kuchangia mkuu.

Ila ushauri wa haraka wa bure, Ukiona mwenzio ananyolewa saloon, wanasema na wewe andaa kichwa tihari. nafikiri kama vip wewe anza pia kufikiria ni benk gan unaweza kuhamishia fedha yako
 
Kwa kufunga matawi kwa Zanzibar ni kwa sababu ya kuyumba kwa uchumi ulaya. Maana Zanzibar waliweka matawi mengi kwa sababu wazungu (watalii) wengi hutumia bank zao ila kwa uchumi kuyumba na watalii wamepunguza spendings na sekta ya utalii Zanzibar imebinafsishwa sasa inaendeshwa na sekta binafsi na sio zanzibar commision of tourism.

kiasi kwamba watalii wengi wanaoingia Zanzibar huwa wameshafanya malipo yao yote huko ulaya waliko maana yake haitaji tena kutoa pesa nyingi akifika huko Zanzibar.

Kwa ishu ya Pemba miaka kama mitano iliyopita kulikuwa na uwezekano wa kuboresha utalii Pemba. Ila siku zinavyokwenda uwezekano huo kama haupo na mji ule kuwa na watalii wa kudunduliza kufungua tawi katika mazingira hayo ni hasara tupu maana wenyeji wengi sio wapenzi wa bank hiyo.

kwa ujumla hao jamaa kwa Zanzibar walilenga wazungu na wameona hakuna haja ya kuwa na matawi kama kwerekwe maana wazungu hawafiki huko.
 

Shukran mtaalam felix,ngoja nikiipata nitakutumia maana kwenye gazeti sidhani kama waliitoa.
Ila ushauri wako pia ni mzuri nauzingatia.
Ubarikiwe
 
Mtaji Tumbo nakuabaliana na wewe.
Nikweli Target ya Bank hii ilikuwa ni Utalii,na hata ATMS zao ukienda ya pale Darajani au head office wazungu kibao kuliko sie.
Hizi Banks sasa hata mtu hujui ufanyeje sasa.

Kuna mtu aliwahi kuniambia kwamba Local Banks ndio zakukimbilia maana hakuna Local Bank iliyowahi kupata tatizo kulinganisha na hizi za kigeni kila siku linazuka jipya.
 
Hiyo bank last week niliona kwenye news kati ya BBC au CNN ikipigwa faini kule USA kwa makosa ya kiufundi,vilevile hata waliomba kupatiwa support na serikali yao huko UK,nadhani kuna tatizo.
 
Sorry wakuu hyo overdraft maana yake nini
 
Sio kweli kuwa wanafilisika. Kwa ufupi ni kuwa wanataka kuwa corporate bank,corporate wana withdraw kwa cheque pekee,lakin pia siku hz cheque imekuwa na matumizi na secure zaidi Standard charterd nlifungua a/c pale wakanipa na cheque book.
 
Hizo product wanazo; Personal Banking; Presitage Banking; Corporate Banking and Premier Banking.
 
Nilikuwa nawaza sana kufungua account kwao
 
Ungana na wenzio walioshitukia haya mabenk yanayopitia mambo tata kuhama. DTB nako wateja wanahama kwa kasi inayohatarisha msitakabali wake miaka miwili ijayo mbele. Hofu ya kupoteza amana na kuanzishwa masharti mapya baada ya kukubwa na kashfa ya ugaidi. Hali hii pia inaikumba NBC ingawa wao wamepmbana sana kuinasua isifilisike ila bado haijakaa sawa ingawa hali si mbaya sana. Kwa upande wa znz kama utalii ukitikisika znz ni sawa benk kuyumba kwan waznz wengi huficha pesa ndani na wachache ni wazalendo kwa benk yao PBZ. mobile money service nazo zinayumbisha mabenk kwa sasa. Benk salama ni zile zenye idadi kubwa ya wateja wafanyakazi sina haja ya kuzitaja.
Nikutaadharishe kuwa kuokoa bank ni.kazi sana hvyo mtegemee mabadiliko na ukiritimba kuwazuia angalau mchekewe kuchukua amana zenu ili bank iiende. Kwa taarifa hata ulipaji mishaara umekua na tabu kidogo bank hii. Pia overtime zimekua zikikwepwe kwa kadr iwezekanavyo. Bank iko hatarini chukua hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…