Mustakabali wa elimu yetu ni upi?

Mustakabali wa elimu yetu ni upi?

successiful dreamer

Senior Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
103
Reaction score
191
Habari ya uzima wanajamvi? Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya.

Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu ya msingi. Mimi ni mdau wa elimu nimekua nikifatilia kwa kiasi mijadala inayohusiana na elimu ya nchi yetu kwa kipindi kirefu sana bila kupata majibu sahihi.

Kinachoniumiza zaidi ni jinsi mfumo au mtaala wa elimu yetu usivyokuwa na mwelekeo sahihi wa kumjenga kijana wa Kitanzania kuitumia elimu anayoipata mashuleni na vyuoni katika maisha ya mtaani baada ya kupata elimu.

Elimu yetu haina kipimo sahihi cha kuonesha uwezo walionao wasomi wetu zaidi ya vyeti vinavyotolewa na taasisi zetu za elimu kama shule na vyuo. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wataalamu wasio na umahiri katika taaluma zao kwani wengi wakiwa masomoni wanalazimika kukariri na si kuelewa kile kinachofundishwa kwa undani wake.

Mwanafunzi wa chuo yuko radhi akose lectures lakini ahakikishe anapata notes akariri ajibu test na UE peke yake akitoka kwenye mtihani ukimuuliza swali lolote kati ya aliyoyajibu kwenye mtihani baada ya siku moja hawezi kukujibu chochote.

Ukifika mda wa kuajili kila mwajili anatafuta mtu mwenye vyeti vizuri lakini mwenye vyeti hivyo kimsingi alivipata kwa kukariri wengine waanahonga rushwa ya ngono kwa wakufunzi ili wafauru mitihani hivyo Basi kigezo cha kupima ubora wa taaluma ya mtu kwa kutumia vyeti kwa kiasi kikubwa mimi sikiamini. Matokeo ya kupima uwezo wa mtu kupitia njia hii ni mabaya mno kwani tumejikuta tukiwa na wataalamu feki wanaoharibu kazi na kuliingizia taifa hasara kila uchwao.

Kwa mtindo huu sisi kama taifa tunaenda wapi kama hatuwezi kubadili mfumo wetu wa elimu ili uje kuleta tija zaidi katika nyanja tofauti tofauti kuliko kutengeneza wataalamu waliokariri na kupendezesha vyeti vyao huku kichwani kukiwa hamna kitu?

Mstakabari wa elimu na taifa letu kwa ujumla ni upi? Wapi tunakoenda kama taifa au tuendelee kuwapa heshima wataalamu wa kigeni katika mambo ya muhimu kama afya na teknolojia?
 
Mijadala hii huwa inanoga kama ungeweka na kilinganishio cha mfumo mwingine ambao unatoa matokeo tofauti na huu wa kwetu.
 
Unachokiongea ni sahihi mm ni mdhibiti ubora ,kitaalamu na ndio kazi yangu hayounayoyasema yanaukweli ,mitaala yetu haiwafanyi watu wanapo hitimu wajitegemee....,ni wazi kabisa ....kwenye Elimu yetu panahitajika mapinduzi makubwa,leo ukilinganisha wahiimu wa vyuo vikuu vya kenya na Tanzania ukawawekapamoja wakenya watawahi kuziona fursa , watu wengi Tz wakihitimu wanawaza ajira

sent from HUAWEI
 
Back
Top Bottom